News Alert: Masha awasalimia Keko..

News Alert: Masha awasalimia Keko..

Quote:
Originally Posted by Field Marshall ES
Wakuu sometimes tunakwenda out of the lines na hizi uncalled and unconstructive criticism! Au kwa sababu tu ni Minister Masha? a successful young man and larger than life at his age of 30s?

Quote:
Originally Posted by FDR.Jr
MAADILI GANI MNAYOYAZUNGUMZIA HAPA? MASHA HATA JUZI ALIKWENDA PALE KISUTU NA ALISALIMIANA NAO PUBLICLY.
UWAZIRI WAKE HAMFUNGI KUONGEA AU KUMTEMBELEA MTUHUMIWA PALE ANAPOSHIKILIWA NA VYOMBO VYA SHERIA.
NARUDIA TENA MASHA YUKO SAHIHI KAMA MTANZANIA, KIONGOZI NA MWANASHERIA

Quote:
Originally Posted by moelex23
Habari za ndani kabisa ni kuwa Masha hakwenda Keko hizi ni rumors ambazo hazina msingi wowote.
Tuwe waangalifu

Lo !! masikini !!

Quote:
Originally Posted by Mzee Mwanakijiji
Aliulizwa: "Mhe. Je ulikutana na kina Mramba au Yona" Jibu lake ni kuwa "nani nimekutana naye nyie haiwahusu"

Duh, tuna safari ndefu. Hii jeuri huyu kijana anaitoa wapi - when will some of these amateurs ever learn ? -ama ni yale yale ya birds of a feather ya kuleni majani na vijisenti. Tuendeleze mapambano ila tujihadhari na mabweha. Akumulikaye mchana, usiku atakuchoma - hivyo lazima tukae macho.
__________________

Uzuri wa demokrasia ni kwamba unaruhusu kutokubaliana mawazo kistaarabu, wengine inaonekana mkipewa urais itakuwa ni mawazo yenu tu yaani wote lazima tukubali mawazo yenu tu, otherwise tunakuwa kila kitu kuanzia kutumwa mpaka kutumiwa, what a waste thinking!!

Masha ameenda kuwaona watuhumiwa, he did sasa kama tuko serious basi ni kutaka kujua sheria inasema nini, otherwise tunaweza kukubali kutokubaliana lakini sio lazima wote tukubali mawazo ya mtu mmoja tu hapa kwamba he is wrong, kwa sababu he is wrong on what base? Sheria au maneno tu, it is about time sasa Tanzania tukaanza kuwa na sheria zinazoeleweka, kama amefanya makosa kisiasa basi aadhibiwe kwenye kura,

Otherwise, Masha kama binadam ana haki ya kufanya anything, as long as havunji sheria je hapa kuna sheria ya jamhuri imevunjwa? Ajiuzulu kwa sababu gani eti kuwaona marafiki zake rumande ni sababu ya kujiuzulu kwa waziri wa jamhuri, si tutashusha hata hadhi ya kujiuzulu, yaani walioiba richimonduli wajiuzulku na anayeenda kuwaona marafiki zake rumande ajiuzulu?

Itakua serikali ya kusadikika basi!, Masha apewe nafasi ya kujieleza kwa nini ameenda huko kabla ya hizi hukumu!
 
Arguments kuwa alienda kuwatembelea kama raia mwingine does not hold water. Swali la kwanza linalokuja ni je alifuata taratibu zinazomiliki utembeleaji wa raia wa kawaida? Mathlani, je alienda wakati wa kutembelea mahabusu? Je, alionana na hao mahabusu katika sehemu ambayo raia wa kawaida huwa wanawaona mahabusu?

Maswali hayo na mengine magereza wanatakiwa kujibu.

Watu wa magereza wawe makini na utendaji wao.Masha aliingia kama nani kwenye gereza? tuko serious kuuliza hilo swali.

Hao watuhumiwa wakidhurika kwa lolote Askari magereza mtawajibika.Huwezi kuruhusu mtu yeyote aingie gerezani bila taratibu hata kama ni Raisi wa nchi.Ni lazima taratibu zote zifuatwe na protokali za kiziara zote zifuatwe.Kama protokali zilikiukwa askari magereza mkae mkao wa kuwajibika.
Je watu wa magereza mnao ushahidi kuwa mlizingatia taratibu za protokali zote kabla ya kumruhusu kuingia? Mna documentary evidence za kuonyesha kuwa mlizangatia protokali zote yakiwalipukia?

