Wanajamii,
Yaliyompata Sitta ndiyo yaliyostahili yampate! Alikuwa anajijengea himaya na utukufu wa bandia. Akiwa kiongozi wa mhimili mmoja wa dola, alikuwa anapeleka nchi pabaya anajiona yeye na mhimili wake ni bora zaidi kuliko mihimili mingine, yaani Serikali (Utawala/Baraza la Mawaziri), na Mahakama! Wakati fulani, baada ya Rais kumaliza kulihutubia Bunge, Sitta, kwa kujiamini kwake kupita kiasi, akamkoasoa hata Rais na kumsema kuwa ni mpole sana
na sisi (tunaojua zaidi) tuko tayari kukusaidia Ni matamshi ambayo hayakustahili yafuatie hotuba nzuri ya Rais!
Huo unaoitwa Ufisadi ambao Sitta, ndani ya Bunge na watu kama Mfanyabiashara Mengi nje ya Bunge, wanajifanya ndiyo wapiganaji wake watakatifu, siyo chochote ila ni kuwasakama tu waliofanikiwa kuongoza Serikali, mwaka 2005, ikiwa ni madhila yanayotokana na genge fulani kushindwa katika kinyanganyiro cha Urais, mwaka huo. Sitta naye alijiunga na kulisaidia gnge hilo, kiusaliti, kwa vile naye alikuwa mhanga - aliutaka Uwaziri Mkuu na akaukosa! Lilipojitokeza suala la Richmond, likasukwa katika namna ya kumsulubu Edward Lowassa, kwa kumninginiza nalo shingoni mpaka akalazimika, kiungwana, kujiuzulu. Waliukataa hata ushahidi wake wa maandishi na hawakutaka hata kumhoji! Sitta na Mwakyembe ndiyo authors (watunzi) wakuu wa Ripoti ya Richmond, ambayo siyo tu ilikuwa ni uzushi, bali ni ushuzi mtupu! Hakuna uthibitisho wowote, mpaka leo hii, wa Richmond na Lowassa! Kama Ufisadi maana yake ni ubinafsi na ubadhirifu wa fedha za umma , basi muangalieni huyo Sitta wenu:-
· Amejipangishia nyumba, ambayo anahusika nayo, inayolipiwa na Serikali pango la USD 8,000 (sawa na Tsh. Milioni 12) kila mwezi, zikiwa ni kodi za wananchi;
· Samani ya nyumba yake ya hapo juu iligharimiwa na Serikali kwa TSh. Milioni 300;
· Amejijegea hekalu la Ofisi ya Mbunge Urambo, kwa gharama ya zaidi ya mara kadhaa juu ya kile kiasi kiichotengwa maalum na Serikali kwa Ofisi za aina hiyo kwa Wabunge. Alisema ni ya hadhi ya Spika, ambaye alidhani wakati wote utakuwa ni Mbunge wa Urambo, mpaka afe;
· Ana interest katika biashara ya kuuza nje mbao/magogo/maliasili;
· Ndiye aliyeshinikiza Wabunge kupata marupurupu manono, zaidi ya Tsh. Milioni 40 kwa kukaa Bungeni kwa miaka mitano tu, yakiwa ni mara 10 zaidi ya anayopata Profesa wa Chuo Kikuu aliyenoa bongo kwa uhakika na anayefundisha vijana wetu kwa miaka 30;
· Ameshabikia kukifarakanisha Chama chake vs Serikali na Bunge, mpaka utekelezaji wa Ilani ya CCM ukasuasua na chama hicho kupata ushindi kiduchu mwaka 2010! Alishabikia porojo za EPA, Suala la Madini, Kiwira (kwa kusaidiwa na akina Mengi na vyombo vyake vya habari na magazeti yaliyokubali kutumiwa ya akina Saed Kubenea), bila ya tija yoyote! Fitina tu!
Huyu ndiye mpiganaji wa Ufisadi. Tatizo letu siyo Ufisadi. Kwani Mafisadi walikuwepo enzi za Nyerere tulipokuwa tunakula sembe ya njano ya msaada wa Marekani; maduka ya kaya yasiyokuwa na kitu; foleni za kila kitu; petroli ya mgao; idadi kiduchu ya vijana wanaopata elimu ya juu (ndiyo maana tukawa tunasaidiwa kusoma bure Urusi, Uchina, Cuba na nchi za kijamaa za Ulaya Mashariki); uchumi uliokuwa hasi wa 2%; mfumuko wa bei wa 35%; sigara inayouzwa kwa mkupuo; bia ya ya kibali n.k.?
Bwassa