DOKEZO NFRA inahujumu mfumo wa Stakabadhi Ghalani

DOKEZO NFRA inahujumu mfumo wa Stakabadhi Ghalani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa, yaani NFRA ni Taasisi iliyoanzishwa mahsusi kuhakikisha kuna kuwepo na Hifadhi ya Mazao ya Chakula muda wote Nchini.

Hununua mazao ya Chakula, kuyahifadhi, kuyachakata, kuweka kwenye Vifungashio na Hatimaye kuuza ndani na nje ya Nchi.

Mazao ya Chakula yanajulikana kama vile mahindi, maharage, mchele, karanga, mazao ya mafuta kama Alizeti n.k.

Kama Wakala wa Mazao ya Chakula tungetegemea wajikite kwenye mazao hayo japo tunajua changamoto zao za kuchelewesha malipo kwa wakulima mara kwa mara na kuna maeneo huwa inachukua hadi mwaka kulipa wakati ni Taasisi ambayo huuza mazao hayo kwa faida ndani na nje ya Nchi.

Jambo la kushangaza ni kwa hivi Karibuni NFRA kuacha jukumu lake la kuanzishwa kwake kwa kushughulika na mazao ya chakula na sasa wamejiingiza kushughulika na Mazao ya Kimkakati ya Biashara haswa kwa kuanza na zao la Mbaazi.

Katika msimu tulio nao sasa wa zao la mbaazi kupitia mfumo wa Stakabadhi Ghalani NFRA nao wamejiingiza kama wanunuzi.

Wameshinda minada katika Wilaya kadhaa, Mpwapwa, Kondoa, Chemba, Kilosa, Morogoro DC, Singida na zingine nyingi.

Sasa ni takribani wiki moja tangu washinde minada na hawajafanya malipo kwa Vyama vya Ushirika ili waweze kuwalipa wakulima pesa zao.

Ikumbukwe kuwa wafanyabiashara wengine ambao wamekuwa wakishinda minada hii huwa wanahakikisha kuwa malipo kwa wakulima yanafanyika ndani ya masaa 48, sasa ni zaidi ya wiki toka NFRA ijiingize kwenye mazao haya ya biashara na kushinda minada, kutolipa na kutengeneza taharuki.

Tunakumbuka Mhe. Rasi Samia amekuwa akitaka mazao yote ya kimkakati yaingie kwenye mfumo ili mosi wakulima wapate nguvu ya pamoja ya soko na kuuza mazao yao kwa bei nzuri na kwa vipimo sahihi vilivyothibitishwa na wakala wa vipimo wa Taifa (WMA). Na zaidi kuweza kuletea nchi fedha za kigeni kwani bidhaa hizo ni Maalum haswa kwa soko la nje ya nchi - Export.

Kitendo cha NFRA kuingia katikati ya msimu na kuanza kujihusisha na haya Manunuzi bado wadau hatujaelewa maana yake. Ikumbukwe Wilaya hizi ni mpya kwenye mfumo na wananchi wameitikia wito wa Serikali kuleta mazao yao katika mfumo wa Stakabadhi Ghalani.

Kuna watu wengi ndani na nje ya Serikali ambao hawaupendi huu mfumo sababu wamekuwa wakifaidika na mfumo holela wa mauzo unaowanyonya na kuwakandamiza wakulima.

Je tuamini huenda watu hao katika kuhujumu mfumo huu na kumhujumu Rais wetu na Serikali yake wameamua kutumia Taasisi hii kununua mazao kwa kuwashinda wanunuzi wengine kwa bei na kutolipa ili kutengeneza taharuki na kuwafanya wakulima wakose Imani na mfumo ili waendelee kulanguliwa?


Inakuwaje NFRA waibukie katikati wakati mfumo umeanza na unaendelea vizuri na kutengeneza uharibifu?


Tunaomba Serikali iichunguze NFRA na watendaji wake kwani liko wazi kuna jambo linapikwa kuichonganisha Serikali na Wakulima.
 
NFRA ichunguzwe. Naona malalamiko dhidi yake ni mengi sana huku.
 
Aya yako ya pili si dhani kama wanafanya. Kuna hawa CPB nadhani ndiyo wanachakata.

Hoja yako bado ni ya msingi sana. Sijui kwa nini tunashindwa wakati mazao yote haya yanasoko.
Mtaji sio shida, uongozi wa hizi taasis naamini ndiyo changamoto.
 
Back
Top Bottom