Ngassa aamua kuoa

Ngassa aamua kuoa

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,947
Reaction score
4,470
Winga machachali wa club ya Dar Young African almaaruufu kama Yanga Mrisho Ngassa ameamua kusogeza jiko. Ngasa amemwoa Latifa shamla shamla za mnuso huo zilifanyika Dar es salaam maeneo ya Tabata.
Wengi katika mnuso huo walikuwa wanadai dogo kaoa akiwa na umri mdogo mno sijui wadau mnasemaje kwa hilo.

1.JPG
Ngasa anaonyesha ufundi wa malavi davi kwa Latifa

2.JPG
huyu ndo Latifa mwenyewe ustadhi Ngasa kashikilia my wife wake.

3.JPG
Sheikh,Maustadhi na wageni waalikwa wakimpongeza Ngasa.
 
hahahah dogo lazima atasaidiwa kumega na wazoefu!
 
Masanilo usione wivu,najua wivu huna lakini roho itakuuma hapo tunaisubili yako na ya Bellie.
 
Hongera zake huyo Ngassa na maiwaifu wake..

Fidel, mdogo ana miaka mingapi?
 
hongera zako mrisho!tunaomba usipungukiwe na kiwango chako cha soka KISA MWANAMKE.maanake kule nako nguvu inatumika sana!jaribu kubalance,professional yako inahitajika zaidi

DOGO ANA 21
 
yeah huyu naskia anaenda na 20 sasa hivi kitu kama hicho.
Unaona ni umri right kuoa?

Tusiusemee moyo kila mtu na mipango yake maishani, kama kajikamilisha na amekuwa tayari kuoa sawa. Ila kwa mwanamke kuolewa ana 20 years siyo kitu cha kushangaza.

Hongera zake!..
 
hongera zako mrisho!tunaomba usipungukiwe na kiwango chako cha soka KISA MWANAMKE.maanake kule nako nguvu inatumika sana!jaribu kubalance,professional yako inahitajika zaidi

DOGO ANA 21

Huo umri anakuwa kweli amekomaa kijana?Na kuwa na maamuzi ndani ya ndoa?
Ok mi nahofia hicho hicho kwa maana jamaa atakuwa na usongo wa kukamua tunakuja tunashangaa kiwango kinashuka...inabidi aweke ratiba ya kujiexpress lasivyo tutashangaaa anaacha soka akiwa na 25yrs
 
Masanilo usione wivu,najua wivu huna lakini roho itakuuma hapo tunaisubili yako na ya Bellie.

Oyaah! sisi tumekuwa pamoja for six or more yrs...twajuana sasa dogo huyu mmmhh siangekuwa naye kama boy friend na na girl kwanza akipima upepo!?
 
Oyaah! sisi tumekuwa pamoja for six or more yrs...twajuana sasa dogo huyu mmmhh siangekuwa naye kama boy friend na na girl kwanza akipima upepo!?

Yawezekana huyo mtoto ni wa Sheikh sasa alikuwa anashindwa kujiexpress free ndo maana akaamua kuchukua jumla jumla ale kiuhuru.
Lakini nilisikia huyu dogo ana mtoto sijui kazaa na huyu Latifa?
 
Yawezekana huyo mtoto ni wa Sheikh sasa alikuwa anashindwa kujiexpress free ndo maana akaamua kuchukua jumla jumla ale kiuhuru.
Lakini nilisikia huyu dogo ana mtoto sijui kazaa na huyu Latifa?

Naweza shawika dogo amekarabati umri kama Masha amezaliwa 1966 lakini anajifanya kazaliwa 1970....Ngasa Mrisho huenda ni kijeba wa zaidi ya 25 miaka....unamkumbuka mzee wa kiminyio hahah Madaraka Selemani tokea miaka ya early 1980 alikuwa anaupiga huko Songea na Maji maji lakini kila siku wanasema ana miaka 42...yule nadhani yuko early 50s...
 
Inawezekana maana wachezaji wengi huwa wanadanganya umri
 
Dogo naona anajioverwork tu, labda! mi naona hivyo maana haya mambo hayatakiwi upelekwe na hisia tu inabidi utulie, inawezekana dogo anafanyia kazi mawazo ya zola ya kuja kujenga mwili maana nilisikia kaambie aje ajenge kwanza mwili, mwili hauji hivi hivi lazima awepo mtu wa kuutunza.
 
Vijiposho tu vya wiki mbili London kwenye majaribio- ameoa! Akisajiliwa, I doubt kama hataongeza mke wa pili! Hongera kaka, effect ya 'kukipiga' daily utaisikia tu kwenye magoti na mgongo!
 
Vijiposho tu vya wiki mbili London kwenye majaribio- ameoa! Akisajiliwa, I doubt kama hataongeza mke wa pili! Hongera kaka, effect ya 'kukipiga' daily utaisikia tu kwenye magoti na mgongo!

Kana Ka Nsungu, umejuaje kwamba kuoa katika kipindi hiki hakukuwa kwenye ratiba yake way before safari ya "Vijiposho tu vya wiki mbili London"?

Halafu kizazi cha leo watu wanaanza hicho ulichokiita "kukipiga daily" na wachumba zao way before ndoa, hivyo huna hakika kwamba Ngassa ndio atazidisha kitendo hicho baada ya kuoa. Isitoshe, ni wachezaji wangapi wana wake ndani na wanacheza mpira bila hizo effect za magoti na mgongo kutokana na tendo la ndoa? Nilitegemea ujue better manake una run thread za mipira humu, kumbe duu, hazikusaidii.
 
Kawaida yetu waislamu, tukipata hela tunaongeza mke sasa nadhani huu ni mwanzo tu kwa ustaadh huyu, ni mtazamo wangu tu, kama alikuwa na plans za kuoa- mimi na wewe hatujui!
Its a simple logic, kama unalala nayo daily, frequency ya 'kukipiga' itaongezeka, tena kama ndoa yenyewe ni changa?
 
Harusi za kiislam nzuri sana, yani ukiwa na alfu sabini tu ya kununulia ubwabwa ushaimailiza.
Mwenzenu natafuta milioni tano kwanza ndo nianze kuchangisha michango.
 
Mambo ya wikiendi mmeyapeleka kusiko kabisa..yaani ndoa ya mshkaji ndo mmeifanya stori ya wekendi? Masela sio fresh..
 
U-celebrity sio kihivyo. Yaani hapa naona mnasema chochote tu, mnavurumisha kila linalokuja kichwani badala ya kumtakia kheri kijana kwa kuweka kitu ndani. Yani mwelekeo wenu ni ki zeutamu ivi..hamtaki hamtaki ivi..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom