New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Baada ya hii risala kesho nisikie baragumu la shinikizo la katiba mpya maana nchi inaenda vizuri mno.


MAMA SAMIA ANAYETUKANWA NA WAPINZANI NI HUYU?

Na Thadei Ole Mushi.

Ndiye Rais ambaye Alihakikisha Lisu amepata haki yake ya kutibiwa na haki zake za kibunge alizokuwa amedhulumiwa.

Ndiye Rais ambaye amekubali kuwaita wapinzani Ikulu na kuongea nao kuhusu mambo mbalimbali ya Kisiasa nchini hapo kabla hili halikuwezekana.

Ndiye Rais anayejitahidi kuajiri kuliko Marais wengine wote waliomtangulia.

Ndiye Rais ambaye kuingia kwake madarakani hakutaka kuanzisha miradi yake anapambana kukamilisha miradi yote ya Mtangulizi wake kwa mara ya kwanza tunaona Continuity kati ya Rais mmoja na mwingine.

Ndiye Rais aliyevitoa vyombo vyote vya habari Gerezani na kuviruhusu kuandika wanavyotaka.

Ndiye Rais aliyehakikisha waliokuwa wametupwa lupango kwa sababu za kisiasa na kiuchumi kama kina mzee Rugemalila wanatoka na wapo uraiani.

Ndiye Rais ambaye anapambana Sector Binafsi itoke ilikokuwa imefukiwa ifanye kazi sambamba na serikali.

Ndiye Rais ambaye hakusanyi kodi kwa kutumia kikosi Kazi wala mabavu.

Ndiye Rais ambaye unaweza kumwambia akili zake ni matope lakini bado akavumilia na ukaendelea kula Ugali wako Uraiani.

Ndiye Rais Ukanda huu wa Africa unaweza kumwambia anafuga wezi na akakuacha ukaendelea kula ugali wako Uraiani.

Ndiye Rais ambaye baada ya Kuingia madarakani aliwaondolea watumishi kifungo cha kutokupanda madaraja kwa wakati na sasa kila mtu anapanda kila anapostahili.

Ndiye Rais ambaye aliwafungulia kina Mbowe account zao zilizokuwa zimefungwa na kuwarejeshea haki zao.

Ndiye Rais ambaye kuingia kwake madarakani wasiojulikana nao walikwenda kusikojulikana.

Ndiye Rais ambaye alitufutia Retention Fee sisi wanufaika wa Bodi ya Mikopo na mikopo yetu kumalizika kwa wakati.

Ndiye Rais ambaye ameweza kuleta tofauti ya maendeleo ya vitu na watu kwa kusogeza huduma za kijamii kadri anavyoweza kwa wananchi.

Ndiye Rais aliyefuta ada kwa vidato vya tano na Sita.

Ndiye Rais ambaye amepandisha kiwango cha fedha za wanufaika wa Mikopo na kuongeza wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Ndiye Rais nwenye uwezo wa kuhimili wakosoaji wake kuliko watangulizi wake.

Ameichukua nchi ikiwa imetoka kwenye Wimbi kubwa la Corona ila Uchumi haukuyumba, wananchi hawakukosa chakula ulizeni majirani athari za Corona watawaambia.

Kwenye miundombinu ya Barabara, Madarasa, Vituo vya Afya na Huduma za Maji safi na Salama amevunja Rekodi.

Binadamu tuna tabia za kusahau, kwa sasa tushasahau yote haya, huyu ndiye Rais tunayetakiwa tumeombee adumu nasi. Huyu ni mama haswa. Sio mtu dhaifu, mtu dhaifu hana uwezo wa kuvulia hivyo, kupitia taasisi yake anaweza kufanya mengi kama ambavyo watanguluzi wake walifanya. Kuna siku tutamtafuta kiongozi kama huyu tutamkosa.

Ni miaka miwili tu madarakani lakini katurudishia kila kitu tulichopoteza.

Ole Mushi
0712702602
 
The speech of Madam president today has given new hope of abiding to the rule of law and good governance which activists were clamouring for years.

We are beginning to see commitment to the rule of law and good governance after the rights of whistle blower will be restored. No more incitement to be used to clamp down freedom of speech and expression.

Without freedom of speech and expression the fight against official graft is lost even before it started because in opaque graft thrive unimpeded.

