Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Wamasai ni watu! Wamasai ni watanzania, wamasai ni waafrika na wamasai ni ndugu zetu! Nilipokuwa mdogo miaka ya 80 nilipata bahati kubwa ya kuzunguka na mzee haswa nyakati za likizo tukitembelea maeneo mbali, nilipata uzoefu wa kuona Maisha ya watanzania wenzangu, na hii ilinifanya kujifunza lugha kadhaa za makabila na makundi mbalimbali, nilitumia muda mchache sana kuzishika lugha mbalimbali, Kisukuma, Kijita, Kikara, Kikerewe, Kiikizu, Kihehe, Kinyaki pamoja na lugha nyingine ambazo kwa ukubwa wake ninazisikia na kuelewa sarufi yake.
Kitu ninachomshukuru sana Marehemu Baba ni kunifundisha kuipenda nchi yangu, alikuwa akiniambia kuwa Tanganyika ni jina mama la ardhi yangu, ingawa nilivyokuwa nikienda shule nilifundishwa kuwa nchi yangu ni Tanzania sio Tanganyika. Alinifundisha pia jambo la kuonesha upendo kwa watu, mtu wa kabila tofauti akihitaji msaada basi nisitazame kabila lake bali nitazame ubinadamu wake na kuweka mbele utu. Maskani yangu niliyolelewa ni Mwanza maeneo ya Pasiansi ila hii haitoshi kunizuia kumsikiliza na kumpa msaada mtu aliyetoka Ilundamatwe huko Iringa.
Malezi haya kutoka kwa Marehemu Baba yalinifanya kumtazama jirani yangu kama sehemu ya msingi sana kwenye asili ya Afrika na Dunia kwa ujumla. Kujitazama bora zaidi kiasi kwamba ukamvua utu wake mwezako ni jambo ambalo linatosha kukupatia jina la ADUI. Haipunguzi chochote kumtendea vibaya binadamu mwezako kwa kigezo ambacho hakina mashiko hata dakika moja, tengeneza mazingira ya haki pasipo kumuumiza mtu yoyote yule.
Na katika hilo tumepata kuwa na mifumo ya usimamiaji wa sheria na haki, Bunge na Mahakam ani sehemu ambazo wananchi ni kimbilio lao katika kupata suluhu ya mambo ambayo hayaendi vile inavyotakiwa. Ni muda sasa tumepata kusikia habari kuhusu ndugu zetu Wamasai katika suala lao la kuhamishwa kutoka Ngorongoro, ni ajabu ila hili ni jambo ambalo tumepata kuona serikali na viongozi wakilitolea majibu ambayo hakuna mwananchi mzalendo anawaelewa. Majibu mepesi sana tena yasio na ufafanuzi kindakindaki, binafsi nalitazama kama sio jambo sahihi kulifanya.

Rais Samia kwanza nafurahi sana kuona juhudi zako katika kuleta michoro ya namna Tanzania Bara itapata neema katika siku za mbeleni (HONGERA SANA) ila pasipo kuficha chochote sidhani kama washauri wako wanakupatia ushauri mzuri kuhusu baadhi ya michoro hii. Rais Samia sio mzaliwa wa Tanganyika maarufu kama Tanzania Bara, na sidhani kama washauri wako wanakupatia michoro kwa ajili ya Tanzania kwa ujumla. Hakuna suala ambalo utajiharibia jina kama suala hili la Wamasai.
Kuna mdau mmoja kwenye mtandao wa X aliwahi kusema kuwa “Nguvu inayotumika kwenye sherehe na matamasha ya Kizimkazi basi nusu ya jitihada hizo zingeokoa kaya nyingi sana za Ngorongoro, na kitu kibaya hakuna mtu ambaye ni mamluki kama mzawa wa Tanganyika kushindwa kuongea kuhusu watanganyika na kwenda kupiga debe kwenye shughuli za Kizimkazi. Sio kwa ubaya ila tusisubirie waje wapemba kuweka nguvu suala la kulinda ardhi yao Wamasai.
Tanzania tuna makabila zaidi ya 200 makabila ambayo yamesambaa kila kona, Kuna wasukuma wengi sana wapo Mbeya, kuna Wanyaturu wa kutosha wapo Lindi, kuna Wahaya wa kutosha wapo Dar es Salaam, ila pia kuna Wangoni wengi tu wapo Mwanza, hakuna siku utakutana na ugomvi wa Mhehe akizichapa na Mjaluo kisa Mhehe amepata kiwanja Utegi mkoani Mara, hakuna siku utapata kusikia kuwa kuna fujo Wahaya wamewafukuza Waluguru kutoka Kagera. Ila ni mara ngapi tunasikia matukio na kesi kadhaa za chuki kutoka kwa wakazi wa Tanzania Visiwani maarufu kama Zanzibar kwa watu waliotoka Tanzania Bara, chuki ambazo kiuhalisia hazina msingi wowote katika maendeleo.
