Nairobifly
Member
- May 3, 2012
- 75
- 26
Umaarifu wa Hifadhi hiyo ni kwa sababu ya mfumo wa maisha Jumuishi (Wanyamapori na Jamii). Ukiondoa jamii pale, maana yake umeiondolea sifa Hifadhi yake ya multiple Land na umaarufu. Haitakuwa tofauti na Hifadhi ya Manyara na Tarangire. Haitakuwa tena moja ya maajabu ya Dunia.
Niliwahi kuona mkataba wao na serikali ya mkoloni muingereza wakati wanapisha kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti, hivyo kisheria ni haki yao kuwepo pale. Babu zao kukubali kuachia Serengeti ni jambo kubwa walilofanya, hii ndiyo Hifadhi Bora Afrika kwa sasa.
Tanzania tunajivunia kuwa na maeneo mengi ya Hifadhi lakini ukijaribu kuangalia yalikuwa maeneo ya wafugaji zaidi wakiwa wamasai, kwa maandiki hiyo wanastahili kuheshimiwa na kudhaminiwa. Nina Imani ingekuwa makabila mengine hakika tusingekuwa na wanyama/hifadhi hao/hizo wengine tunakula mpaka konokono.
Shida nyingine huenda wahifadhi wa mle hawana mipango mizuri ya kuendeleza mfumo ule wa matumizi Jumuishi kama sheria inavyotaka, wakae na jamii wakubaliane watafute majawabu ya changamoto kwa pamoja, lakini pia ushirikishwaji na elimu uimarishwe. Serikali itazame hili huenda na wahifadhi wanashindwa majukumu yao ikiwezekana ibadilishwe mfumo wa usimamizi wa eneo hilo.