New TARURA Parking Fee System inaenda kuwa aina mpya wizi na uonevu

Huu mwaka wa 2 situmi gari mjini
Gari mjini ni mastress tu....
Poleniiii wenye magari

Ova
 

Kuna tatizo. Hakuna namna ya mdaiwa kujithibitishia (verify) mahali na muda wa parking aliotumia kulinganisha na deni.

Details zaidi zinatakiwa. Au watoe risiti (printout) kwenye maegesho.
 
Hii system ni ya uongo itakuwa ukituma kuangalia ndiyo unawekewa deni mimi nimejaribu kuangalia kwa no ya gari iliyopaki tu bila ya kutoka nayo inadaiwa eti
 
Ni hivi, hayo malalamiko sijayakataa, ila kwa uzoefu wangu na kazi hii, hayo madai ya ukubwa wa deni nina mashaka nalo kwa sababu madereva wengi, kwa uzoefu wangu, wakipark gari, hata kama imekaa nusu saa, wanadai ndiyo wamefika, mwingine atasema hajakaa hata dk tano, au anakuambia bado hajashuka yaani kiufupi wanatoa madai ya excuse kwamba wamekaa muda mchache.

Sasa, hoja yangu ni kwamba, ikiwa madereva wengi hawajui ni muda gani wamepark, na madereva hao hao wanadai deni ni kubwa, basi, madai ya ukubwa wa madeni ni batili kwa sababu deni kuwa kubwa au dogo inategemea gari imepaki muda gani. Na hapa uzoefu unanionyesha kuwa madereva hukadiria dakika chache kuliko uhalisia.

Halafu kingine, madereva wengi hawajui maana ya kuegesha. Hapa nina mifano; moja; dereva anakuja parking na kuegesha gari ila hashuki na atakaa hapo hata lisaa, nikienda kudai parking fee, dereva anajibu hawezi kulipa kwa kuwa hajashuka. Pili, gari inatoka getini, dereva anadaiwa parking fee anajibu hawezi kulipa kwa sababu hajaegesha gari.

Sasa, kama dereva kapark, na kabaki kwenye gari akidhania kuwa hatadaiwa, au amepark masaa kadhaa ila akadhani alikaa sekunde, huku mhudumu wa TARURA kamwingiza kwenye Mfumo, huyu dereva ni lazima alalamikie ukubwa wa deni maana japo alipark, hakujua kwamba amepark.
 
Details mfano T000DxV, location Buguruni Malapa, time 1230, parking attendant Rose.
Haiwezekani, basi waseme gari zote nchini kwa mwezi zilipie to parking fee standard ya 25,000...thru TRA payment system. Kwa mwaka discount, lipia miezi 10..park popote.

Huu ubabaishaji utaisha. Watakusanya mpaka waombe pooh! Shida yao makusanyo wala siyo kujenga barabara.

Everyday is Saturday................................😎
 
Hata hiyo ya risiti bado mlikuwa/ ni wasumbufu.

Mfano sasa hivi 12:20pm nimetoka kumdai dereva hela, anaanza kumwambia abiria alipe. Abiria anamwambia ni jukumu la dereva. Dereva anadai hana hela. NB: Mimi nipo Mamlaka nyingine siyo TARURA.
Holy Crap
 
Kwa system ilivo ni rahisi sana Attendant wa TARURA kuandikia Parking fee hata gari ambayo haija-park, sababu anachohitaji ni Plate number tu.
 
Nani ana thibitisha au kuhakikisha hiyo bill unayopewa ni halali? Bora zile receipt ilikua mtu unaona umewekewa kuanzia muda flani hadi unapoondoka unaweza kuthibitisha. Lakini hii ya sasa kubambikiwa rahisi sana.
Wanataka kutuumiza
 
Mimi wiki iliyopita nilipack kisutu mida ya Saa mbili, kwa nusu Saa, baada ya hapo nikaenda Kkoo, mtu wa parking Kkoo ananiuliza umepaki wapi asubuhi hii? Mbona umechajiwa 4,500 kwa siku hii ya Leo ? Na hapo ni Saa Tatu asubuhi


Hizo ni MBINU za waziri wa fedha za kuongeza mapato ya Serikali.a
 
Hizo ni MBINU za waziri wa fedha za kuongeza mapato ya Serikali.a
Mbinu za kishamba, mwendazake, aliwaambia watz tushavuka hatua ya ujinga, tunajua kupambanua mambo na kutafakari.

CCM na ilaumiwe tu na aina viongozi waliowapandikiza.
Ni upuuzi kuiga mfumo wa ulaya huku hauna miundo mbinu ya ulaya, UK mfano, wewe park tu kindezi, fee inakufuata nyumbani kwako. Camera na IT systems zitawasiliana naye. Digitally kweli!

Everyday is Saturday...............................😎
 
Una uhakika gani kama alipata Elimu Mkuu unaposema akadai Ada..
 
Mkuu unakwaza sana watu kwa comment zako ujue!

Mada inayoongelewa hapa siyo unacho comment wewe.

Watu wanalalamika kuandikiwa parking fee za ghushi, yaani watu wengine hawajaondoa magari ndani lakini magari hayo inasomeka yanadaiwa tozo ya maegesho!

Sasa wewe umekazania ukwepaji wa malipo, nani kasema hilo?

Embu nenda na mada husika.
 
True.wanabeti Sana kama matraffic.Nilikuwa na daladala lipo garage mwezi mzima kucheck kwenye system Ina cheti tena cha ruti isiyo yake
 
Parking attendant kama hesabu haitoshi ana bet tu namba yeyeto.Muhimu ukipaki chukua ushahidi wa video.
 
Kwenye madai ya ukubwa wa madeni, hata kwenye mfumo wa cash yapo.

Siyo kwamba haya madai yameanza wakati huu wa mfumo mpya. Mimi ni mzoefu wa hii kazi.

Sasa wabishi wamekamatika. Kama una analytical skills unaweza ukaelewa ninachomaanisha.
 

Mkuu uliona mbali sana
 
TARURA wamerudisha mfumo ule ule kama zamani unalipa kwa mtoa risiti,ile ya kulipa online imesimamishwa maana hasara zimekuwa nyingi na malalamiko pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…