New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Tovuti ya tume iwe wazi na kuonyesha fomu ya kila kituo ili kila mpigakura ajihakikishie ile fomu aliyoiona kwenye kituo ndiyo iliyotumika kupata majumlisho ya kura za jimbo
 
Marekebisho ya sheria za uchaguzi ni lazima yaishurutishe Tume ya uchaguzi kutumia tekinolojia ya kisasa katika kusafirisha na kuyahesabu matokeo ya kila kituo kwenda kuhifadhiwa kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi
 
Tunasema jinsi sheria ya uchaguzi ilivyo inaitaka Tume ya uchaguzi itangaze matokeo ya kila jimbo lakini msingi wa hayo matamko wapigakura hawawezi kuyahakiki na hivyo kwa kupitia sheria mbovu za uchaguzi utendaji wa tume ya uchaguzi hauwezi kuhakikika.

Wapigakura wanayo haki ya kikatiba kuhakiki jinsi tume ya uchaguzi inavyotekeleza majukumu yake ya kisheria lakini sheria za uchaguzi ni kikwazo kikubwa kwa sababu wapigakura hunyimwa taarifa za majumuisho ya kura kwa kila kituo
 
Sheria za uchaguzi inabidi ziwape mamlaka makatibu wakuu wa vyama vya siasa kuwakilisha orodha ya wagombea wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa
 
Ni jambo la ajabu kabisa tume ya uchaguzi imejianzishia kanuni za uchaguzi ambazo tunadiriki kusema zinalenga kuengua wagombea wa upinzani kwa vigezo vya dosari za ujazaji wa fomu za wagombea
 
Kanuni za uchaguzi za tume ya uchaguzi zinazoanzisha sifa mpya kinyume na sifa zilizoainishwa kwenye katiba ni haramu.
 
Jinsi ilivyo kanuni za tume ya uchaguzi zimetengua sifa za wagombea zilizoanishwa kwenye katiba
 
Wengi hatuoni uhaja wa kwenda mahakamani kupinga kanuni haramu za uchaguzi kwa sababu hatuna imani na mahakama hususani kwenye masuala ya kikatiba
 
Sifa za wagombea ubunge zilizoanishwa kwenye katiba ni kujua kusoma na kuandika
 
Lakini jambo linalotia uchungu ni pale Tume ya uchaguzi kwa kupitia kanuni ilizojitungia yenyewe inazifuta au kuzidhoofisha hizi sifa kwa kuanzisha sifa nyingine ambazo hazihusiani na ufahamu wa kusoma na kuandika kama katiba inavyosema
 
Dosari za ujazaji wa fomu sasa ni kisingizio ya kutengua sifa za kikatiba za mgombea ajue kusoma na kuandika
 
Kwa lugha nyingine, mgombea anayejua kusoma na kuandika kama fomu yake ya kugombea ina dosari basi huenguliwa kinyume na matakwa ya kikatiba
 
Kama fomu haina sahihi ya mgombea au hakimu au muhuri wa kimahakama au hata tarehe kanuni tajwa zinasema hana sifa kinyume na matakwa ya kikatiba
 
Kama fomu haina picha ya mgombea au imenyofolewa na CCM basi hana sifa hata kama kakidhi sifa za kikatiba za kujua kusoma na kuandika
 
Kama mgombea kaporwa fomu na vyombo vya dola au magaidi wa mgombea wa CCM basi huyu wa upinzani kapoteza haki ya kugombea na wa CCM hupitishwa bila ya kupingwa
 
Swali la kujiuliza ni kwanini tume ya uchaguzi inatunga kanuni za uchaguzi zinazokiuka katiba kwa minajili ya kuwapora wagombea wa upinzani na wapigakura kiujumla kuwachagua viongozi wanaowapenda?
 
Kwanini tume ya uchaguzi hujiundia kanuni ili kujenga mazingira ya vyombo vya dola kuwapora wapinzani haki yao ya kimsingi ya kugombea na vile vile kuwanyimwa wapigakura haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wao wanaowaamini?
 
Kwa lugha nyingine, kwanini tume ya uchaguzi inakuwa nayo ina masilahi mazito ya kuhakikisha CCM inaiba kura ili wawatangaze wagombea wake wameshinda?
 
Tunaposema hatuna imani kabisa na tume ya uchaguzi ni kwa sababu tunao ushahidi wa kutosha wa jinsi inavyoipendelea CCM
 
Pengine madhara makubwa kuliko yote yanayosababishwa na sheria batili za uchaguzi ni baada ya wakurugenzi tajwa kuiba uchaguzi kwa niaba ya CCM huu uwakilishi haramu hushindwa kukemea maovu yanayoendelea kwenye serikali za mitaa na kuishia kuwafokea fokea na kuwahamisha hamisha tu kwa sababu wanadeni la fadhila kwa kupachikwa madarakani kinyume na katiba
 
Back
Top Bottom