Ngoja nikwambie sasa, sisi wahuni wa miaka ya 90 na tulivyo sasa


Umenikumbusha mbali sana nimesoma mabibo enzi za mwaikenda hayo yote maeneo yangu mimi nimezaliwa na kukulia mitaa ya external karibu na UFI
 
Mimi naikumbuka Mandela Bar (tabata Kimanga) ya yule mzee mwanajeshi, ndiko nilikuwa nashindia muda wangu wote wa ziada. Hiyo timu alikuwepo dogo mmoja mrefu mweusi ana mwili wa kispoti na mpira alikuwa anaujua balaa.
Mandela Bar. ..naifahamu ya zamani sana hiyo Bar.tulikuwa tunafika kule kupata maji...Kimanga napafahamu.
 
Nashindwa changia naona kama nilikuwa mwanaume wa 80's! Kweli kikongwe..
 
Sifahamu alipokuwa anakaa. Unamfahamu Mama Mshuza? Alifariki lini?
Kuna mshuza alipata ajali ya gari mandela road mwaka sikumbuki ila ni kabla ya 1994. Alikiwa maarufu sana. Kwa kumbukumbu zangu alifariki pamoja na mkewe maana walikuwa wote kwenye gari ndogo iliyoingia nyuma tela la semi.
 
Kuna mshuza alipata ajali ya gari mandela road mwaka sikumbuki ila ni kabla ya 1994. Alikiwa maarufu sana. Kwa kumbukumbu zangu alifariki pamoja na mkewe maana walikuwa wote kwenye gari ndogo iliyoingia nyuma tela la semi.
Mamshuza alikuwa hai nadhani mpaka late 1990s kama sikosei. Sijui wenyeji waliokuwepo watatukumbusha.
 
[emoji23][emoji23]muwamba ngoma huvutia kwake mkuu.
Hata ungelikuwa dhaifu usingelisema hapa.
 
Huyo Santana alijiingiza kwenye siasa akawa upande wa Ccm, alipokeaga kichapo kutoka kwa mlinzi wa Prof. Lipumba asee.
 
sinza star na abajalo ,wakikutana ngoma inakuwa si ya kitoto mitaa ya sinza,

lazima watu walale saa moja usiku
Siaba yupo wapi now?
Pia kulikua na Timu inaitwa TP Africa....weka tuwekeee, Lunyamila na Mohamedi Hussein mmachinga ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…