Ng'ombe wa maziwa au bajaj used ipi option nzuri? Changamoto zake

Optimists

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2021
Posts
467
Reaction score
1,358
Nipo kwenye mchakato wa kugawa pesa katika miradi midogo midogo, nione namna ya kufikia uchumi wa Kati Kwa makusanyo ya tsh 100,000/= Kwa siku na kuzidi, hii miradi ambayo nataka mtaji wake usizidi million 4-5 pia inipatie only 20,000/= per day

Nimechakata mawazo mengi nikaona nikimbie uchumia wa Frame Kwa Sasa maana uko TRA,OSHA,NEMC N.k hawachekeshi katika utawala huu, nikavunja idea nyingi nikabaki na idea mbili ya kuanza nao.

Bajaj 3.5M -4M kikubwa board iwe nzuri namba C/D engine mbeleni unaweza kubadilishwa sio mbaya, ukimpa kijana 20,000/ Kwa siku anakupatia sio mkataba, changamoto sizijui sijawahi kufanya.

Ng'ombe wa maziwa nipe naendelea kufanya research, but uko pia naona uhakika wa kupata 20,000/= Kwa siku, mwenye any idea kuhusu hizi investment mbili tofauti? Changamoto zake na advantage zake ni ipi?
 
Bajaj ni depreciating asset, thamani yake inashuka kila mwaka , kuna mambo pia kama ajali, wizi yanayo weza kukuongezea gharama zisizo za msingi.

Ng'ombe, yeye ana anazaa, kifupi ataongeza thamani ya mtaji wako siyo kwa kutegemea uuzaji wa maziwa tu.
 
Nimeichukua hii. But Kwa huo mtaji nitaweza kupata ng'ombe? Au niendelee kufanya research?
 
Nenda kwa ngombe w maziwa kama sehemu uliopo majani na pumba zinapatikana kwa wingi. Na pia cjui imani yako ungemaliza na nguruwe mbegu za kisasa. Usinge juta. Ni vzr kufanya vitu vinavyo fanana pia anasaidia uangalizi.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Bro kama una eneo fuga ngombe wa maziwa. Ngombe 1 unaweza ukammudu wewe mwenyeweg hakikisha una nyasi kwanza kwanza afu chakula cha dukani kiwepo kama nyongeza. Nunua mabeseni kadhaa nyasi unakata unaweka kwene mabeseni hapo home hata ukienda misele yako watamuekea chakula na sio uajiri kijana wa kazi kwa ngombe mmoja no. Ajiri kijana after ngombe amezaa ndio amhudumie atoe maziwa na hayo hayo maziwa ndo mshahara wake. Maji yasikose mda wote utakuja nishukuru baadae. Achana na bajaj kwanza. Ufugaji wa ngombe wa maziwa inahitaji uvumilivu tu na matunda yake utayaona.
 
Hii nimeichukua, nafanya research zaidi Kwa waliofanikiwa nilipo majani sio issue sana
 
acha utafiti anza wewe kama wewe bro unakuta watu wawili na wote ni madereva wa magari tena aina moja lakini mwingne anakuwa na mafanikio kumzidi mwenzake kama majani sio shda fuga ngombe nasema fuga mnyama bajaj utaipata kwahao ngombe tena mpya. Nimeenda.
 
Bajaj ni depreciating asset, thamani yake inashuka kila mwaka , kuna mambo pia kama ajali, wizi yanayo weza kukuongezea gharama zisizo za msingi.

Ng'ombe, yeye ana anazaa, kifupi ataongeza thamani ya mtaji wako siyo kwa kutegemea uuzaji wa maziwa tu.
Kumbuka na yeye anaumwa na anakufa.
 
Back
Top Bottom