New York, Marekani: Rais Samia ashiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali Wanawake

New York, Marekani: Rais Samia ashiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali Wanawake

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itaendelea kuhakikisha kunakuwepo Usawa wa Kijinsia licha ya vikwazo vinavyojitokeza‬

‪‪Amesema hayo akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali Wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa‬

Aidha, amesema hivi karibuni ameunda Timu ya Wataalamu inayoangalia namna bora kwa Tanzania kupata Usawa wa Kijinsia na miongoni mwa maeneo inayopitia ni marekebisho ya Sheria Kandamizi‬

————
Rais wa WorldBank, David Malpass amesema Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali kukuza Uchumi kupitia mabadiliko ya kidogitali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi

Ameeleza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu ambaye ameishukuru WB kwa mchango wake kwa Tanzania kwenye huduma za jamii na mapambano dhidi ya COVID19

Pia, Rais amefanya mazungumzo kuhusu kuwezesha Biashara kwa kuimarisha upatikanaji wa Chanjo, usimamizi wa uvuvi na kilimo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala

9750F1A6-7BC9-4F6C-8720-4D84DD13DCAD.jpeg
80122794-BC0A-4056-9425-9CA6BAFAC1AD.jpeg
 
Kiswahili kigumu au labda mimi sijaelewa kwenye aya ya pili inayosema "Pembeni wa mkutano huo....."
 
Vigezo alivyotumia JPM kujipima dhidi ya watangulizi wake na kuwashinda, vitumike pia kumpima Mhe Rais Samia.
 
Kuna watu wanalalamika why Balozi hajamwakilisha kaenda mwenyewe, wengine wanasema why hajaenda Makamu, roho za kimaskini shida sana, Hivi Balozi or Makamu wangeweza kupewa nafasi ya kuongea na hao watu wazito hivyo duniani?

Ni kama kuna kikao cha akina Baba wote mtaani kwako then wewe unamtuma mwanao or HB huku ukiwa huna sababu yeyote ya maana ya kutohudhuria, nobody atawasikiliza or mchango wao hauwezi kuwa na nguvu kama midingi mingine!!

WaTZ tumezidi ujuaji aisee!!
 
Kila kitu kisiwe sasa wanawake wanawake jamani, watu wanataka maendeleo, regardless of gender. Very simple, watanzania tunataka maendeleo, haijalishi jinsia gani anaongoza.
Hayo mambo ya wanawake waliyajadili kwenye hiko kikao chao cha wanawake duniani!! Nje ya hapo watu wengine wote aliokutana nao kaiongelea TZ kwa ujumla
 
Mwenzake kutoka Zambia Mh. Hakainde Hichilema kipenzi cha wana-zambia na Rais aliyechagulia kwa kufuata misingi ya demokrasia na kusimamia haki amewasili siku mbili nyuma yake, kesha hutubia mbele ya viongozi wakuu wa nchi mbalimbali.

Ila mama yetu hadi leo, bado hajaaminiwa kuzungumza? Kweli sisi kama taifa hatuthaminiwi hatuna ushawishi tena kwenye mataifa yaliyoendelea.
 
Kila kitu kisiwe sasa wanawake wanawake jamani, watu wanataka maendeleo, regardless of gender. Very simple, watanzania tunataka maendeleo, haijalishi jinsia gani anaongoza.
Bongo Tumevurugwa.
Akili na Maarifa Shidah.
Tatizo letu Watanzania,
Sio Jinsia au Nini,
Tatizo ni kwa Namna Gani Tutapata Yafuatayo:-
1) Utawala Unaofuata Sheria na Sio Matakwa ya Rais.
2) Sheria Mama Inayokidhi Mfumo Tulio nao Sasa.
3) Katika Chaguzi Huru na Za Haki.
4) Ili Tutengeneze Society ya Watu Wanaorithiana Kistaarabu, Lengo Tusikwaruzane.
5) Society yenye Kuzingatia Haki, Upendo na Mshikamano kwa Maendeleo ya Watu.
6) Democrasia Sio Gender Bali ni Serikali ya Watu,
Kwa Ajili ya Watu na kwa Manufaa ya Watu.
Kwa Hiyo basi , Cha Msingi Hapa ni Kiongozi Bora na Sio Bora Kiongozi Eti Sababu ni Mawazo ya Gender.
 
Umesema vema mkuu, Tuandike Katiba Bora, CCM wanatuchelewesha kutegemea busara na hisani ya mwenyekiti wao.
 
Back
Top Bottom