New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Nobody knows for sure what happened to the founder of WAGNER.

Everything else is speculation and conspiracy theories.
 
BRICS is a game changer. Hatuhitaji mwekezaji wa aina yeyote bandari zetu.

Ukiwa ndani ya BRICS biashara ya bandari huhitaji kuwa pembezoni (satellite) kwa waarabu kama huu mkataba wa DP WORLD.

Hata kama watawala ni wasaka tonge heshimuni utu wa mtanganyika huu mkataba wa DP WORLD unatudhalilisha mno.

Unatufanya tujione na hivyo tuonekane hatuwezi kitu wakati siyo kweli.

Tatizo letu tangu tupate uhuru tumeshindwa kubuni mfumo utakaoibua vipaji vya uongozi bora na tumeishia na mawakala wa ukoloni mamboleo
 

Attachments

  • PSX_20230825_090750.jpg
    PSX_20230825_090750.jpg
    133.2 KB · Views: 2
Kuwa Rais wa nchi hakumaanishi utafanya utakavyo bali utaheshimu utu wa unaowaongoza.

Utawapeleka wanakotaka kwenda siyo unakotaka kwenda wewe.

Wengi wape au watajichukulia.
Ukitaka kwenda mbali nenda na wengi walakini ukitaka mwendo wa kasi basi nenda peke yako
 
Maamuzi ya mahakama kuu ya Mbeya tumeyakataa kwa sababu yanadhalilisha katiba na sheria za nchi hii.
 
Uamuzi tajwa umeikana katiba maeneo ya usawa, haki, uwajibikaji, ufuataji wa sheria zitungwazo na bunge na Dubai kukosa sifa ya kuingia katika mikataba ya kimataifa
 
Dubai siyo signatory au mwanachama wa makubaliano ya Lome na Geneva.

Hivyo, hawawezi kuingia mikataba ya kimataifa na kunufaika nayo.

Mahakama kuu Mbeya imepinga hilo sasa tuna mahakama au kijiwe cha kulangua haki za wanyonge?

Aidha, kinyume na sheria za mikataba ya kimataifa, Mahakama Kuu Mbeya iliwahalalisha Dubai kuwa wana sifa ya kuingia mikataba ya kimataifa kwa kutumia katiba ya Falme za Kiarabu ambayo haihusiki. Walipaswa kujiongoza vizuri kwa kutumia orodha ya wanachama wa makubaliano ya Kimataifa ya Lome na Geneva.
Hawakufanya hivyo siyo kwamba hawajui bali kwa makusudio mazima ya kuhalalisha maliasili za nchi ziporwe na watawala wetu kwa mgongo wa mwekezaji.

Swali lililobaki la kujiuliza hawa majaji walinufaikaje? Tutalijibu hili swali siku za usoni. Hatuwezi kulifumbia macho hata kidogo!
 
Mahakama kuu Mbeya imebatilisha katiba na sheria zilizopitishwa na bunge ili kuhalalisha Azimio la bunge ambalo limetengua sheria za manunuzi, mikataba na uthibiti wa maliasili!
 
Kisingizio cha Mahakama Kuu ni huo mkataba ni wa kimataifa wakati siyo wa kimataifa na hata ungekuwa ni wa kimataifa hauwezi kuwa juu ya katiba yetu
 
Sheria zetu ni tunda la katiba yetu kama sheria zetu siyo walinzi wa maliasili zetu sasa hizo sheria ni za nini na katiba ni ya nini
 
Kama mikataba ya kimataifa inaweza kutengua katiba na sheria zetu sasa misingi ya usawa, ushindani na uwazi iliyomo kwenye katiba na sheria zetu kawekewa nani kama siyo mahakama inakuwa kichocheo cha uporaji wa mali za umma?
 
Maamuzi ya namna hii ambayo yanatengua katiba na sheria zetu yanaleta maswali mazito hawa majaji walipatikanaje maana hawana sifa hata ya kuwa mahakimu wa mahakama ya mwanzo
 
Tulizoea mahakama kuu kuwa watetezi wa haki za kikatiba na tulikuwa na shida na mahakama ya rufaa kutengua haki za kikatiba sasa hatuna muhimili unaojali katiba au sheria zetu
 
Swali ambalo mahakama zetu kamwe haitakaa kulijibu ni sheria zipi sasa zitumike kulinda maliasili na utajiri wa nchi hii kama katiba yetu na sheria zake hazihusiki?
 
Ni vyema tukaanza kutafakari mfumo mwingine wa ajira za mahakimu na majaji kwani huu mfumo uliopo kamwe hautatutendea haki.
 
Tutakuwa tunatumia hela nyingi kuwagharimia majaji mafisadi na ambao watabandikwa hapo kunadi haki za wanyonge na kutoa maelezo ya kipuuzi kabisa kama huu uamuzi wa Mahakama kuu ambao umeihalalisha DP World kumiliki bandari zetu bila hata ya kutoa senti moja
 
Kulingana na sheria za mikataba zetu ni lazima mkataba uwe na haki na wajibu. Mkataba hauwezi kuegemea au kupendelea upande mmoja wa mkataba huo mkataba ni batili.
 
Huu wa DP WORLD mwarabu ana haki zote na hatakiwi kufanya lolote ili kuzipata haki miliki za bandari zetu.

Mazingira ya namna hii ni ukiukwaji wa sheria zetu za mikataba lakini mahakama kuu ikasema sheria tajwa haihusiki!!!!!!

Eti sababu yao walidai huu ni mkataba wa kimataifa wakati hauna sifa ya kuwa mkataba wa kimataifa na hata ungekuwa siyo kigezo cha kutengua sheria zetu ambazo kulingana na katiba yetu ndizo zinatawala usimamizi, uendeshaji na umiliki wa mali za umma.

Yaani hata hawakutaja kanuni za mikataba ya kimataifa inayowaongoza wajibu bila haki ndiyo mwendo mdundo.

Mikataba ya kimataifa ni sawa tu na sheria zetu ambazo msisitizo ni haki na wajibu siyo uonevu kama huu mkataba feki
 
Mahakama ikadai tunywe mtori kwanza na minofu tutakutana nayo chini kwenye mikataba midogo midogo.

Mikataba midogo midogo inatoka wapi kama babalao ni batili?
 
Kama ingelikuwa ni hivyo walipaswa kusema haikuwa sahihi kwa haki za upande mmoja kubainishwa bila wajibu pia kubainishwa.

Aidha vyote (wajibu na haki)viondolewe kwenye mkataba au vyote viwekwe.

Ni mahakama gani haioni noma kwenye swala wazi kama hili kama hawajatiwa mfukoni?


Hili tu lilitosha kutengua Azimio la bunge la kifisadi
 
Back
Top Bottom