Ngorongoro sio sehemu ya makazi ya binadamu bali ni hifadhi ya wanyamapori

Ngorongoro sio sehemu ya makazi ya binadamu bali ni hifadhi ya wanyamapori

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2016
Posts
250
Reaction score
409
#NGORONGORO SIO SEHEMU YA MAKAZI YA BINADAMU BALI NI HIFADHI YA WANYAMA POLI Naa Joseph #Yona

Mwaka 1960 Ngorongoro Ilikuwa na Tembo zaidi ya 2000! Ila leo hii Tembo waliobaki Ngorongoro ni 30! Moja ya utajiri wa kipekee duniani ni kuwa na wanyama Mwitu kama hawa ambao sisi wabongo tunawachukulia poa sana!

Ila wana thamani kubwa katika ulimwengu huu! Dunia nzima kwa sasa inateigemea zaidi Tanzania kuhusu wanyama pori. Tanzania ndio wenye wanyama wengi tuliobaki duniani. Ila mbali na hilo wanyama wamekuwa wakiangamizwa kwa speed ya kutisha na sisi wenyewe Watanzania na sasa kuna wanyama ambao wapo kwenye Hatari ya kuangamia kabisa katika uso wa dunia.

Muhimu kuanza kuchukua hatua stahiki kuinusulu Hifadhi adimu Duniani kwa vivutio vya utalii.

MADAI YA WATU KUISHI HIFADHI YA NGORONGORO NA WANYAMA POLI KUWA NI KUVUTIA UTALII NI UJINGA NA UPUUZI

Hivi karibuni kumezuka mijadala mingi juu ya uwepo wa zaidi ya watu zaidi ya laki Moja kuishi hifadhi ya Ngorongoro kuwa ni njia Moja wapo ya KUVUTIA UTALII ni ujinga na upuuzi usio vumilika hata kidogo.

Tumeshudia Waandishi wa habari Maulid Kitenge na Oscar Oscar Mzee wa Kaliua wakiwa wanaripoti kutoka Hifadhi ya Ngorongoro na kueleza ualisia unaoendelea hapo Hifadhini kumejitokeza, kundi la wajinga flani kwa maslahi yao binafsi bila kuangalia hali ilivyo wameanza kampeni ya kuwashambulia waandishi hao, bali tuangalie uhalisia, taarifa ni kuwa kuna jamii ya watu wachache ni wanufaika na shida za watu walio wengi maskini, huko Ngorongoro Tuendako watoto wanakufa, hakuna barabara, hakuna huduma za kijamii nk ndo maana MECIRA tunasema hatua za haraka zichukuliwe kuondoa hali ya hatari zaidi baadaye na sasa.

Shida inayoonekana hapo ni wafugaji kuingilia hifadhi, kwa ajili ya malisho na Taifa linaweza kukosa watalii kwani watakuwa wanafika kwenye hifadhi badala ya kuona pundamilia, au Twiga wanakutana na Ng'ombe na Taifa kukosa mapato yatokanayo na utalii, lakini pia kizazi Cha Sasa kitaona mazingira rafiki kwa malisho ni kwenye hifadhi kwani kitaona hakuna katazo lolote kama wanahabari tunapaswa kuishauri serikali njia sahihi za kuepukana na hili tatizo, kazi iendelee.

Hakika mapendekezo ya Kitenge na Oscar* yanatakiwa kuchukuliwa haraka hatua za makusudi kwa ajili ya kuokoa kizazi ambacho kinaishi maisha hatarishi, na kuokoa hifadhi kuondokana na hatari ya kuwa jangwa.

#PazaSauti
#KataaMakaziYaWatuNgorongoro
IMG_20220207_125935_884.jpg
IMG_20220207_125935_834.jpg
 
Wakati Ngorongoro inaanzishwa kuwa hifadhi kulikuwepo na watu 8,500 hawakuwa wengi, na serikali ya kikoloni ikaamua NCA iwe na title maalum, yaani uchanganyaji wa hifadhi na watu na mifugo yao michache.

Ambacho hawachokikifahamu ni kuwa waafrika tuna mtindo wa kuhamia na kujenga popote pale bila ya kujali mazingira yanaharibika au la, mfano halisi katika nchi yetu karibu vyanzo vyote vya maji vimekauka! Sababu watu wamevamia na kujenga maeneo ya vyanzo vya maji vikiwemo chemichemi na vyanzo vya mito. Sijui waafrika akili zetu zipo wapi?

Wenzetu wa Ulaya na Amerika wamejali vyanzo vya maji na wameweka mazingira yao salama, sisi tunakata miti kwa kwenda mbele, serikali haijali wala wananchi hatujali....hatuangalii kesho.