Haya ni maoni yangu:
- Serikali imekuwa ikidai kuwa wamasai wanaharibu mazingira ndani ya Ngorongoro, ningetamani sana Waziri wa Maliasili pamoja na Waziri wa Mazingira watoke mbele wazungumzie kuhusu jambo hili kwa kutazama muktadha huu: (a) Je uharibifu wa mazingira umeonekana katika kipindi gani? Na kwa kiasi gani? (b) Je miaka ya nyuma Wamasai wameishi Ngorongoro je kuna athari zozote za kimazingira zilizoonekana? (c) na mwisho ni kuzungumza na wamasai na kupata maoni yao. Ni ngumu sana kwa Rais Samia kuweka amri ya wamasai wahamie Tanga Wakati hajawahi kuishi na wakazi wa Ngorongoro zaidi ya kulala kwenye hoteli ya kitalii ya nyota tano. Msiwaonee!
- TLS ambacho ni chama cha mawakili wa Tanganyika wakishirikiana na LHRC na asasi zingine za usaidizi wa kisheria zipeleke kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga hamisho la watanganyika wenzetu. Katika hilo tunahitaji umoja mkubwa sana kwani hapo tena Zanzibar haiusiki, hivyo ni sawa na kumshinikiza Mheshimiwa Mpango kumshauri Rais Samia kutengua jambo hilo mara moja. Hakuna faida hata moja ambayo serikali itaipata kwa kuwaondoa wamasai kwenye ardhi yao ya asili.
- Tume ya Uchaguzi fanyeni kazi na majukumu yenu kwa kutazama na kuzingatia sheria na kanuni na sio maagizo ya viongozi waliopo juu. Uwepo wenu umethibishwa kisheria na sio na kiongozi, nafahamu kuwa tume sio huru hata kidogo na wengi tunatambua hilo sio jambo jipya kwa watanganyika wengi. Ila viongozi ndani ya tume ya uchaguzi mpo katika nafasi hizo kwa mujibu wa sheria hivyo fanyeni kazi kwa kuangalia sheria. Hakuna jambo la ajabu na lenye jeuri kubwa kama kutokuweka kituo cha kuhakiki taarifa za wapiga kula kwa jamii ya wamasai, sio fair hata nusu. Katika uchaguzi wa 2020 kuna vijana waliokuwa na umri wa miaka 14, 15, 16 na 17 walishindwa kupiga kulak wa sababu mbalimbali kama vile kuwa na umri mdogo wa kupiga kula na wengine kukosa kadi za wapiga kura. Tume ya uchaguzi msifanye kazi ili mpate kuonekana na Rais Samia ili mbeleni mpate kupandishwa vyeo, mnawaumiza watanganyika wenzetu kwa sababu za kijinga. Ebu fikiria ZEC watoe orodha ya vituo na wasiweke sehemu ya kuhakiki wapiga kura waliopo Wete, je Rais Samia ataendelea kukaa kimya? Wote tuna haki sawa, wekeni vituo Ngorongoro watu wapate kujiandaa na uchaguzi.
- Mwisho kabsa, viongozi kuweni makini sana na mambo ambayo mnayatolea maagizo, tusije kuwabariki ndugu zetu wamasai kilemba cha Uyghur na kilichotokea Uchina huko Xinjiang mwaka 2014. Kinachoonekana kwa sasa ni kama serikali ya Rais Samia inataka kufuta kabsa utambulisho wa Wamasai, hakuna sababu ya msingi ya kuwaondoa kwenye makazi yao na kuwapeleka Tanga, ni sawa na kuwachukua Wamatengo na kuwahamishia Geita, mahala ambapo unakwenda kuanzisha utamaduni wao mpya kabsa, sio jambo zuri hata kidogo kuharibu historia ya jamii yoyote. Rais Samia usipokuwa mwangalifu utabeba hii dhambi ambayo unataka kuwafanyiwa Wamasai kama vile Uchina wanachokifanya kwa waislamu jamii ya Uyghur. Tunafahamu kuwa nguvu kubwa Rais umeiweka Kizimkazi ila kura za 2025 hazitoki Kizimkazi pekee, zinatoka Ikizu, Mji Mwema, Kilolo, Matembo, Kilimahewa, Miazini, Ibadakuli, Kibada na sehemu ambazo watanganyika wanakutazama na kusikia kila agizo ambalo unalitoa.
Kama Rais na wateule wako mtaruhusu ukatili huu basi wakazi wa Vitongoji vinavyozunguka Lamadi pamoja na Lukungu mkoani Simiyu nao mjiandae kuondoka mpelekwe Mtwara kwani wapo Karibu na hifadhi ya taifa ya Serengeti. Kina Dotto Magari na wenzako huko Kizimkazi sio kwenu, acheni kutumia nguvu nyingi kumpamba Rais Samia wakati kuna watu wanaporwa haki zao za msingi.