New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Chanjo ipi?
millardayo_20210705_191911_5.jpg
 
We project from TODAY going forward every leader who misleads the general public about the importance of constitutional reforms will die from HIV & AIDS and Covid-19 complications so do not strive with dead men walking.

The choice is stark clear so which choices are you gonna make: speak the gospel truth and live or lie and die?

I choose the former option

Ukitaka kumfuata shujaa wa Chato aliko endeleza dhuluma zake hutakawia kuishia kusikojulikana na tutakuita mwendazake

millardayo_20210705_191911_7.jpg
 
Bunge "dhaifu la Ndugai" limekubali kwa kauli moja maombi ya serikali ya kuongeza kodi ya TSZ 100/= kwenye kila lita moja ya mafuta kama chanzo kipya cha mapato.

#SWALI: Je, kulikua na ulazima wowote wa kuongeza TZS 100/= kwenye bei ya mafuta katika bajeti ya mwaka huu?

#Jibu ni HAPANA kwa sababu zifuatazo;

1. Kutatokea mfumko mkubwa wa bei za bidhaa na huduma kwa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta. Nauli za mabasi zitapanda, bidhaa za viwandani na mashambani zitapanda pia. Kama Parachichi kutoka Sanya juu liliuzwa TZS 1,000/= hapa Dar, sasa litauzwa 1,500/= kwa sababu gharama za usafirishaji zimeongezeka.

2. Kabla ya July 1, serikali ilikua inakusanya kodi ya TZS 580/= kwa kila lita moja ya mafuta (VAT, Excise duty, Railway levy etc). Kwahiyo serikali kuongeza TZS 100/= inafanya kwa sasa ikusanye 680/= kwa kila lita moja ya mafuta. Huu ni unyang'anyi usiotumia silaha.

Bunge lisingekua DHAIFU lilipaswa kukataa mapendekezo ya serikali ya kuongeza 100/= kwa sababu tayari inachukua 580/= ambayo ni kubwa kuliko faida wanayopata wamiliki wa vituo vya mafuta. Ukijenga kituo cha mafuta, ukalipa wafanyakazi, umeme, maji, ulinzi, etc unapata faida chini ya 100/= kwa lita, lakini serikali ambayo haijakusaidia hata kupaka rangi inakomba 580/= kwa kila lita unayouza. Na kuanzia jana (July 1) itakua inachukua 680/= kwa kila lita. What a shame?

3. Hii nchi ina vyanzo vingi vya mapato kama tukiwa wabunifu, hivyo hatuna sababu ya kung'ang'ania vyanzo vinavyomuumiza mwananchi. Mauritius inaingiza $10 Bil (TZS 23 trilion) kutokana na utalii wa fukwe (Beach tourism), lakini sisi kwa mwaka uliopita wa fedha tuliingiza $2.4 Bil (TZS 5.4 trilioni) kwa utalii wote kwa ujumla.

Yani Mauritius imetuzidi mapato ya utalii mara 4 wakati wanategemea fukwe tu. Sisi tuna fukwe, mbuga za wanyama, mapori ya akiba, mlima Kilimanjaro, Bonde la ufa, Michoro ya mapangoni, kaburi la mwendazake etc lakini tumeachwa mbali kimapato. Tukiwekeza vizuri kwenye sekta ya utalii na sekta nyingine tunaweza kupata fedha nyingi zaidi kuliko kuwaumiza maskini kwa kuwaongezea kodi kwenye mafuta.

4. Ni aibu nchi za jirani zinazopitisha mafuta hapa kwetu wanauza bei ya chini kuliko sisi. Lusaka bei ya Petroli ni Kwacha 15.60 sawa na TZS 1,700/=, Kinshasa Franc 1,800 sawa na TZS 2,087/=. Dar es Salaam ni TZS 2,500/=. Hii ni Futuhiii. Ndio ni Futuhi.!

5. Bei ya mafuta katika soko la dunia imeanza kupanda kwa kasi, kwahiyo hakukua na sababu yoyote serikali kuongeza tena kodi kwenye mafuta. Mwezi June mwaka jana bei ya mafuta ghafi (crude oil) katika soko la dunia iliporomoka kutokana na athari za Covid19 hadi kufikia $40.1 kwa pipa. Hili ni anguko kubwa sana la bei kuwahi kutokea. Lakini anguko hilo lilitufaidisha sisi nchi maskini kwa sababu bei ya Petroli ilishuka hadi 1,800/= kwa lita.

Sasa hali ya Covid19 imeanza kutengemaa huko Ulaya na nchi zilizoendelea baada ya kuchomwa chanjo. Hata viwanjani mashabiki wameanza kuruhusiwa kuingia. Kwahiyo bei ya mafuta imeanza kupanda tena. June 21 mwaka huu bei ya pipa la mafuta ghafi imefika $74.3 na wataalamu wanasema itaendelea kupanda. Kwahiyo December inaweza kufika $100.

Serikali yetu ingekua na akili, ilitakiwa kufanya simple economic anticipation, kwamba huko duniani mafuta yanapanda bei, kwahiyo kuongeza kodi ya TZS 100/= ni kuongeza mzigo usiobebeka kwa mwananchi. Jiulize kama bei ya pipa kwa sasa ni $74 na tunauziwa 2,500/= kwa lita, je ikifika $100 tutauziwa bei gani kwa lita?

Kama serikali ingeangalia trend ya dunia ilitakiwa iachane na mpango wa kuongeza kodi kwenye mafuta ili huko mbeleni iweze kufanya "adjstment" ya kumlinda mwananchi kama bei ya soko la dunia ikizidi kupanda.

Lakini Serikali imeshindwa ku-anticipate phenomenon rahisi kama hii ya uchumi. Hii ni assignnent ya mtoto wa First year, Introduction to Macro Economics (EC102) pale SAUT, UDSM au Mzumbe. Lakini imemshinda Rais ambaye ni Mchumi, Makamu wake ambaye ni daktari wa uchumi, Waziri wa fedha ambaye ni Mchumi mwandamizi. Wote wamekula Supp. Shame.!

Malisa GJ
IMG-20210706-WA0020.jpg
 
Back
Top Bottom