Neymar Jr kipaji cha soka kilichoshindwa kufikia malengo

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Nimeona taarifa Neymar Jr anarejea zake kwao Santos kutokea Uarabuni. Kipaji maridhawa kilichoenda na maji.

Neymar alitajwa kama mmoja ya wachezaji bora watakaovunja ufalme wa Messi na Ronaldo, lakini wapi!!

Neymar baada ya kuona ameshindwa kuwa mfalme Barcelona akakimbilia PSG ghafla na Messi nae akaibuka hukohuko🤣🤣

Neymar akashawishika na pesa nyingi za mafuta, akakimbilia uarabuni kwenye klabu ya Al Hilal.

Huwezi amini, kwa misimu miwili aliyokaa Al Hilal, amecheza mechi tatu tu na hakufunga goli lolote. Majeraha yalimuandama!!

Na sasa anarejea nyumbani, Santos alikoanzia maisha. Uamuzi sahihi hasa baada ya kula pesa za kutosha za mwarabu.

Kwangu mimi Neymar ni kama amefeli, hajafikia wala kukidhi matarajio makubwa ya wapenda kandanda ambao walitabiri makubwa zaidi kwake.
 
Ubishoo wa kiBrazil nao umechangia kumfanya ashindwe kufikia malengo.

Ronaldo & Messi ni wanaume wa kazi kweli kweli na nidhamu ya hali ya juu na wote wako busy na mpira na familia zao pekee hawana mambo mengi.
 
Kaharibu mwenyewe
Ukiondoa Barcelona team zingine zote alikuwa liability kuliko asset
Aende binafsi ningependa kuona ana staafu kuliko kuendelea kuweka hasira kwa mashabiki
Mitrovic kufanya kazi kubwa pale Hilal Neymar kaja kuvaa medal
 
Nimeona taarifa Neymar Jr anarejea zake kwao Santos kutokea Uarabuni. Kipaji maridhawa kilichoenda na maji.

Neymar alitajwa kama mmoja ya wachezaji bora watakaovunja ufalme wa Messi na Ronaldo, lakini wapi!!

Neymar baada ya kuona ameshindwa kuwa mfalme Barcelona akakimbilia PSG ghafla na Messi nae akaibuka hukohuko
 
Nimeona taarifa Neymar Jr anarejea zake kwao Santos kutokea Uarabuni. Kipaji maridhawa kilichoenda na maji.

Neymar alitajwa kama mmoja ya wachezaji bora watakaovunja ufalme wa Messi na Ronaldo, lakini wapi!!

Neymar baada ya kuona ameshindwa kuwa mfalme Barcelona akakimbilia PSG ghafla na Messi nae akaibuka hukohuko🤣🤣

Neymar akashawishika na pesa nyingi za mafuta, akakimbilia uarabuni kwenye klabu ya Al Hilal.

Huwezi amini, kwa misimu miwili aliyokaa Al Hilal, amecheza mechi tatu tu na hakufunga goli lolote. Majeraha yalimuandama!!

Na sasa anarejea nyumbani, Santos alikoanzia maisha. Uamuzi sahihi hasa baada ya kula pesa za kutosha za mwarabu.

Kwangu mimi Neymar ni kama amefeli, hajafikia wala kukidhi matarajio makubwa ya wapenda kandanda ambao walitabiri makubwa zaidi kwake.
Discipline ni msingi WA Mafanikio yoyote ....Neymar ana kipaji ila Hana nidhamu ya Yale anayofanya mfano Ronaldo ni wakawaida Sana sasa hivi ila ana discipline ya kufanya mazoezi na kupambana hilo ndilo linalomweka sokoni mpaka sasa
 
Keshakuwa bwenyenye mpira umemshinda huko Santos ndio anaenda kuwa na kitambi mazima
 
KWANGU MIMI NEYMAR NI MCHEZAJI WA KAWAIDA MNO, NI MCHEZAJI MDOGO MWENYE MBWEMBWE NYINGI ASIYE NA KIPAJI.

Amejaa ujanja ujanja mwingi , kuumia na kuanguka kila siku.

Neymar ameihadaa sana Dunia.

MCHEZAJI GOIGOI.
 
Back
Top Bottom