We are planning to follow closely the challenges and achievements of this new administration without biasness in the next four years or so.

As usual we will attempt to focus in the rule of law and good governance.
 

Attachments

  • VID-20220524-WA0084.mp4
    2.9 MB
Tuna chama cha change au kwa kiswahili kinaitwa ni chama cha mapinduzi 😃 😀 😄 😁 🤣 😂 😃
 
Unyenyekevu kwa viongozi wa Afrika siyo mila wala desturi yao.
 

Attachments

  • IMG-20230916-WA0026.jpg
    IMG-20230916-WA0026.jpg
    49.1 KB · Views: 1
Catching masterminds of drug cartels really not a game changer because Fentanyl is not locally produced. It is smuggled from China where its production capacity is entrenched and waxing strong.

Picking chief players who are basically international couriers in the drugs circulation interferes with nothing albeit we must concede it smacks of spectacular symbolism akin of the assassination of ailing Osama Bin Laden which was more of vendetta than fixing international terrorism.

The fight against illicit drugs is spiritual and like all spiritual wars they are not subdued by flesh and blood but by the armour of God which is exclusively in His word.

The more we commit sexual immorality the more we shall rummage for carnal ecstacy, the unquenchable exhilaration and its associated crimes to fund the addiction.
 

Attachments

  • PSX_20230916_215423.jpg
    PSX_20230916_215423.jpg
    133.5 KB · Views: 1
Maadili na utamaduni wetu unaruhusu wizi wa kura au kukataa kuheshimu haki za mpigakura?


Hallo Bern,

Hili ni andiko langu refu tangu nijuinge hapa na inawezekana la kwanza na la mwisho. Sijui.

J5 nilichangia andiko lako la J4 na kuahidi kuchangia hili jambo la MAADILI YA MTANZANIA kwa lengo la kuelimishwa, haya maadili ya Mtanzania ni yapi?

Katika hotuba ya Mhe. Rais wetu, nadhani siku ya Jumanne, tarehe 12.09.2023 alisisitiza sana juu ya maadili ya Mtanzania.

Katiba hotuba yake, Mhe. Rais wetu alitumia maneno mengi kwa muktadha wa maadili kwa kuchanganya na kingereza ambayo ni – utamaduni wetu, Mungu kawaumba Watanzania na roho rahimu, Mungu kawaumba Watanzania na sifa za pekee, Watanzania tumeachiwa misingi na Waasisi wa taifa letu, Watanzania tuna quality za pekee yetu, tuna mila zetu, tuna desturi zetu, mambo yetu ya Kitanzania, tuna values, ethics, moral standards zetu, utu, heshima kila nchi ina zake, utu wa mtu lazima uheshimiwe, heshima ya mtu, hali ya mtu, utovu wa adabu, hatuwezi kupokea toka nje, mmomonyoka wa maadili, morality and ethical standards, kuna kilio cha mmomonyoko wa maadili, Watoto wanatupotea, vyama vya siasa vikadhibiti mmomonyoka wa maadili ya vijana/Watoto wetu, n.k.

Mimi naandika andiko hili kwa lengo kuu moja tu la kutaka kuelimishwa kwa kuuliza swali au maswali au kwa tafakuri yangu ifuatayo, hivi maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Mimi nimeishi nje ya Tanzania kwa miaka 12 mfulilizo na nimetembea dunia hii si haba na naweza kusema baadhi ya desturi za nchi zilizoendelea ambazo nimebahatika kuishi na kuzitembelea. Naweza kuzitaji baadhi ya desturi zao kama ifuatavyo:
1.Wanajali muda
2.Wanatimiza wajibu wao (si wavivu, ni wachapa kazi)
3.Wanaishi neno akutamkialo
4.Wanapanga foleni sehimu zote zenye watu wengi – kwenye huduma za usafiri, maduka, benki, nk
5.Wanapisha kwenye viti wakae au wapite mbele ili wapate huduma kwanza wajaozito, wenye watoto, wagonjwa, vilema, wazee, nk.
6.Ni wakweli (si matepali). Hii haitofautiani na desturi Na. 3 hapo juu.
7.Ni wasafi kwa maana hawatupi ovyo uchafu wao.
8.Ukiendesha gari vibaya barabarani, dereva mwenzako aliyekuona na mwanachi yo yote hupiga simu polisi na mara moja utaona gari ya kimuli muli ya polisi inakusimamisha na kukuhudumia.
9.Unalala usingizi wa pono, wala huna waswasi wa vibaka.
10. Kelele nazo kwao ni uchafuzi wa mazingira,
11. Katika familia zao, wana nidhamu ya kuangalia picha za luninga. Kuna picha ni marufuku kuangalia watoto, nk
12. Wanapotoka nje (outings) za kirafiki, kila mtu anajitegemea.
13. Nk