Je ziara yake hiyo ya waziri Masha taratibu zote za protokali za kiserikali zilifuatwa kabla ya yeye kuingia humo gerezani? Kama aliwapelekea sumu ambayo itawaathiri hao watuhumiwa je? Je kama angevamiwa na kuumizwa na hao watuhumiwa kwa hasira walizonazo juu yake pia ingekuwaje? Taratibu na sheria za magereza zilizingatiwa? Kazi kwenu.

Nchi iko vitani na mafisadi .Yeyote aweza dhurika au kudhuru wengine bila kujali cheo chake au hadhi yake kutegemea ana maslahi gani? na ya nani anasimamia? Magereza kuweni makini.

Tunatarajia magereza watatoa jibu tu watake wasitake.Kama wanakauka sasa kutoa jibu wajiandae kulitoa jibu bungeni krefu litakalokuwa na maswali ya nyongeza ya kuwatosha kwenye kikao cha bunge lijalo.Hiyo itakuwa moja ya mada moto.

Uhuru ni wao wajibu sasa maswali ya wana jamii forum au wasubiri bungeni.Uchaguzi ni wao.
 
Nakumbuka wakati Marehemu Ditopile yuko jela,Jk alitaka kwenda kumtembelea baada ya kutoka safari,and he was rightly adviced against it na usalama wa taifa.
Kwangu mimi,sidhani kama ni sahihi kwa Masha kwenda jela kuwatembelea.What does it say,kwamba kama ana uwezo angewaachia? Hivi ni vitu vya kukaa navyo mbali.Inaleta hisia gani kwa wananchi? Pale mahakamani,watuhumiwa hao walizomea sana tu,then wananchi haohao wanakuja kusoma kuwa waziri wao wa mambo ya ndani kaenda kuwatembelea.Wanazidi kudhihirisha kuwa wenye nacho wataendelea kuwa pamoja,hata kwenye nini
 
Hakuna ubaya kwa waziri kutembelea gereza tukumbuke nae na raia ana haki kama raia wengine
 
Hakuna ubaya kwa waziri kutembelea gereza tukumbuke nae na raia ana haki kama raia wengine

Sawa lakini mbona kaenda siku ya kazi?
Ana haki ndiyo ya kwenda kuwajulia khali lakini siku za kuwaona mahabusu si zinajulikana?Kwa nini aende siku ambayo si ya kuwaona mahabusu huoni kama kavunja sheria za gereza hapo katumia dhamana ya uwaziri kuingia gerezani.
 
Hakuna ubaya kwa waziri kutembelea gereza tukumbuke nae na raia ana haki kama raia wengine

Waziri si kama raia wengine.Yeye ni kioo cha serikali na hili hapaswi kulisahau. Matendo yake yote inabidi ajue kuwa yanaweza kutafsiriwa kama ni msimamo wa serikali. Ndiyo maana matendo yake yanapimwa si kwa sheria tu bali kwa ethics vile vile. Je ni ETHICALLY correct kwa waziri, ambae serikali yake imewafungulia mashitaka watuhumiwa kuwatembelea kabla ya hukumu kutolewa? Hatuzungumzii sheria hapa. Kisingizio kuwa sijavunja sheria hakina nafasi hapa. Huyu bwana anasimangwa kwa kuipunguzia credibility serikali ambayo yeye ni kiungo muhimu. Mwinyi hakujiuzuru kwa kuwa amevunja sheria bali kwa sababu kitendo cha kufa mahabusu kiliaibisha na kupunguzia credibility serikali yake. Kiongozi makini, hangojei tume au mahakama imtie hatiani ndiyo awajibike. Matatizo kwetu hili neno kuwajibika halina uzito wowote. Hata kuomba samahani tunapoteleza tunaona kazi!

Tofauti na wengine wanavyofikiria, kujiuzulu si kujivunjia heshima. Huyu bwana akijiuzulu ( hata kama ombi lake litakataliwa) litamjengea sifa ya uadilifu. Mtu makini ambae yuko tayari kuwajibika inapopaswa. Kwa kutojiuzulu ndiko kunakozidi kujenga imani ya arrogance. Kwamba kwa sabau yeye ni bigger than life kwa hiyo hapaswi kuwajibika hata anapokosea. Si anatufanyia favour kuwa waziri wetu!
 
