Ngoma chapambire moto: Internet ya Tigo post itaweza kumudu huu mziki mpya wa Airtel?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
TIGO POST PAID:
  • 15 GB kwa 15,000
  • 35 GB kwa 35,000
  • 48 GB kwa 40,000
  • 72 GB kwa 60,000
  • 120 GB kwa 100,000

Gharama ya usajili utalipia kiasi kinacholingana na bei ya bando unalotaka kuungwa

Bando utalochagua utakuwa unaungwa kila tarehe 1 ya mwezi

Kila mwezi inabidi ulipie bando unaloungwa, usipolipa lain inafungwa na unadaiwa deni.


AIRTEL SME:
A. Vifurushi vya sme bila kununua router ya airtel
  • 22 GB kwa 20,000
  • 35 GB kwa 30,000
  • 60 GB kwa 50,000
B. Vifurushi vya sme ukinunua router ya airtel inayouzwa elf 50
  • 22 GB kwa 20,000
  • 35 GB kwa 30,000
  • 65 GB kwa 50,000
  • 100 GB kwa 75,000
  • 200 GB kwa 100,000/=
Hakuna gharama za usajili, wanachohitaji ni Tin Number na leseni ya biashara hata iwe ya kibanda.

huna wajibu wa kulipia kila mwezi, mambo yakitaiti unaweza nunua kifurushi cha chini au kusubiri mfuko ukae sawa

unachagua kifurushi cha kununua, mwezi huu unaweza nunua cha elf 20 mwezi ujao cha elf 50


CONCLUSION

Mimi tigo post paid nilijiunga mwaka jana kabla hawajabadili vifurushi, huwa naungwa gb 80 kwa elf 60 kila mwezi. hapa nilipo napima mzani kwasababu kifurushi changu nacho kipo fresh si haba lakini kama ningekuwa nalipia vifurushi hivi vya sasa ningehamia airtel fasta tu.
 
Naweza tumia laini yangu ya Tigo!?
 
Airtel wanatufaa.
Mimi tigo post paid nilijiunga mwaka jana kabla ya mabadiliko ya kuleta hizi bei mpya, huwa naungwa gb 80 kwa elf 60 kila mwezi. hapa nilipo napima mzani kwasababu kifurushi changu nacho kipo fresh si haba lakini kama ningekuwa nalipia vifurushi hivi vya sasa ningehamia airtel fasta tu.
 
Boss. Last time nilienda kununua router ya tigo nikapewa na zile 40GB ila nilipoomba niungwe na hii huduma wakasema siku hizi ni kwaajili ya makampuni tu.

Lazima niwe na kampuni iliosajiliwa sijui blah blah.

Kwahiyo GB40 zilivoisha router ipo tu na laini yao sijawahi weka ata jero.

Je, imerudi hii naweza jiunga au Bora niende Airtel naona hawana mambo mengi.
 
Ni kweli kuna mabadiliko yalifanyika, bei zilipanda mno ila kwa sasa wamefanya tena mabadiliko tena, vifurushi vina nafuu na huenda hata usajili umelegezwa, jaribu kwenda tena.

Ila ikishindikana kuna wadau hata humu ndani wanaviunga na kuna magroup kabisa ya whatsapp
 
Tatizo la airtel ni speed tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…