Kwa hiyo, bila wasiwasi unaweza sema haya ni maadili au mila au desturi au utamaduni wa baadhi ya nchi ambazo mimi niliishi na kutembelea. Watakushangaa ukifanya kinyume yake na kama ni barabarani, polisi watakuhudumia.

Sasa, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Mimi ni Mtumishi wa Umma mstaafu ingawa bado naendelea kutumikia umma kama Mhadhiri. Naleo Watoto/vijana wenu na nashuhudia mengi sana juu ya maadili ya si vijana wetu na yetu sisi wenyewe kama Wahadhiri.

Je, kutojali muda ndio maadili ya Mtanzania?
Je, kutotimiza wajibu (uvivu) ndio maadili ya Mtanzania?
Je, kutoishi neno ulitamkalo ndio maadili ya Mtanzania?
Je kutopanga foleni sehimu zote zenye watu wengi – kwenye huduma za usafiri, maduka, benki, nk ndio maadili ya Mtanzania?
Je, kutopisha wakae kwenye viti au wapite mbele ili wapate huduma kwanza wajaozito, wenye watoto, wagonjwa, vilema, wazee, nk ndio maadili ya Mtanzania?
Je, kutokuwa wakweli (kuwa matepali) ndio maadili ya Mtanzania?
 Je, wizi, vibaka, panya road, ufisagi, nk ndio maadili ya Mtanzania?
 Je, kutofuata sheria za barabarani kama kutanua, nk ndio maadili ya Mtanzania?
 Je, makelele ya vyombo na sehemu za burudani na makelele ya makanisa, nk ndio maadili ya Mtanzania?
 Je, watoto/vijana wetu hasa wa kike kurubuniwa kwa chips na soda, nk ndio maadili ya Mtanzania?
 Je, nk ndio maadili ya Mtanzania?

Nina kiu sana ya kuelimishwa hivi maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Mimi ni Mkatoliki na miaka ya 90 nilisoma gazeti moja la hapa nchini likimhoja Padri mmoja Mkatoliki na kwa maelezo ya gazeti hilo, alikuwa ni Mwitaliano aliishi sana na kuhudumu hapa Tanzania na wakati huo alikuwa anahamishwa na kurudi kwao moja kwa moja. Moja ya swali aliloulizwa, una nini la kusema juu ya Watanzania?

