New York: Mwizi wa gari atishia kuita polisi baada ya kukuta mtoto ameachwa kwenye gari aliyoiiba

New York: Mwizi wa gari atishia kuita polisi baada ya kukuta mtoto ameachwa kwenye gari aliyoiiba

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Vituko, huko New York, mwizi baada ya kuiba gari na kutokomea kusikojulikana, katika harakati za kukagua gari akakuta kuna mtoto ndani yake, ikabidi arudi hadi alipoiiba na kumkuta mama wa mtoto.

Baada ya kumkuta mama na mtoto akatishia kuita polisi kwa uzembe wa mama wa mtoto kuacha mtoto peke yake kwenye gari.

Mwizi hakuishia hapo, akamfundisha mama wa mtoto jinsi ya kutunza watoto wadogo, akamuonya kwa uzembe uliopitiliza wa kuacha mtoto peke yake kwenye gari.

Mwizi baada ya kutoa onyo kali na somo kubwa kwa mama wa mtoto, akamuamuru mama achukue mtoto wake kwenye gari na kisha jamaa akatokomea na gari huko kusikojulikana.

Hii ni somo kuwa sio wezi wote wana roho mbaya😂😂.

Car thief turns around, threatens to call police on woman for leaving young child in the vehicle, officials say Car thief turns around, threatens to call police on woman for leaving young child in the vehicle, officials say
 
Aliiba vyote kesi ndogo hiyo kwa hakimu kuamua.

Huyo mwizi aletwe Tanzania tumhukumu kwa kuiba vyote mtoto na gari.
 
Kwahiyo baada ya kumrudisha mtoto akaendelea kuliiba tena lile gari...?
 
Hata huku bongo kuna wengine waungwana, akikupora simu anakuachia laini yako.
 
Busara ya hali ya juu mwizi katumia ,gari litataftwa ilasio mtoto hatakama atatafutwa hawezi kua kama huyo akipotea au kufa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hata huku siku hizi watu wanasindikiza wezi baada ya kuibiwa na kuwatakia kila la heri.
 
Kuna movie ya kisauzi jamaa aliiba gari akaja kushtuka kumbe kuna mtoto ameachwa kwny siti ya nyuma,mwizi ikabidi amlee tu huyo dogo.
 
Back
Top Bottom