Ngassa alikataa dili la bilioni 1.6 El Merreikh

kwa akili ya Ngasa hata leo ahitajike canada hawezi kwenda jamaa ni bwege sana ana amini kuichezea yanga akiwa ba dhiki ni bora na uzalendo mkubwa kuliko kuchuma pesa

ila kikubwa jamaa ni mfano wa watanzania wengi tulivyo waoga kutafuta fursa nje ya miji/mikoa/nchi yetu.

hapa namlaumu tu ila hata mimi nilisha lengeshewa dili kusoma nje ya nchi (afrika hapa hapa (Algeria) ila kwa uoga wa ile nchi kuwa ya kidini nikaogopa. aliye enda sa iv ana cheo kikubwa nimebaki ku like picha zake fb.
 
Nakumbuka hiyo ya Marekani alicheza dhidi ya Man United

Huko Ulaya alienda West Ham naskia aliambiwa akaongeze lishe alikua dhaifu mno
 
Nakumbuka hiyo ya Marekani alicheza dhidi ya Man United

Huko Ulaya alienda West Ham naskia aliambiwa akaongeze lishe alikua dhaifu mno
Hilo la lishe na mimi nimeliona.

Kuna siku nimetoka zangu Unyamwezini nimekuja likizo Tanzania.

Sasa nimetoka zangu Mwanza nimetua airport Dar, nikakutana na wachezaji wa mpira wa miguu wanashuka kwenye ndege.

Sasa nishazoea kuona wachezaji wa Marekani wana miili mikubwa. Nikasema hawa wachezaji mbona miili yao midogo hivi? Hawa inawezekana ni wanafunzi wa shule ya sekondari au chuo. Labda wapo katika michezo yao ya UMISETA wameamua kupanda ndege. Nikasema tumeendelea siku hizi.

Nikajiuliza. Lakini inawezekana kibongobongo timu ya shule ikapanda ndege kwenda kwenye michezo?

Nikaambiwa hao ni wachezaji wa Yanga.

Hapo hapo nikaelewa sababu moja kubwa tunashindwa katika soka kimataifa.

Wachezaji wana lishe dhaifu.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alifichwa hotelini kupewa yule mwanamusic wa kike Snura ajiburudishe nae...wakati kama angekubali kuchukua hilo deal leo wangekuwa wanampapatikia mpaka leo..
Leo hii hao bongo movie hamna hata anayempapatikia kabakia kulialia kwenye mitandao.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndiyo ya Boban akiwa Sweden na Kapombe Ufaransa. Tena hawa walikuwa tayari wapo huko. Sasa wakaumiss ugali na bangi.
 
Anaipenda sana yanga na hakufikiria maisha yake ya kesho,
pengine hakujua kama mpira ni biashara na sio mapenzi kwa club,
Hau pengine ni uzwazwa na kutojiamini,
Jinga kabisa huyu kijana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.5 bln,jamaa kaongezea chumvi tu,el merreikh hawana hela kwa mchezaji wa kibongo,kwa mujibu wa huyo mwandishi el merreikh baada ya kushindwa kumpata ngasa ikabidi wamchukue ndiku,ndiku kwa sasa yuko azam hapo anasugua benchi,angefanya kutafuta muda akamuulize kama kule sudan alilipwa pesa hiyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilitokea kwa Sekilojo Chambua. Yeye mwenyewe anasema alipokuwa Yanga yeye na Nonda Shabani Papii walitakiwa na klabu ya Moroka swallows ya bondeni lkn Yanga walikataa na anasema Yanga iliwaahidi donge nono. Anasema tabia ya sisi wabongo wengi kutokuwa na passport na kubweteka tukifika simba na Yanga anavijutia Sana. Nonda shabani alikuwa na passport yake akakwea pipa akitoroka pale jangwani na hatimaye kupata mkataba na timu hiyo ya South Africa. Nonda hatimaye akawa Star Ulaya.
 
habari hii niliifuatilia sana kipindi hicho nipo vimbweta vya coet napiga rb....... machozi yalinitoka sn nilipokua nasoma hizi habari........


edo kumwembe na shaff dauda walipiga sn kelele facebook kuhusu upuuzi huu wa ngasa......


maisha kwakweli ni funzo kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…