Ng’ombe wa Ndani (Zero Grazing) vs Wakuchunga

Ng’ombe wa Ndani (Zero Grazing) vs Wakuchunga

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2009
Posts
1,174
Reaction score
835
Wanajamvi nimekuwa mfugaji wa ng'ombe wa maziwa wa kuchunga kwa miaka kama 10. Hata hivyo nimepata changamoto zake hasa upande wa magonjwa na kesi za majirani kila wakati. Pia wezi wanathaminisha kiurahisi na wakaniibia ng'ombe kama 7. Kwa sasa sina hata 1 kutokana na matukio hayo.

Kufuga siwezi kuacha kwani hapa nilipo biashara ya maziwa ni uhakika na ilifikia wakati napata lita 50 zinanipa elfu 60 kila siku. Nikitoa gharama za uendeshaji nabaki kama 1.5 kwa mwezi.

Nafukiria nianze kufuga wa ndani kama 5 hivi ambapo nitazalisha hadi lita 80 kwa siku ila bado sijaua management regime yake hivyo naomba kujua yafuatayo:

1. Nitahitaji vijana wangapi.
2. Banda liwe na sifa gani?
3. Vitendea kazi vya aina gani
4. Mengineyo kadiri mtakavyoona.

Nawatakia Jumapili njema.
 
Unamaanisha wa kisasa hawa wanafaida zaidi japo pia ni ghalama kwa ng'ombe tano utahitaji vijana 2 hiyo picha ni mfano tu
20200406_183222.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu magonjwa hayakwepeki kikubwa ni chanjo na matibabu, pakuzingatia usafi ni kuzingatia ili kuondo magonjwa hayo.
Idadi ya ngombe kubwa au ndogo si uhakika wa maziwa mengi, kikubwa mbegu nzuri kuanzia majike mpaka madume/dume.
Matunzo mazuri kuanzia lishe,chanjo na matibabu.
idadi ya wahudumu ni wawili, wanatosha kabisa ila wawe nanauelewa wa mifugo la sivyo watakupasua kichwa na ng'ombe utawaona ka adhabu kwako.
banda liwe la kawaida ila liwe na ukubwa wa kuwatosha ng'ombe wako katika namna ya kula na kulala pasipo kusongamana, ila liwe limezibwa juu lote au nusu pindi jua litakapokuwa kali waende kivulin/upande uloezekwa hivyo hivyo nyakati za mvua, pia ukumbuke sehemu ya kukamulia, uwe na sehemu ya kuweka ndama la sivyo utalia kila uchwao maana ndama watakuhujumu katika maziwa.
vitendea kazi ni ka hivyo ulivyokuwa watumia kwa kwa hao ng'ombe wa nje yana kamba ni muhimu hata ka ng'ombe wanakaa free bandani, vyombo vya chakula kwa ng'ombe. vyombo vya usafi. n.k.
Kila la heri mkuu
 
Usifananishe ng'ombe wa zero grazing na mambo ya kiajabu ajabu
Ufugaji unaongaliwa maji, chanjo, Malisho na usimamizi ni zaidi ya ajira
N.B picha haiendani na mada
 

Attachments

  • VID-20191015-WA0097.mp4
    3.9 MB
mchango wako kwa mtoa mada ni upi mkuu? Achana na porojo hizo nenda mojakwamoja kutoa majibu kwa maswali yake
Usifananishe ng'ombe wa zero grazing na mambo ya kiajabu ajabu
Ufugaji unaongaliwa maji, chanjo, Malisho na usimamizi ni zaidi ya ajira
N.B picha haiendani na mada
 
Back
Top Bottom