News of Rwanda yaandika kuwa Rais Jakaya Kikwete anaweza kuwa na asili ya Gitega Burundi....

News of Rwanda yaandika kuwa Rais Jakaya Kikwete anaweza kuwa na asili ya Gitega Burundi....

Status
Not open for further replies.
mambo ya ajabu kabisa haya,sasa sensorship kwa bloggers au wenye mitandao ya nini? JF wameenza kufyeka topic/post za watu especially zinazosema kuhusu JK...something fish hapa.
 
Nadhani umefika muda wa kupuuza hizi propaganda za Kagame kwenye mitandao sisi tujikite kwenye propaganda za kidiplomasia kimya kimya na matokeo yake aje kuwa kama Taylor.
Hiyo report has nothing to do with Kagame ni wikileaks ndio waliandika 2005,issue hapa ni kubwa kuliko hiyo report ni"sensorship" kutaka crackdown bloggers/net users....mlivyokariri kila kitu mnamlaumu kagame.
 
this is another shit out of the vampire!. These pipo has no brain in their skull and ya can simply gues what they gonna say the next day when it comes a simple thing which needs no attention, when it's something clucial for the country expect no one to give a statement. We didn't see them giving a statement on the drugs sagga neither salva nor this man. Their conscious minds are awake but the subconscious minds are not within them.
 
Huu nao ni upuuzi mwingine...kukanusha taarifa za mitandaoni za Rwanda....what about za hapa nchini kuhusu dawa za kulevya ....

Any way hizi thread zilinifanya kuji-ban mwenyewe 10 dys. Watu kuchangia kwa mihemuko ya utaifa....kwa id fake...., ukanushaji wa taarifa hizi nao...hivyo hivyo.....hatuambiwi yule mhamiji haramu anayeshona nguo za Salma....na yule aliyeolewa na nduguye Kikwete kutoka Mkugwa miaka hiyo...

By the way operation imefikia wapi? logistics zake zikoje? Ni kweli kuna warundi na wakongo wamerudi au ni wanyarwanda tu...6 dys late after deadline ndo Nchimbi anajitokeza leo na matamko....msipofanya zoezi ili kwa weledi na endelevu....kama halitawachanganya...maana id za watanzania hamna mpaka mfuate historia za vizazi...sijui watu wamijini itakuwaje...mtaishushia hadhi Tanzania.
 
BTW,
Hii ni issue Personal ya JK na Marehemu Habyarimana, kwa Sababu hatujaambiwa ushemeji wao ukoje ukoje ...
Halafu sioni issue Hapa Mbona, kwani kuna ubaya gani hawa watu kuwa Mashemeji ????
 
tatizo magogoni wamejaa wajanja wajanja muoneni huyo anavoropoka ujinga.
 
Huu nao ni upuuzi mwingine...kukanusha taarifa za mitandaoni za Rwanda....what about za hapa nchini kuhusu dawa za kulevya ....

Any way hizi thread zilinifanya kuji-ban mwenyewe 10 dys. Watu kuchangia kwa mihemuko ya utaifa....kwa id fake...., ukanushaji wa taarifa hizi nao...hivyo hivyo.....hatuambiwi yule mhamiji haramu anayeshona nguo za Salma....na yule aliyeolewa na nduguye Kikwete kutoka Mkugwa miaka hiyo...

By the way operation imefikia wapi? logistics zake zikoje? Ni kweli kuna warundi na wakongo wamerudi au ni wanyarwanda tu...6 dys late after deadline ndo Nchimbi anajitokeza leo na matamko....msipofanya zoezi ili kwa weledi na endelevu....kama halitawachanganya...maana id za watanzania hamna mpaka mfuate historia za vizazi...sijui watu wamijini itakuwaje...mtaishushia hadhi Tanzania.

Mkuu ndiyo shida ya kutawaliwa na watu ambao hawajui walitafuta madaraka kuwafanyia nini wananchi. Matokeo wanajitumbukiza ktk mambo mengine ambayo mwisho wake watazidi kujionyesha walivyo wapuuzi!

Suhala la Wahamiaji ktk mikoa ya Kagera na Kigoma ni kielelezo cha kushindwa kwa watawala kwasababu ya watendaji wala rushwa na dhaifu. Matokeo ni operesheni za kipuuzi ambazo zitaishia kuwabambikia Watanzania masikini huko mipakani kwamba ni wahamiaji haramu.

Operesheni hizi huwezi zisikia nje ya mikoa hii licha ya maelfu ya wahamiaji haramu toka Uchina,Msumbiji,Malawi,Ngazija,Pakistan,Bangladesh na Arabuni kujazana nchini! Ndugu zangu Wahaya kama unafanana na Watutsi jiandae kupelekwa kwa nguvu kwa Kagame
 
Hayo ya Rwanda na kutudhibiti sisi hapa nchini, WAPI NA WAPI??.
Wengi wa WaTZ wanamtetea Rais Kikwete dhidi ya Dikteta Kagame, kwa heshima ya Taifa hili. Sasa tena wanapendekeza tudhibitiwe!!!. Huu ni upuuzi. Upuuzi mkuu wa msemji wa serikali ya Wakurupukaji. Huyo msemaji ninamashaka hajui kinacho endelea nchini ila kaelekezwa na mafisadi fulani kwa malengo ya kisiasa.
Kumbeee!!, wanataka kutumia ushenzi wa Kagame, kukandamiza uhuru wa watanzania tunao ipenda nchi hii.
 