Alijibu kama ifuatavyo, Watanzania ni watu wazuri sana na hawakatai neno lakini katika neno lao la hawa Watanzania, ukweli au utekeleza wa neno analokuambia ni asilimia ndogo sana na alizitaja asilimia lakini bahati mbaya sikumbuki (hii ni yangu - ukweli au utekeleza wa neno analokuambia Mtanzania ni asilimia 5 na 95 ni uongo). Mtanzania akikwambia tukutane saa 4 asubuhi, kwa asilimia 99 hatafika 4 asubuhi. Je, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Jibu la Padre huyu Mwitaliano, ndivyo ninavyopitia katika maisha yangu katika mahusiano yangu na Watanzania wenzangu na ndani ya familia yangu. Ni zaidi ya 95% ya rafiki zangu na ndugu zangu walichukua pesa kwangu kwa kuazima hawakurudisha katika muda mwafaka. Up to 40% hawakurudisha kabisa na nimelazimika kuzifuta kama bad debts. Je, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa? Hapa nitatuma jedwali moja la mikopo kwa wanachama la taasisi ambayo mimi na wenzangu tuliianzisha kwaka 1998 ili kulinda UTU wa mwanadamu aliyedhalilika sana wakati huo mimi narudi toka masomoni nje kwa kukosa elfu moja mchango wa matibabu hivyo anakosa kutibiwa, kwa kukosa elfu moja hivyo mtoto wake anafukuzwa shule, kwa kukosa elfu 10 aanzishe ujasiriamali, n.k na wakati huo huo alidhalilika sana na UKIMWI Pamoja na ndugu zake. Muone jinsi wanavyopa na hawalipi. Hii ni hadidhi ndefu na ya kusisimua. Je, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Mwanzoni kwa mwaka huu rafiki yangu mmoja na ni kiongozi mkubwa tu hapa duniani na ni tajiri kunizidi mimi kabisa kwa mbali alikuja kwangu na kuniomba nimkopee pesa au nimtafutie kwa rafiki zangu. Sikuamini alipokuja kwangu lakini niliamini juu ya concern yake kwani aliniambia amepata biashara kubwa somewhere na atazirudisha ndani ya miezi 3 kwani atakuwa amesha supply mzigo na kulipwa. Mimi nikamjibu, sina rafiki yo yote lakini nina mafao yangu ya kustaafu utumishi wa umma naweza kukupa. Nikampa yote. Mpaka sasa kimya. Je, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Hulali usingizi wa pono kwa kila mara kushtuka vibaka, panya road, nk usikiapo mstuko wa aina yo yote na kuna wakati, kumbe ni paka tu unakuja gundua. Wakati naishi Mwenge kabla ya kuhamia Mbezi Beach - Kunduchi nilikuwa kila wiki lazima niibiwe nyumbani hata ndala (kanda mbili). Wakishindwa kuingia ndani, basi cho chote kilichopo nje, wataondoka nacho. Siku moja nimekaa na rafiki yangu hadi karibu ya 11 asubuhi na ndio nikaelekea kulala. Kabla sijapata usingizi nikasikia kelele kelele za vitu, nikajua hawa ni watoto wameamka. Mara walipoamka, naitwa chumbani, mlango wa jikoni umevunjwa na tumeibia tena. Je, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Mchana na usiku ni makele kila mahali ya kila aina, burudani na baadhi mikesha ya makanisa ya kilokole. Kwenye daladala, vituo vya mabadi, nk ni makelele ya wahubiri. Je, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Sitaki kuzungumzia ya mashuleni juu wizi wa mitihani, udanganyifu, kuibia, kwenye usafiri wetu wa umma, benki, hospitali, makazini ambako mimi nimehudumu kama mtumishi wa umma nenda rudi, njoo kesho, njoo kesho, nk, uchafu wa mazingira yetu, tunavyo tupa takataka ovyo, maisha ya utapeli tapeli, uvivu, nk. Mambo ya ovyo ambayo nimewahi kuyashuhudia kwa macho yangu mwaka 2020 wakati wa uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais, n.k. Pia, siku hizi umezuuka UCHAWA kwa maana ya tabia ya kusifiya na yasiyo stahili kusifiwa. Je, maadili au mila au desturi au utamaduni za Mtanzania ni zipi hasa?

Nina mengi, lakini itoshe niishie hapa. Nitafurahi sana ye yote ambaye anajitolea muda wake adhimu kunielelimsha juu ya maadili au mila au desturi au utamaduni ya Mtanzania ni yapi?

Asanteni sana.

Betram B. Kiswaga
 
A pastor in DRC burnt all his flock, following what Mackenzie did in Kenya, now this one in Congo.

How much trust do you have in ur pastor?

We are surely living in a crazy world!


Punchline- Faith must be guided by reasoning and if not, we are all going to perish in the name of looking for heaven from the fake religious leaders of nowadays
 

Attachments

  • IMG-20230918-WA0017.jpg
    IMG-20230918-WA0017.jpg
    71.1 KB · Views: 0
Ghana kafilisika kisa kukopa kwa riba kubwa ili ajenge miundombinu ambayo hailipi hayo madeni.

TZ inafuata njia hiyo hiyo huku ikijigamba bila ya takwimu madeni yanabebeka haiko mbali nayo kujitangaza mufilisi.

Ukope ujenge shule au barabara au sijui nini swali la kujiuliza hiyo miundombinu inalipa vipi hayo madeni na riba sasa hivi haishikiki?

Bado kwenye mahesabu hatujaweka ufisadi, wizi na ubadhirifu
 

Attachments

  • PSX_20230919_081617.jpg
    PSX_20230919_081617.jpg
    216.3 KB · Views: 0
Back
Top Bottom