Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Waganda wapo huru kuja huko Tanga, lakini kama ilivyo kawaida ya soko huria, hutegemea na jinsi umejiandaa. Leo hii tumeshusha gharama ya kontena tokea Mombasa hadi Nairobi kwa asilimia 50%. Yaani hapo awali walilipa 100,000Ksh sasa ada imeshushwa na kuwa 50,000Ksh. Hivyo hiyo ni hatua muhimu sana ya kuteka soko lote la Uganda, Rwanda na batoto ba Kongo DRC.
Hela za kufikisha reli hadi mpakani zimepatikana wakati nyie bado mnaomba kila rais anayewatembelea, juzi mlikua mnambembeleza Zuma akawawakilishe kule Brics, badala wenyewe mvae masuti na kwenda kujipigia debe, au Kingereza ndio majanga, si kwenu kuna evening English classes.
Tukikamilisha hadi mpakani, gharama itashushwa na kuwa nusu kwa wadau wote wa ukanda huu, tunataka kunyakua hadi soko la Kaskazini mwa Tanzania na kanda ziwa maana pale Kisumu kuna safu imechana na kutua kwenye ziwa kwa ajili ya Mwanza. Huu mchezo hautaki hasira wala ukurupukaji.
Haha inachekesha kuona umeandika kishabiki lakini sio ki-mantiki. Leo ni siku ya pili gari moshi la kenya linaendeshwa kwa hasara maana gharama zote mpaka hivi sasa na kwa kipindi chote cha mwaka mzima ni ruzuku. Hiyo bei ya Shs 50,000 sio gharama halisi, hata nauli za abiria sio halisi, ni ruzuku ndio inashikilia mradio huo. Wachina wamelalamika mnavyo shusha bei mpaka mradi unapoteza maana yake kalisi, lakini serikali ya Jubilee imeziba masikio na kutwanga mguu.
SGR allocated Sh15.5bn ‘subsidy’ for operations
Kenyatta ameenda na bakuli China lakini akasahau kwaambia wachina kama jirani zake Waganda na wao wanataka reli. matokeo yake mchina kawakaukia Waganda eti mpaka kenya ione faida ndio itawakopesha, kwa maana nyingine Mchina ameshaaza kuona reli ya Kenya inaweza isizae matunda kutokana nchi ambazo Kenya ina zitegemea wameshaanza kufikiria plan B.