Ila huu utamaduni wa vyombo vya habari kuweka uwanja wa mapambano kwenye cyber si mzuri, watu hawafikilii, ni kutukana tu, hakuna hoja hata moja!

KAGAME IS A KILLER........Hakuna ubishi hapa. Time has come for his life to be taken away. No more mercy, we do not need leaders like him.
 
Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mitandao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda, marehemu Juvenal Habyarimana.

“Taarifa hizi siyo za kweli na nafikiri taarifa zimeandaliwa kwa ajili ya kumpaka matope Mheshimiwa Rais. Kama kuna taarifa zozote basi tunaweza kutoa ufafanuzi lakini taarifa hizo siyo za kweli na bahati mbaya zimeendelea kujirudia na zinatoka kwenye mitandao mingi hasa kutoka Rwanda,” amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.

Ili kukabiliana na taarifa potofu, Mwambene amesema, “...katika mabadiliko ambayo yanapendekezwa katika Serikali ya ku-deal na tatizo hili, tunakuja na pendekezo la kisheria litakalohakikisha kwamba tunamtambua kila mtumiaji wa mitandao hii kwa mfano blog. Nafikiri mmeanza kuona kuna training sasa zinafaanyika kuhakikisha kwa mfano --- wote wenye blogu unakuta wengi siyo waandishi wa habari, hajasomea uandishi wa habari lakini blogu yake inafanya kazi kama gazeti --- tulichokifanya sasa na nafikiri tutaendelea mpaka uje utaratibu wa kisheria, tunamtambua kila mtumiaji wa iwe ni blog, iwe ni Twitter, iwe ni internet cafe...” alisema Mwambene.

Source: wavuti.com - Blog

KWAKO BWANA MKUBWA

(Mwambene)

Mheshimiwa, kwanza kabisa nianze na kukushukuru kwa kuwa mwepesi kujibu na kufanya masahihisho kuhusu upotoshaji wa vyombo vya habari vya Rwanda. Ila nikuombe jambo moja kuhusu pendekezo lako kwa watumia blog kwamba ukifanya kama ulivyosema hapo juu, utakuwa huboreshi bali kuongeza tatizo litakalo leta malalamiko mengi dhidi ya Rais na serikali yake: Kama itatokea hivyo basi Rais atalazimika kujitetea mwenyewe, la pili ni kukuachisha kazi wewe na kumpa mwingine anayeweza kuboresha vyombo vya kijamii na habari. Kama huo ndio ushauri anaopewa rais juu ya vyombo vya habari basi anapotoshwa. Mimi nashauri kuwa uzingatie kukanusha habari na kuuelimisha umma juu ya yote yanayo andikwa na watu wa Kagame ukijuwa kuwa Tanzania ipo katika vita baridi na Rwanda. Na ndiyo maana ya maneno yote hayo ya kipuuzi kutoka Rwanda. Sasa tunataka msemaji wa serikali anae elewa maana ya matusi ya watu wa Kagame kwa kina. Na si kujibu kwa kutumia hoja nyepesi.

Mimi nadhani uondoe hiyo hoja ya kushughulikia hivyo vyombo (social media) angalau kwa sasa, la msingi hapa ni kuielimisha jamii ya watanzania unaowatumikia na si kushughulikia vyombo wanavyopokelea habari. ukifanya hivyo utakuwa umeepusha lawama ambazo zingeleekezwa kwako.

OMBI LANGU KWAKO

Nakuomba ulipanue jibu lako kwa watu wa Kagame kuwa Rais wetu siyo shemejie na Habyarimana. Naomba uandike kwa upana zaidi. Ikiwezekena tumia Library weka references za kutosha. Tumia maneno imara zaidi na si kwa ufupi kama ulivyofanya. Ukijua kuwa wataandika sababu nyingine tena maana wana lao moyoni.

Ahsante mheshimiwa

Idumu Tanzania yetu na watu wake.
 
Ninaamini kuna wafanyakazi waandamizi wa serikali wanachukua au kupewa jukumu la kuwa wasemaji au waratibu kuhusiana na taratibu, sheria na muundo wa mawasiliano kwa njia ya utandawazi bila hata kujua kilicho nyuma ya taratibu, sheria na muundo wake.

Watawezaje ku-regulate utandawazi wakati hata Ofisi ya Rais bado inatumia mbinu za kijima katika mawasiliano yake.

Huyu Assah Mwambene nina wasiwasi kama anafahamu kile anachokisema na implication yake nchini ambapo zaidi ya 29% ya budget inategemea wahisani wanaokuja na masharti kama wapendavyo.
 