Fundi Mchundo said:
JokaKuu,

Hapa nadhani unakosea. Kwa huyu mheshimiwa kutembelea mahabusu kunatia dosari maamuzi yeyote yatakayotokea dhidi ya watuhumiwa. Wakiachiwa, watu watasema ni kutokana na ujumbe wa huo mkono mzito. Wakifungwa, itasemekana hivyo. Credibility ya the whole judicial system itaonekana ina walakin.

Arguments kuwa alienda kuwatembelea kama raia mwingine does not hold water. Swali la kwanza linalokuja ni je alifuata taratibu zinazomiliki utembeleaji wa raia wa kawaida? Mathlani, je alienda wakati wa kutembelea mahabusu? Je, alionana na hao mahabusu katika sehemu ambayo raia wa kawaida huwa wanawaona mahabusu?

Sasa tunaambiwa kuna simu alipigiwa hakimu, halafu tunasikia kuwa alitumwa na mkono mzito n.k. Kwa nafasi yake kama wakili aliyebobea, alipaswa kuuambia huo mkono mzito kuwa hatua kama hiyo ni improper to the extreme!

Ishu ya kwamba alitumia gari lake binfsi is not petty at all. Kwa kufanya hivi ndiko kunajenga hoja kuwa alienda kule kama raia wa kawaida and not katika capacity yake kama waziri. kwa kufanya hivi vile vile kunaleta hisia kuwa safari yenyewe ilikuwa ya kujificha. Which brings other issues to the fore!

Unakuwa naive unaposema kuwa yeye kama waziri hawezi kuvuruga kesi yenyewe. Huyu kama waziri ni sehemu ya kabinet kwa hiyo ana sikio la viongozi wote wa juu katika nchi yetu. Huyu akimpigia simu hakimu na kusema kuwa ni maagizo kutoka mkono mzito, ataaminika. Hapana, huyu si kama Fundi Mchundo. Huyu ni Mkuu katika nchi yetu.

Kama hakutumwa, he should apologise and tender his resignation. Though I am not holding my breath on this one.

Nadhani wenzetu wanasema; Justice should not only be done but it should be SEEN to be done. Au kitu kama hicho.

Amandla......

Fundi Mchundo,

..nimependa hiyo quote hapo niliyoisisitiza kwa rangi ya blue.

..so far nimeridhika na mwenendo wa hii kesi. kwa mtizamo wangu mambo yote yamekwenda kwa kufuata taratibu.

..sasa sintokwenda na kuanza ku-quote na kugeuza-geuza kauli zako, you know how it is sometimes done in here, na kuanza kuleta ubishi usio na msingi.

..kitu kimoja ninachoweza kusema ni kwamba habari hii ya Waziri Masha kutembelea rumande ya Keko, imeletwa kwa nia ya kumshawishi msomaji kwamba, Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa pale kwa nia ya kuvuruga kesi hii kwa manufaa ya washitakiwa Mramba na Yona.

..wananchi tunapaswa kujiuliza maswali ya msingi na kujiridhisha kabla ya kutoa conclusions zozote. nafurahi kwamba hata wewe umeuliza maswali magumu, hata kama ni tofauti na yale niliyouliza mimi.

..mwisho, mimi najizuia kusikiliza "dataz" na kuzimeza nzima-nzima. at least lazima niulize maswali magumu kidogo.

..kwa mfano, kuna habari za simu kupigwa mahakamani wakati Hakimu ana-sort out suala la dhamana. vilevile kuna aliyedai kwamba hakimu alisisitiza kwamba lazima washitakiwa watoe dhamana in cash kwasababu wamezoea kushika pesa.

..kwa mtizamo wangu pamoja na dataz/fununu hizo, lakini mwenendo mzima wa kesi mpaka sasa hivi unaridhisha.
 
..mwisho, mimi najizuia kusikiliza "dataz" na kuzimeza nzima-nzima. at least lazima niulize maswali magumu kidogo.

..kwa mfano, kuna habari za simu kupigwa mahakamani wakati Hakimu ana-sort out suala la dhamana. vilevile kuna aliyedai kwamba hakimu alisisitiza kwamba lazima washitakiwa watoe dhamana in cash kwasababu wamezoea kushika pesa.

JokaKuu,

Hata mimi hizi za simu, mkono mzito n.k. nimezichukua with a pinch of salt! Lakini kama Mheshimiwa alienda kuwatembelea hawa mahabusu ( nakubaliana nawe kuwa kuna uwezekano anasingiziwa) anastahili kuwajibika.
 
