New Force/Golden Deer kwanini ajali mnapata nyie tu?

New Force/Golden Deer kwanini ajali mnapata nyie tu?

Upo sahihi kabisa,mchina bado yupo kwenye utafiti na basi zake ili ziweze kuwa compatible na hali yetu huku Africa
Kwamba ni matatizo ya kiufundi ndio hupelekea ajali za New force kuwa nyingi? Yanaweza kuwa yepi Mkuu?
 
Pia wana bus nyingi sana barabarani kila siku..

Kampuni kama sauli ama katarama zinaingia mara 20 kwenye kampuni ya new force
Kwahiyo hii ndio sababu ya ajali!

Unaifahamu Feo/Selous?
NF wanaingia Mara ngapi kwa Feo na hawana ajali za kipuuzi kama hizi?

Halafu ajali ni ya NF unaanza kutaja kampuni zingine kama excuse.
 
 
 
Pia wana bus nyingi sana barabarani kila siku..

Kampuni kama sauli ama katarama zinaingia mara 20 kwenye kampuni ya new force
Sauli hana gari siku hizi

Na kama zipo ni mbili

Nazo hazisafiri kila siku.

Wamegeuka matapeli,wanakatisha watu tiketi wakijua kabisa gari hakuna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyota yao ya bahati imechafuka, misukosuko na mikosi ya ajali inawaandama.
 
Kuna jamaa Mweusi hivi mrefu Huwa anakuwa konda ila baadae anampokea dereva aisee Yule ni balaaa.. Jamaa anakimbiza hatariii!
 
Baadhi ya basi za kichina manufacturers anaweka option ya basi kuja na retarder. Na retarder za kwenye basi za kichina zinazokuja ni Eddy Current Retarder hii efficiency yake huwa inapungua maji yakigusa na inatumia umeme.

Kwenye Golden Dragon za UDART mchina kafunga gearbox ya Voith na hydraulic retarder.

European manufacturers wanatumia hydraulic retarder ukicheki kuanzia Volvo,Scania,Man Diesel,Daf,Iveco etc.

Retarder ya Bus za kichina na Scania au European brand uwezi linganisha, dereva wa Scania ana faida kubwa kwenye Braking ukiacha kutumia pedal brake, retarder iliyopo kwenye gearbox inampa faida kwenye brake.
 
Ushaambiwa shida ni madereva mkuu

Mziki wa New Force hata mkurugenzi Sauli mwenyewe anajua hauwezi hata waungane na Super Feo
Inawezekana. Nilisikia mtu akisema kuwa madereva wazee wengi ktk new force wametolewa. Wamepewa vijana. Hasa route za kupitia mbeya aliyekabidhiwa gari anataka madereva vijana wanaoweza kukimbia. Inawezekana hayo ni matokeo yake. Either wazee wamereact au uzoefu kwa vijana kuendana na speed. Kwa kuwa inasemekana ukichelewa sana gari anapewa mwingine.
 
Mchina sasa hivi ana brands nyingi za mabasi hapa Tanzania kaiacha Scania kwa mbali sana

So obvious ikitokea ajali hata kama mabasi yako 10 hukosi Chinese brands 8 au zote 10 utakuta ni Chinese brands

Kwa hapo hauna hoja ya msingi
Hv ww unaongelea ubora wa magari sokoni au idadi ya magari sokoni

Kwa idadi ya magari kweli mchina anakimbiza solo la bongo
Kwa ubora wa magari mzungu anakimbiza soko la bongo na duniani kote

So kwa hoja yako kuwa mchina kamzidi scania idadi ya magari uko sahihi mnoo ...ila kwa ubora utakua unatuongopea
 
Back
Top Bottom