View attachment 2105366
Habari ya mtandaoni kwasasa ni watu kupita na magari, bajaji, pikipiki, bodaboda katika daraja jipya la Tanzanite.
Wapo wenye kuisifu Serikali ya Mama, Wengine wanamuenzi Magu, wengine wanalaumu kuwa kwanini lisingejengwa Jangwani n.k
Mimi binafsi nimeshangazwa na mkinzano wa jina na uwakilishi wa daraja. Jina Tanzanite lakini nembo iliyowekwa Mwenge. Zilongwa mbali zitendwa mbali...
View attachment 2105368
Hii ni tafsiri kuwa jina lilikuja baada ya project kuanza au hakukuwa na mawasiliano kati ya msanifu na watoa kazi (Serikali)
Hiki ni kihoja, au nasema uongo ndugu zangu? Imenishangaza KWERI KWERI