Ngoja nijaribu kutunga jinsi ya kuwa bilionea kwa hii 500

Ngoja nijaribu kutunga jinsi ya kuwa bilionea kwa hii 500

Hapo umenunua tikiti nakuiuza saa hiyohiyo hujapinga mahesabu ya kuharibika,hujala,hujavaa,hujaweka vocha,yaani kirahisi hivyo duu mkuu tusidanganyane kiasi hicho ila simaanishi haifai lakin sio kwa urahisi ka ulivyotiririka ww
 
huyo atakuwa bado yupo kwa wazazi wake au ndo ndo kapo udom mwaka wa kwanza, [emoji23]
Chuoni hata kama unakula boom kuna mtu mwenye mawazo haya kweli, hii ni akili za f1 unawaza usome ufike chuo umalize uajiriwe uoe au uolewe uwe na magari na nyumba lakin ukitinga f4 unaanza kuona aliyeenda veta anaafadhila
 
Mtoa post uwe unaweka uzi ukiwa hujala,ukishiba unaandika tu,,,eti nunua tikiti 500 kwenye gari?nani atakuuzia tikiti moja tu kwa 500,?hata shamba tu yaweza kuwa ngumu kupata,,ebu zima hiyo luninga kazurule huko maana unamaliza tu umeme
 
ongezea hapo kuwa unakula kwa baba yako, anakununulia nguo, unalala kwake we kazi ni kuuza tikiti tyuu majukumu mengine ya mzee baba na ma lma au uwe umeolewa mahitaji yote unapata ,.

shenzi sana wewe[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Niliwahi jaribu kufanya Biashara ya Saa aisee nilikuwa nikiuza saa tu Hela naipigaa yani hadi nakuja kumaliza saa zote sina hata miaa...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23]Bishara noma sanaa
 
Hata sikufanaanishi Ila haya majaribio labda wewe unayaweza. Maana Mi hata sijaelewa
Majaribio kwa kitu ambayo unaona kabisa hata haiwezekani si mtihani huo. 😀😀 hivyo umetoka kapa. 😀😀
 
Majaribio kwa kitu ambayo unaona kabisa hata haiwezekani si mtihani huo. [emoji3][emoji3] hivyo umetoka kapa. [emoji3][emoji3]
Hahahha kumbe haiwezekani hiyo analysis alitoa?? Mi nimependa tu huko mwisho nilipoiona hiyo 41 Mil..Kwingine kapa kwakwel
 
Hahahha kumbe haiwezekani hiyo analysis alitoa?? Mi nimependa tu huko mwisho nilipoiona hiyo 41 Mil..Kwingine kapa kwakwel
Haiwezekani ndio. Mi mwenyewe ilinishawishi aisee mpaka nikajisemea siku zote pesa kuiandika ni rahisi mnoo. 😀
 
Haiwezekani ndio. Mi mwenyewe ilinishawishi aisee mpaka nikajisemea siku zote pesa kuiandika ni rahisi mnoo. [emoji3]
Au labda kuna sehemu tunakwama ngoja aje atupe darasa bwana.. Uwe makini mi nitajifunza kupitia kwako.. [emoji4]
 
Au labda kuna sehemu tunakwama ngoja aje atupe darasa bwana.. Uwe makini mi nitajifunza kupitia kwako.. [emoji4]
Kameshakimbia hata sikaoni. Yaani kameacha ujumbe halafu kenyewe kamekimbia. 😀😀 mie mzito kuelewa nakuachia wewe hii ya umakini halafu ndio unifundishage na mie ili na sie tupatemo hayo mahela. 😀😀
 
Kameshakimbia hata sikaoni. Yaani kameacha ujumbe halafu kenyewe kamekimbia. [emoji3][emoji3] mie mzito kuelewa nakuachia wewe hii ya umakini halafu ndio unifundishage na mie ili na sie tupatemo hayo mahela. [emoji3][emoji3]
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]haya tutajuaa
 