Ili kukabiliana na taarifa potofu, Mwambene amesema, “...katika mabadiliko ambayo yanapendekezwa katika Serikali ya ku-deal na tatizo hili, tunakuja na pendekezo la kisheria litakalohakikisha kwamba tunamtambua kila mtumiaji wa mitandao hii kwa mfano blog. Nafikiri mmeanza kuona kuna training sasa zinafaanyika kuhakikisha kwa mfano --- wote wenye blogu unakuta wengi siyo waandishi wa habari, hajasomea uandishi wa habari lakini blogu yake inafanya kazi kama gazeti --- tulichokifanya sasa na nafikiri tutaendelea mpaka uje utaratibu wa kisheria, tunamtambua kila mtumiaji wa iwe ni blog, iwe ni Twitter, iwe ni internet cafe...” alisema Mwambene.
Non sense .. yote haya kwa kuwa tu First Lady kaguswa?
 
Ninaamini kuna wafanyakazi waandamizi wa serikali wanachukua au kupewa jukumu la kuwa wasemaji au waratibu kuhusiana na taratibu, sheria na muundo wa mawasiliano kwa njia ya utandawazi bila hata kujua kilicho nyuma ya taratibu, sheria na muundo wake.

Watawezaje ku-regulate utandawazi wakati hata Ofisi ya Rais bado inatumia mbinu za kijima katika mawasiliano yake.

Huyu Assah Mwambene nina wasiwasi kama anafahamu kile anachokisema na implication yake nchini ambapo zaidi ya 29% ya budget inategemea wahisani wanaokuja na masharti kama wapendavyo.
Sasa asiposema atajulikanaje anafanya kazi. Just throw anything hata kama hakina facts.
Labda nihoji weledi na uelewa wake! hizi kazi za kupeana zina matatizo sana.

Halfu serikali inapswa kujibu upuuzi wa blog za Rwanda kweli!
 
Kaka,

Assah alikua msemaji wa wizara ya mambo ya nje.Angeweza kufanya vizuri zaidi ya hapa kwa exposure na weledi aliotakiwa kuwa nao
 
Kaka,

Assah alikua msemaji wa wizara ya mambo ya nje.Angeweza kufanya vizuri zaidi ya hapa kwa exposure na weledi aliotakiwa kuwa nao
Nakubaliana kabisa kwamba hakutumia exposure yake kupambanua mambo.

Kwanza alitakiwa aelewe kuwa kuwajibu watu hao wa blog ni kama kuwa promote na hadithi zao za kutunga, kesho watakuja na uongo mwingine. Mambo kama hayo huwa yanamalizwa huku katika forum. Mbona wamekuja hapa JF na madai lukuki siku hizi hawajishughulishi, kila habari imegonga mwamba.

Pili, alitakiwa ajue internet inafanya kazi vipi. Sasa atawezaje kumshtaki Mnyarwanda aliyetumwa kuichafua Tanzania akiwa huko Rwanda? Sisi hapa tunasoma habari za dunia na tunatuma kwa wenzetu sasa atazuiaje. Na kibaya anatisha hata katika interent cafe watajulikana~! huyu yupo out of touch ndio maana nasema aliamua tu kusema leo.

Viongozi lazima wajue umuhimu wa teknolojia ya leo, enzi za one way traffic zimeisha miongo mingi iliyopita.
Ukimuona mtu anaogopa blog na forum kama Assah angalia uadilifu wake. Huna sababu ya kuogopa dudu lislokudhuru!

Ben, huyu bwana anaweza kuwa alifanya kazi maeneo mengi na ana ceritificate za kutosha, tatizo lake vitu hivyo havimsaidii katika ku deliver ndio maana nahoji weledi wake
 
Sasa asiposema atajulikanaje anafanya kazi. Just throw anything hata kama hakina facts.
Labda nihoji weledi na uelewa wake! hizi kazi za kupeana zina matatizo sana.

Halfu serikali inapswa kujibu upuuzi wa blog za Rwanda kweli!
Mkuu Nguruvi3 , Hawa watu huwa wananishangaza sana. Kwenye mambo ya msingi ambayo wanatakiwa kuwaeleza Watanzania wala huwaoni hata kutoa pua zao lakini wanakuwa very active kwenye mambo ambayo ni trivia.

Wanatumia nguvu kubwa kukanusha mambo ya kwenye mitandao na vijiwe vya kahawa Rwanda wakati tuna mambo muhimu nchini yanayohitaji clarification kama ya vile 'waharifu' kusafirishwa na helikopta ya serikali kwenda kusomewa mashitaka na kurudishwa tena mahabusu.

Kwani ni dhambi au kosa kuwa na uhusiano wa kindugu au kirafiki na Habyarimana?. Toka lini binadamu akapata uwezo wa kuchagua ndugu.

Hizi political correctness zinawapeleka kubaya.
 
Last edited by a moderator:
Tamko ni jepesi sana, sioni mahali nichangie au kuunga tamko.

MAELEZO: Jipangeni vema na msikurupuke, mnatuaibisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom