Ngorongoro hatarini kupoteza uhai na umaarufu wake kutokana na kukithiri kwa shughuli za binadamu

Umaarifu wa Hifadhi hiyo ni kwa sababu ya mfumo wa maisha Jumuishi (Wanyamapori na Jamii). Ukiondoa jamii pale, maana yake umeiondolea sifa Hifadhi yake ya multiple Land na umaarufu. Haitakuwa tofauti na Hifadhi ya Manyara na Tarangire. Haitakuwa tena moja ya maajabu ya Dunia.

Niliwahi kuona mkataba wao na serikali ya mkoloni muingereza wakati wanapisha kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti, hivyo kisheria ni haki yao kuwepo pale. Babu zao kukubali kuachia Serengeti ni jambo kubwa walilofanya, hii ndiyo Hifadhi Bora Afrika kwa sasa.

Tanzania tunajivunia kuwa na maeneo mengi ya Hifadhi lakini ukijaribu kuangalia yalikuwa maeneo ya wafugaji zaidi wakiwa wamasai, kwa maandiki hiyo wanastahili kuheshimiwa na kudhaminiwa. Nina Imani ingekuwa makabila mengine hakika tusingekuwa na wanyama/hifadhi hao/hizo wengine tunakula mpaka konokono.

Shida nyingine huenda wahifadhi wa mle hawana mipango mizuri ya kuendeleza mfumo ule wa matumizi Jumuishi kama sheria inavyotaka, wakae na jamii wakubaliane watafute majawabu ya changamoto kwa pamoja, lakini pia ushirikishwaji na elimu uimarishwe. Serikali itazame hili huenda na wahifadhi wanashindwa majukumu yao ikiwezekana ibadilishwe mfumo wa usimamizi wa eneo hilo.
 
Asante kwa kuongea ukweli. Kuna watu wamelipwa posho kuongea hovyo bila kuangalia uhalisia na namna ya kutatua changamoto.
Wale pesa lkn waongee ukweli.
Ukiwaondoa wamasai pale hakuna NCAA na utakuwa tu umewaonea watu ambao hawadhuru wanyama.
Ingekuwa makabla yao, si wangeshamaliza kila kitu?
Hakuna ulazima wa kulazimisha NCA kuwa kama Mikumi au Serengeti. NCA ibaki na huo upekee wake.
 
Wanaopaharibu Ngorongoro ni hawa wawekezaji hasa wa kihindi wanaojenga mahoteli na pia hawa Ant-porchers yaani askari wa wanyama pori.
 
Basi eneo lipangwe
Ijulikane tu mipaka ya kuishi Masai ni wapi over

Pori libaki intact
Kuchunga sio ishu sn
 
Endelea kuota... Kwanza umesomea nini wewe?
 
Iwafikie wagagagigikoko
 
Soon konde boy ataenda kupiga show hii si sawaa panakua kama mji sasa si mbuga
 
Kuna kitu kinaitwa Afforestation

Halafu kingine kinaitwa Deforestation

Hilo liko kwenye maendeleo ya Ma zingira lakini kwenye sekta ya MISITU.

HALAFU Kuna OVERSTOCKING

HALAFU TENA KUNA DE-STOKING.

Overstoking iko kwenye sekta ya Mifugo.

Suala la kufuga wanyama wengi zaidi ya inavyoshauriwa katika eneo stahiki-ni OVERSTOKING.

Na madhara yake ni makubwa sana.

Hilo haliko Ngorongoro peke yake.


Liko Nchi Nzima.

Hatuna data.

Hatuna Mfumo.

Hatuwezi kufikiri tu kwamba Mifugo ni mingi kumbe pengine hata siyo ya kwetu.

Au pengine haitoshi.

Hatua ya kwanza tuwatambue Wafugaji.

Tutambue uwezo wao.

Tukae chini tuelimishane.

Kisha tupange pamoja.

Kama kuna shida ya Sheria-Tutafsiri sheria.


Hiyo ndo namna Bora ya kudeal na tatizo.
 
Umefikiria sana, nchi hii tukipata watu wachache kama wewe tutasonga mbele. Kwa hii umebarikiwa.
 
hii nchi ilinifaa mie na tata nyarusare ti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…