Ngoja nijaribu kutunga jinsi ya kuwa bilionea kwa hii 500.
.
Nunua tikiti kwenye lori la jumla 500, uza 1500 mpaka 2000 ila nitacheza na 1500. Nunua matikiti mawili 1000 na uuze 1500 jumla 3000. Ile 500 ya usumbufu tu. Chukua matunda mchanganyiko ya 2500 Kwenye maeneo ya jumla kumbuka utapata kwa bei rahisi alafu uza utapata 5000 mpaka 7500 ila nacheza na 5000. Ukifanya vile vile inakuja 10,000 alafu 20,000 alafu 40,000 alafu 80,000 alafu 160,000.
.
Chukua 100,000 anzisha station ya matunda mtaani kwenu na lengo iwe kukishi mahitaji madogo. Ndani ya wiki ilutakuwa na 300,000. Anza kuongeza viungo vya kupikia na mboga za majani. Utavuta 500,000 ndani ya wiki mbili. .
Wakati haya yanaendelea jaribu kufungua account bank, iweke fixed kama mwaka tu, kufungua account siku hizi hata bure. Weka 5,000 kila siku (usipuuzie) kuna sim banking kwahiyo unaweza hata weka kwa mpesa. Sasa tukifanya hujabadilika inamaana unaingiza 500,000 kwa wiki mbili kwenye duka lako la matunda na mboga na pia ndani ya mwaka utakuwa na 1,825,000 kwenye account yako. .
Nunua pikipiki 1,500,000 ajiri ndugu yako ambaye unamuamini hana kazi muambie akuletee mahesabu ya 70,000 kila wiki alafu ndani ya mwaka utamuuzia kwa 700,000 pikipiki inakuwa yake (investing mind). Mwisho wa mwaka unachukua 4,060,000. Mpaka sasa tumetumia miaka miwili najua ni mingi ila nenda sawa na mimi. Nunua gari used 5,000,000 (Unayo kwasababu una biashara kubwa na nimeacha kuiongelea lakini inakuwa ngoja niirudie sasa). Kwenye duka lako fanya kama mini supermarket, kuna matunda na vitu vingine vya madukani vya kula n.k. Kwa mwezi unaingiza 1,500,000 kwahiyo kwa mwaka hauna chini ya at least 10,000,000. Weka na ile 4M una 14M weka na 1.8 ya mwaka huu wa pili una 15.8 approx 16M. .
Narudi sasa chukua gari used 2 za 6M kila moja(nimebadilisha, sio 5 tena, sijasahau). Sasa una gari mbili na 4M. Chukua pikipiki 2 pia unabaki na 1M. Zile gari weka Uber dereva akuletee 30,000 kwa siku kila gari basi utakuwa na 21,900,000 mwisho wa mwaka. Pikipiki fanya kama ya mwanza kwa hizi mbili utakuwa na 8,120,000, dukani utakuwa na 10,000,000 na bank utakuwa na 1,800,000, basi jumla ni 41,820,000.
.
Au nunua bando nitukane, ni wewe tu [emoji5]
Usijua ni kwamba una hiyo 500 ,na mahitaji yako ya msingi ni 2000.
 
Wewe ghalama kwako ni zero na unakula hewa na kulala porini na maji ya kunywa na kuoga unachota mtoni.

Pia muda unakufuata mpaka matikiti yako yaishe ndio mshare usogeee.

Yakikosa wateja hayaozi pia hata mwezi!

Rudia tena kukokotoa weka percent ya upotevu na ghalama ili kuwa na uhalisia kidogo.

Nashukuru hujakimbilia KUBET!
 
Hata biashara ya bodaboda pia huijui, huwezi kumpata dereva boya akakubali akuletee 70k kwa wiki, baada ya mwaka eti umuuzie laki 7.

Huwa baada ya mwaka inakuwa yake na hakupi hata sh kumi.
 
Back
Top Bottom