whiteskunk
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 3,904
- 9,342
Ngoja niisome zaidi maana hata mimi nikila vyakula vya ngano tumbo linajaa gesi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chipole huku Songea.Kijiji gani?
Kwa hiyo nani wa kulaumiwa?Si ngano tu, mimea kibao ina "sumu."
Sasa wewe unachanganya unga wa mahindi na maji usipate udumavu kweli?Mbona mnatuchanyanya?ugali unaleta udumavu wa akili ngano nayo ni hatari kwa afya.
Kwa kifupi ndio kilikuwa chakula kikuu Mashariki ya Kati tangu na tangu mpaka sasa. Yesu na wale washikaji zake 12 walifikia kipindi walikula hadi masuke ya ngano yakiwa shambaniYesu mwenyewe alikula ngano
Kwani mpaka awepo wa kulaumiwa?Kwa hiyo nani wa kulaumiwa?
Hiyo siyo sababu. Yesu angezaliwa China angekula wali.Ngano ni chakula cha kale zaidi kimetumiwa maelfu ya miaka bila shida yoyote ile, Ngano na maziwa husababisha binadamu kuwa na akili nyingi za kushangaza, bali ulaji wa mihogo huondosha akili,fanya tafiti.
Hata yesu alikula mkate wa ngano
Mfanyakazi wa Azam au Mo ndo anaweza kuandika vitisho hivi.Ngano ni nafaka hatari sana na watz wengi hatufahamu. Tofauti na nafaka zingine kama mahindi, ulezi, mtama na mchele, ngano ina aina fulani ya protin inayoitwa Gluten. Protin hii ndiyo hufanya ngano ikikandwa iwe kama banzoka wakati ukikanda unga wa mahindi hauwi namna ile.
Sasa hii protin inaweza kusababisha mzio(allergy/autoimmune reaction) ya hatari sana. Kifupi inaweza sababisha mwili ujishambulie. Maeneo yanayoathirika zaidi ni utumbo mdogo. Hili linaweza sababisha kuharisha bila kukoma, tumbo kujaa gesi, udumavu na afya dhaifu.
Pia inaweza athiri ngozi na mtu kutoka mapele ya kuwasha kama mwenye ugonjwa mkali wa ngozi.
Pia inaweza sababisha matatizo kwenye ubongo na kusababisha mtu atembee kama aliyelewa.
Inasemwa kuwa matatizo haya hutokea hadi kwa asilimia 2 ya watu wote.
Ni vyema tukatumia mikate ya mahindi, ulezi nk. Ngano ni hatari sana.
Ngano ni nafaka hatari sana na watz wengi hatufahamu. Tofauti na nafaka zingine kama mahindi, ulezi, mtama na mchele, ngano ina aina fulani ya protin inayoitwa Gluten. Protin hii ndiyo hufanya ngano ikikandwa iwe kama banzoka wakati ukikanda unga wa mahindi hauwi namna ile.
Sasa hii protin inaweza kusababisha mzio(allergy/autoimmune reaction) ya hatari sana. Kifupi inaweza sababisha mwili ujishambulie. Maeneo yanayoathirika zaidi ni utumbo mdogo. Hili linaweza sababisha kuharisha bila kukoma, tumbo kujaa gesi, udumavu na afya dhaifu.
Pia inaweza athiri ngozi na mtu kutoka mapele ya kuwasha kama mwenye ugonjwa mkali wa ngozi.
Pia inaweza sababisha matatizo kwenye ubongo na kusababisha mtu atembee kama aliyelewa.
Inasemwa kuwa matatizo haya hutokea hadi kwa asilimia 2 ya watu wote.
Ni vyema tukatumia mikate ya mahindi, ulezi nk. Ngano ni hatari sana.
Ndiyo maana nikaweka hapo kuwa ni kama 2% ya watu ndiyo husumbuliwa na Gluten.Nadhani hapa kuna haja ya ku-moderate contents. Kuna watu wana allergy na protini aina ya gluten, ambayo hupatikana kwenye ngano.
Hivyo, tuwe makini tunapotumia vyakula vitokanavyo na ngano.
Ukitumia na unapata tatizo lolote, pata ushauri wa kiafya au achana na vitu husika.
Ndiyo maana nikaweka hapo kuwa ni kama 2% ya watu ndiyo husumbuliwa na Gluten.
Maana hata kuna ambao hawagusi, sembe, nyama, mchele N. K.Hizo effects ni kwa baadhi ya watu.
Nani kasema kuwa kila mtu anaathirika? Watz tuna tatizo kubwa la kuelewa mambo yaliyoandikwa.Mnaokoteza habari mitandaoni, bila kuzisoma vizuri kisha mnakimbilia kuja kuanzisha nyuzi zenye taarifa zisizo sahihi. Acha nikurekebishe.
Si kila mtu ana allergy na gluten, kwa hiyo ngano haiwezi kuwa hatari kwa kila mtu. Itakuwa hatari tu kama mwili wa mtumiaji utakuwa na mzio na component/compound angalau moja iliyopo ndani ya ngano au kitu kingine chochote, mfano sabuni, manukato, n.k.
Sehemu kubwa ya vyakula tunavyokula ni more of a cultural than nutritional requirement, Ngano ni mojawapo.Asbh usinywe soup na chapati? Andazi na chai?
Daily viazi/ mihogo?