Neymar Jr amekurupuka kwenda PSG

Neymar Jr amekurupuka kwenda PSG

BINAFSI sitamsamehe Neymar. Katika umri wa miaka 25, nyakati unazotamani kuona akielekea juu kabisa ya kilele cha ubora duniani, anachagua kuondoka Barcelona na kwenda PSG.

Kwa mchezaji wa aina yake mwenye uwezo kama wake, unatokaje kirahisi katika ligi bora duniani na kuchagua kucheza Ligue 1, ligi namba 5 kwa ubora barani Ulaya?

Tatizo ni nini? Pesa au ni kweli amechoshwa kuwa nyuma ya kivuli cha Lionel Messi? Labda sababu ya kwanza, vijana wa Amerika Kusini mioyo yao haijapishana sana na Waafrika.

Dhiki kali walizokumbana nazo utotoni zilishaichoma mioyo yao na kuiacha ikiwa na hasira kali ya kimaisha. Ilipo pesa, walipo wao.

Hapa kwenye kukimbia kivuli cha Leo Messi, ndiko kunakonipa shaka kidogo. Hapa Neymar anatudanganya, tena uongo mbaya wenye kukera.

Sikatai, kivuli cha Messi kimemficha sana. Ubora wake hauzungumzwi tena. Neymar yule tuliyemsikia akiwa Santos, si huyu wa sasa tuliyenaye hapa Nou Camp.

Chochote atakachofanya kimeshafanya na Messi tayari. Barca wana mfalme mmoja tu, La Pulga pekee. Kwa alipofika Neymar alitakiwa kuondoka Barca.

Lakini kama kweli sababu ni kusaka ufalme wa soka duniani, Neymar alitakiwa kujiuliza mara mbili, ni wapi anaweza kwenda na kutengeneza ufalme wa dunia?

Unakimbiaje kivuli cha Messi kwa kwenda PSG? Dunia ya sasa inaanza vipi kutoa mfalme wa soka katika ligi dhaifu kama ile ya Ligue 1?

Mtazame Zlatan Ibrahimov. Ni mfalme wa PSG. Ni mfalme wa Paris, ni gwiji wa Ligue 1, lakini yuko mbali na hadhi ya wafalme wa dunia. Neymar analijua hili?

Kwa miaka 10 sasa Ligue 1 imeendelea kuwa ligi kubwa ya kawaida duniani. Haisisimui kabisa. Wachezaji bora hudumu kwa msimu kadhaa kisha huamua kusaka malisho sehemu nyingine.

Eden Hazard amepata heshima aliyonayo baada ya kucheza Premier League. N’golo Kante pia. Hivyo hivyo kwa Riyad Mahrez na Didier Drogba.

Mtazame tena Kylian Mbappe? Pamoja na ubora wake, dunia imekuwa na mashaka naye bado. Wengi hawaamini kama ni mkali kama takwimu zinavyosema. Kwanini? Ni takwimu za Ligue 1.

Watu hawaiamini sana ligi ile, ni ngumu sana kuona akiibuka mfalme wa dunia maeneo yale. Neymar asiendelee kutudanganya. Kivuli cha Messi hakiwezi kufutwa kwa nyota anayevaa jezi ya PSG. Ni uongo huu.

Kama kweli Cristiano Ronaldo alimshauri kufikiria mara mbili kabla hajatoka Barcelona, basi CR7 ni mkubwa sana kifikra katika dunia ya soka ya sasa. Tusishangae anavyozidi kufanikiwa.

Ni klabu mbili tu ambazo Neymar angeweza kwenda na kuupata ufalme anaoutaka. Real Madrid na Manchester United. Lakini tayari Madrid wanaye Ronaldo, chaguo sahihi kwake lilikuwa Old Trafford.

Neymar angeweza kusimama na kugombea ufalme wa dunia akiwa na jezi ya Manchester. Pale ndipo mahala anakoweza kushindana na kina Leo Messi na Ronaldo, si PSG.

Ukweli mchungu unaofichwa na Neymar na baba yake ni huu, kinachowakimbiza Barcelona ni pesa tu. Hizi stori za Ufalme ni uongo tu.

Neymar hana shida na mataji tena, hana shida na tuzo ya Ballon d’Or. Shida yake ni pesa tu. Na kwa PSG amekutana na wendawazimu wa biashara, watampatia.

Tayari kuna ofa ya mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki. Atapimwa afya katika hospitali ya kifahari kule Qatar, kisha atatambulishwa pale uliposimama mnara wa Paris maarufu kama mnasa wa Eiffel. Maisha yanataka nini tena zaidi?

