New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Muda wote aliowekwa lupango au kifungoni kwa mwezi alipwe fidia ya KCC
 
Hii itasaidia kuifanya ofisi ya DPP kufikiri mara mbili kabla ya kumkamata raia asiye na hatia kwa minajili ya kumkomoa tu
 
IGP kwa mwezi huhongwa $10K na maafisa waandamizi serikalini wapatao 60 wako kwenye payroll ya ACACIA!

Ufisadi huu huigharimu ACACIA gold $1.2 Mill kwa mwaka.

Na hakuna aliyechukuliwa hatua hadi leo hii.

Kwa hii dhuluma dhidi ya Mwenyezi Mungu baadhi yao wamepewa ulaji hata baada ya kustaafu.

Sasa tunaelewa kwanini maafisa waandamizi wa polisi hutukoromea watahakikisha CCM itatawala milele kumbe hawailindi CCM bali wanalinda vitambi vyao!
 

Attachments

  • PSX_20230922_083346.jpg
    PSX_20230922_083346.jpg
    132.5 KB · Views: 2
Tunasema kuwakatalia maandamano siyo sahihi.

Huwezi ukawa unafanya maamuzi yanayowaathiri utu na ustawi wao halafu wao hawawezi kujibu mapigo.

Nchi gani hiyo ni watawala tu ndiyo wana sauti na watawaliwa hawana sauti hata ya kuandamana kupinga sera wanazoona ni mbovu kwa maendeleo yao.


Nchi ambayo maandamano yamepigwa marufuku huwa hazina maendeleo kwa sababu watawaliwa hawana mchango kwenye mustakabali mzima wa taifa lao.

Na nchi ambayo ni watawala tu ndiyo wanajiona wajuaji huwa inafanya makosa mengi na hakuna wa kuwasahihisha.

Tujifunze maandamano ni sehemu ya utawala bora na wa kisheria.
 

Attachments

  • PSX_20230924_135410.jpg
    PSX_20230924_135410.jpg
    50.2 KB · Views: 3
Tatizo la huyu anapinga Muungano sasa hajui alichonacho na anapaswa kukitunza ni hii kitu inaitwa Muungano?

Akitoka kwenye Muungano hata hiyo Zanzibar anayodai ni nchi haitakuwa nchi?

Atataka Pemba yake maana ataona atapata mkate mkubwa akiwa nje ya Zanzibar.

Na akiipata Pemba yake atagundua kumbe Pemba nayo siyo nchi ila ni Muungano wa visiwa kibao 😃 😀 😄 😁 🤣 😂 😃 😀 😄 😁 🤣
 

Attachments

  • Screenshot_2023-09-25_093014.jpg
    Screenshot_2023-09-25_093014.jpg
    158.1 KB · Views: 2
Tunasema tuhuma za kumwaga maji Mtera ili njemba auze jenereta siyo za kweli ni kuchafuana tu
 
Tangia tupate uhuru hakuna kiongozi aliyewahi kufanya hujuma ya aina yoyote ile inayohusiana na kina cha maji cha bwawa lolote lile
 
Ukiwafuatilia kwa karibu wanaodai kuna hujuma wengi wao uwezo wa kufikiri kwapani
 
Kwanza ya yote ni nani leo atanunua jenereta wakati ana gesi ya kupikia na ana solar ya taa?


Soko la majenereta halipo hapa nchini!
 
Hata Tanesco leo hawawezi kuingia mikataba ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kutumia jenereta
 
Hata walionunua zamani jenereta hizo walizibadilisha mfumo wake wakawa wanazalisha kwa vinu vya gesi kupata umeme
 
Kwa hiyo msukumo wa kulazimisha soko la majenereta kwa kumwaga maji bwawa la Mtera haina makalio
 
La pili, na ambalo ni kubwa zaidi ni dhana potofu Mtera ndiyo tunaitegemea kwa kuzalisha umeme na ukikosekana nchi iko gizani. Dhana hii haijapata darasa la kutosha.

Bila hata ya kuweka takwimu mabwawa yote mchango wao wa uzalishaji umeme ni mdogo mno na sababu zipo kibao.

Hata Mtera ikizimwa leo ni mgao utaongezeka lakini nchi haitakuwa gizani sasa kwanini wanaikuza Mtera kama ndiyo kila kitu kama siyo kutujuza wao ni hamnazo?
 
Hao waliobwaga manyanga Tanesco siyo kwa sababu ya hujuma ya aina yoyote ile kama baadhi wanavyowazushia
 
Sababu kuu utalaamu hawana na michoro ya mlo wako mstari wa mbele na pia aliyewateua huyo waziri aliwapachika hapo kwa sababu hiyo tu
 
Back
Top Bottom