Hapo we mwenyewe hujielewi au huelewi kinachoendelea
Nay wa mitego Yeye ndoto yake ni lowassa kuwa Raisi na sio mabadiliko wala ukawa...
Kwenye Listi yangu sijamtaja Nay wa Mitego kama Msanii wa Hip Hop anayesapoti harakati zinazoendana na Misingi ya Hip Hop:
1. Simtambui na hajitambulishi kama msanii wa Hip Hop yeye ni Mbongo fleva ambaye kuna baadhi ya nyimbo zake kafanya Hip Hop. Na hata nyimbo alizofanya zenye hadhi ya Hip hop hazipo katika misingi ya kiharakati zipo katika battle na entertainment.
HAO WENGINE wakina prof j wote wameangalia awapi pa kutokea kisiasa chadema ndio imewafaa suala la harakati sijui hip hop hakunaa hata hivyo haiingiliani na Suala la kuunga mkono chama fulani labda kama ni kukiuka haki za kibinadamu
Hiyo listi yangu sijawaweka Profesa Jay na SUGU sababu ya kugombea Ubunge kwa Tiketi ya CDM bali kwa nyimbo zao zipo kiharakati zaidi (Harakati za maisha ya watu wa chini, Uonevu, Uvunjifu wa haki za binadamu, ubaguzi wa ajira n.k) rejea Nyimbo zao za zamani:
SUGU:------Mikononi mwa Polisi (Kwa ajili ya mwanafunzi wa Iyunga Michael aliyeuawa mikononi mwa polisi 1998), HAKI feat justine Kalikawe (Machinga Mbeya), Deiwaka, Hali halisi, Money money pesa, Mambo ya fedha, Nje ya Bongo, Ndani ya bongo n.k
PROFESA JAY:-------Chemsha bongo feat HBC, Machozi, Jasho na Damu, Ndio mzee, sio mzee, Msinitenge, Taifa la kesho n.k
Kwa hiyo hawajajikita kwenye nyimbo za kuchochea ulevi, ngono na burudani zaidi bali kuelimisha na kuwakumbusha watawala. kwa hiyo milengo yao imeendana na vyama walikokwenda kugombea. Kwa hiyo akili, upeo na mlengo wake ndio utafanana na chama atakachopenda kukisapoti. Kitakuwa kitu cha ajabu msanii kama ROMA anayewaponda kwenye CCM kwenye nyimbo zake aende CCM kuomba ridhaa ya uongozi si kitu rahisi.
Bahati mbaya nimewasahau malejendari kama Afande Sele na Kalapina walioko ACT wazalendo maana nyimbo zao zipo kiharakati na wamekwenda kwenye vyama vya kiharakati.
Wasanii wengi mwanaosifia pombe, ngono na wapo kiburudani zaidi kwenye nyimbo mpaka maisha yao wanasapoti au wapo CCM sababu CCM itikadi zao sio za kiharakati wao ndio watawala na wanakula bata kwa kwenda mbele ndio maana kwenye kampeni zao wapo kiburudani zaidi na wasanii wengi kutoa burudani na kulipwa pesa na kulisha watu ubwabwa.