PSG wanamhitaji Neymar kibiashara. Hawana shida ya miguu yake, wana shida na sura yake. Neymar ndiye mtu pekee duniani atakayeweza kukaa kwenye matangazo ya ndege zao na wakafanya biashara kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hutomsamehe kwa lipi mkuu huyo Dogo unayemuongelea ana washauri wabobezi, wanasheria, na anamsimamizi katika masuala yake ya soka kuna kitu wamekiona Kwa pamoja wamejadili wameona inafaa-mwache Dogo anyoshe yake hana cha kupoteza kuchukua kila kitu akiwa na Barca

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Binamu kitu fedha! Ukiwa nacho hujui nini maana ya shida.kijana miguu yake inamlipa.Na wewe kama mjomba angewekeza miaka ile sasa hivi ushakuwa CEO wa ile kampuni.kwa nini binamu umetupa fimbo umetegemea mbio? Mkimbizeni siyo sawa na mkamateni.
 
Mbona hujatoa Credit pale ulipoitoa hii Article?

Umeifannya kama umeandika wewe
Kwelii kabisa Mkuu sidhani kama yeye ndo kaandika. ..Kwa mtiririko huu wa mawazo nahisi huyu ni Edo kumwembe ndo kaandika


Nokia ya Torch
 
Kwelii kabisa Mkuu sidhani kama yeye ndo kaandika. ..Kwa mtiririko huu wa mawazo nahisi huyu ni Edo kumwembe ndo kaandika


Nokia ya Torch
Wala sio Edo Mkuu, nimeisoma kwenye Website ya Shafii Dauda, zimepita siku 3-4 hivi.
 
Pambana na maisha yako mwache atafute pesa vikombe hata bachelor tunavyo
 
mimi nipo kati kati. neymar ni brand kubwa ndio ila PSG sio. timu ina mchango mkubwa sana kwenye kumpatia hela mchezaji sababu binadamu tunapenda sana kununua vitu kwa ushabiki.

mfano mzuri muangalie bastian na memphis depay, walikuwa ni wajinga wajinga tu kwenye biashara, lakini ghafla walivyokuja man utd wakabadilika,

kwenye mauzo ya jezi kidunia depay akawa watatu na bastian akawa wa nne, sasa jiulize depay na bastian wanastahili kuuza jezi kulika neymar, hazard, aguero, sanchez, suarez, bale, na masuper star wengine? jibu nafkiri unalijua

hivyo hapo unaona mchango wa timu kwenye kumuuza mchezaji na kumpa umaarufu na hela.

sitashangaa kwa mshahara wote huo lakini still akaja akapitwa kwenye hela na wachezaji wengine ambao watapata hela zaidi.

Dogo atapata mikataba minono ya kutangaza world cup ya qatar

Halaf tukumbuke paris ni mji wa kibiashara sana nina uhakika atapata pesa nyingi huko pia
 
Huyo ronaldo mwenyewe angepata mkataba huo kama wa neymar angeondoka....mpira pesa ndio maana neymar alitoka kwao brazil akapewa hela ndefu na barca la sivyo angebaki kucheza santos mpk leo
 
Neymar ata shine psg then atahamia Real Madrid after two years...
 
Nachokiona mie neymar atakaa psg kwa misimu 2 tu kisha ataenda man united mark my words
 
Kilichomfanya Neymar asepe ni barca kutouona mchango wake na kuuthamini, ilitokea gemu ya PSG pale Neymar alipopachika magoli mawili katika kusawazisha halafu eti Messi akaitwa Hero. Ndio akajua kuwa barca wao ni messi tu.

Afu barca si walikuwa wanamtaka Veratti? Wakaambiwa na rais wa PSG wasijaribu kuwachokonoa wachezaji wao mana yoyote atakaejarobu basi hayupo salama. Barca wakajifanya wajuaji kwenda kwa veratti PSG wakajibu mashambulizi tena kihuni zaidi, hawakutoa ndururu Ney kajinunua mweenyewena Barca wamemkosa Veratti
 
With 25 years old; a contract worth £782,000-a-week for FIVE YEARS is not something you would want to kick into a dust-bin. Hajakurupuka. Dogo keshashinda mataji mengi mno na ni muda sasa wa kuvuta mpunga. Kama ni kukurupuka, labda ni PSG ndo wamekurupuka,
Very Good [emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ache Neymar apige hela asee hizo bil 1 kwa wiki yani hapo kwa mwezi tu bil5...tuzo kitu gani asee
 
Mleta uzi unakadi number ngapi ya Barca
pili Pesa kitu nyingine brother
 
Back
Top Bottom