Ngoja nikwambie sasa, sisi wahuni wa miaka ya 90 na tulivyo sasa

Nashukuru sana
 
Wanaume wa dar ukiwa mwizi au kibaka basi ndio mhuni .. njooni mbeya mjifunze...
 
Watu wa dar huwa wananifurahisha sana..kujisifia ujinga tu,ooh sisi ndio wahuni wa mjini afu mfukoni chenga..
 
Oy uwanja wa Ugimbi bdo upo masta.?
Ni ile bar pale ndani uwanjani tulikuwa tunacheza disco toto back then bado ipo..?
hahahahaha aiseee kitambo mnooo sijafikaa
daaaaaaah nakumbuka enzi za skukuu hapoo disco toto
 
Hawa mababu wanaolawiti wajukuu zao nao wamajifunzia siku hizi mkuu au hawa vigogo tunaosikia fununu zao kuwa ndio wanawaweka mashoga au wanatunza vijana wa mjini nao wamaezaliwa 1990's Mkuu. Mengine ni mambo yanayokuzwa na mtandao tu maana zamani mtu anaweza fiwa mwanza na yeye yupo dar lakini hadi apate taarifa za msiba si ajabu watu washaanza hata kusahau kama washazika

Haya ya watu kuwa na miili ambayo si kama ya zamani ni kutokana na life style na hata mababu zetu walituambia wazazi wetu ni laini laini na hawajui maisha, kwa sasa ni zamu yenu kujisifia na na zamu ya wengine itafika tu maana teknolojia inavyozidi kukua ndio life style inabadilika
 
mkuu kwa hali ilivyo, sidhani kama baada ya miaka 200 kuna kijana yoyote atakuwa na nguvu ya kuponda chochote. watakuwa hooooi!!!
 
Huyu Golikipa Omari alikuwa anakaa maeneo ya Jirani na Kwa Marehemu Mshuza?
 
Enzi hizo hakuna police post ilikuwa ukizingua unawekwa zone (CCM) na pale CCM kimanga kulikuwa na mbabe mmoja anaitwa Genda kwenye 80's-91 na Twiga namkumbuka golikipa Katuba.
Mimi naikumbuka Mandela Bar (tabata Kimanga) ya yule mzee mwanajeshi, ndiko nilikuwa nashindia muda wangu wote wa ziada. Hiyo timu alikuwepo dogo mmoja mrefu mweusi ana mwili wa kispoti na mpira alikuwa anaujua balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…