Fundi Mchundo said:
JokaKuu,
Hata mimi hizi za simu, mkono mzito n.k. nimezichukua with a pinch of salt! Lakini kama Mheshimiwa alienda kuwatembelea hawa mahabusu ( nakubaliana nawe kuwa kuna uwezekano anasingiziwa) anastahili kuwajibika.

Fundi Mchundo,

..kuna "dataz" ambazo zimekuja ku-prove kuwa ni za kweli. hilo lazima nikiri. lakini kuna nyingine mhhh...

..sidhani kama Masha amezushiwa hii habari. lakini bado sijaridhika na madai kwamba Masha amekiuka taratibu za madaraka yake ktk kutembelea rumande ya Keko na kuonana na mahabusu[mramba na yona].
 
..mwisho, mimi najizuia kusikiliza "dataz" na kuzimeza nzima-nzima. at least lazima niulize maswali magumu kidogo.

..kwa mfano, kuna habari za simu kupigwa mahakamani wakati Hakimu ana-sort out suala la dhamana.

Baada ya kujiuzulu tu Lowassa, siku moja aliamua kwenda kwenye TV station moja na kufanya interview, akiwa kati kati ya ile interview ilipigwa simu na mkono mzito kuwaamuru waizime ile interview mara moja na ikazimwa, kwa hiyo ya mkono mzito na simu sio mapya,

Wa-Tanzania sasa tunao wakati mzuri wa kuanza kuishi kwa sheria, badala ya maneno mengi ya kujaribu kulinganisha siasa za Europe/USA na bongo, sisi bongo hatujafikia huko na hata huko majuu zinazofuatwa ni sheria sio maneno maneno!
 
FMES,

..ningekuwa niko karibu na watoa "dataz" kama wewe mwenzetu then I would be telling a different story here. wewe mwenzetu unaweza kuzithibitisha.

..sasa kwa nafasi niliyonayo hapa jamvini siwezi kutumia some of this "dataz" in my decision process. hicho ndicho ninachojaribu kusisitiza hapa.
 
- Mkuu Joka kwenye siasa kuna ukweli na speculations, binafsi ninaifahamu sana nchi yangu bongo, nikisoma dataz za aina yoyote zile za kisiasa sina tatizo hata siku moja kuzichambua, kujua ukweli na mapungufu ulipo, siamini hata siku moja kwamba kuna mtu anaweza kuja hapa ku-mislead wengine kwa makusudi, wanatoa hizo dataz ni binadam na wanaozitengenza hizi dataz kwa matendo yao ni binadam pia, na tunaozipokea na kuzitoa hapa ni binadam pia, wote tuna mapungufu.

- Dataz ni dataz, kwamwe haziwezi kutumika as a guide to a decision process, ni muongozo tu kwa wale ambao wapo interested na siasa na kujua ya behind the scene, ipi ni dataz ya kweli na ipi sio hata mimi sina uwezo wa kujua, ila nikijumlisha dots ninaishia kupata jawabu, kwa faida yangu kwanza. Otherwise, ninakuelewa sana lakini samahani kwamba hatuwezi kuweka dataz zote kama zilivyo hapa uwanjani, lakini tunajitahidi as much as we can.

- Sasa binafsi ninaposikia Masha ameenda Rumande kuwaona watuhumiwa wa political high profile kama hawa, kwanza ninajiuliza swali moja kwamba Masha anajiamini nini? Hii jeuri anaitoa wapi? Halafu ndio ninaenda mbele zaidi hata kumpigia mwenyewe ikibidi.

Thanxs!
 
FMES said:

..asante.

..tuko pamoja ktk maelezo yako niliyoyanukuu.
 
Hapa tupo ukurasa moja - I only hope unatambua kwa nini wengine tumekuwa so critical na hiki kitendo cha Masha. Kitendo chake hicho kimezidi kuchafua credibility ya serikali na kwenye utawala makini angetakiwa awajibike.
 
Bado natafakari kauli hii kwani bado haijafutwa, kusahihishwa au kukanushwa.

Mzee Mwanakijiji ujue kuwa kuna watu wa aina nyingi hapa jamvini. Sasa sijui nini zaidi ya maelezo ya Masha mwenyewe aliyethibitisha kuwa ameenda kutembelea keko, yanayoweza kuthibitisha story hii na huyo ndugu anayesema ni rumour, inaonekana kuwa yeke ndio rumour na kauli ya Masha ni ukweli. Usijichose ndugu.
 
Back
Top Bottom