Suala la Ngorongoro kwa sasa ni suala moto, Ngorongoro inaanza kuwa mji mkubwa na ule uoto wa asili na wanyama unapotea/wanapotea...KISA...Wanasiasa wanatafuta kura " at the expense of our wildlife"

Leo kuna watu zaidi ya laki moja kule Crater na idadi ya mifugo ya wamasai imepita idadi ya wanyama! Sasa watalii gani watakuja kuangalia mifugo? Watu wanauawa na wanyama, watoto wanaliwa na simba lakini bado binadamu hawaelewi, wanajazana ovyo humo ndani! Inachofanyika ni siasa tu.

Wakati wa Nyerere na conservator akiwa Solomon Ole Saibul, Ngorongoro ilipendeza, idadi ya Faru weusi ilikuwa kubwa na wanyama wengi huku idadi ya watu ikiwa wachache ambao hawakujenga "permanent structures" Ole Saibul alipokea Ngorongoro ikiwa bora kabisa kutoka kwa Mr. Foosbrooke.

Wanaokumbuka Nyerere Manifesto leo hii wakiona Ngorongoro ilivyo watatoka machozi, Nyerere alimaanisha alivyotoa hii manifesto"

Julius Nyerere and the Arusha Manifesto
"The conservation of wildlife and wild places calls for specialist knowledge, trained manpower and money and we look to other nations to cooperate in this important task - the success or failure of which not only affects the continent of Africa but the rest of the world as well."

Wanyama wanatakiwa walindwe na jukumu la kuwalinda ni letu sote, kama tutashindwa kuwalinda wanyama, sisi binadamu hatutakuwa na tofauti na wanyama. Sasa leo sisi binadamu tuna uwezo wa kuishi katika mazingira yoyote yale LAKINI tunayavamia maeneo ya wanyama, je hao wanyama wataenda wapi? Tuone aibu!

Siwalaumu watu pekee yao ila pamoja na mipango mibovu ya serikali. Uhifadhi unalipatia Taifa hili pesa nyingi sana za kigeni, je serikali inashindwa kuwapatia mahali pazuri penye huduma zote hao wamasai, wakaishi vizuri kuliko kukaa humo Crater?

Jibu ni kuwa wanaweza ila serikali zetu zote zilikuwa na tabia ya u-selfishness, wanachuma pesa lakini kuwapeleka hao wananchi mahali pazuri na kuwawekea huduma zote wanazohitaji ikiwamo kuwajengea malambo hawataki..hivyo wananchi wanashindwa na wanaogopa kuondoka hapo.

Ombi kwa mama Samia Suluhu Hassan, wahamishe hao wananchi kwenye maeneo mengine kama ya Longido, Loliondo, Serrat, Kiteto au hata Handeni na muwawekee huduma bora! Kwa kufanya hivyo hakuna atakayekataa kuhama hapo Crater.
 
Wakati Ngorongoro inaanzishwa kuwa hifadhi kulikuwepo na watu 8,500 hawakuwa wengi, na serikali ya kikoloni ikaamua NCA iwe na title maalum, yaani uchanganyaji wa hifadhi na watu na mifugo yao michache.
Ambacho hawachokikifahamu ni kuwa waafrika tuna mtindo wa kuhamia na kujenga popote pale bila ya kujali mazingira
Hivi watalii lazima waje Ngorongoro pekee? waende hata huko Serengeti
 
Ona sasa favour za serikali kwa wamasai hadi washajisahau wanajua wao ni haki yao kukaa pale
 
yaani jamii ya kifugaji ya wamasaai wamekuwa wakimbizi ndani ya nchi yao ya asilia ya Tanzania, kila sehem ndani ya nchi yao wanafukuzwa mara ohoo mmezidisha mifugo, ohoo mmevamia mabonde ya wakulima, ohoo, ohoooo…, na sasa mnawafukuza kwenye maeneo yao ya asili kama loliondo na ngorongoro, sasa waendee wapii?? waueni woote na muwa malizee sasa………..
 
Ngorongoro ni Urithi, Maasai wametafutiwa maeneo mengine na huduma zote za kijamii zimewekwa.

Ngorongoro lazima iwe salama.

1959 busara ilitumika lakini Hifadhi inaendelea kuwa hatarini.

Maasai wameanza ku practice ujangili.

Watoke ila wafidiwe pakubwa.
 
Mleta uzi ni vyema ukaijua sheria pamoja na mikataba.
 
Wewe una data zao?
Kwa vile unaniona hapa Jamiiforums ndiyo unafikiri watu wote tuliopo hapa hatujui, wengine bado hatujastaafu. Kimsingi Wamaasai waondoke hapo crater ili Ngorongoro isipoteze uoto wake wa asili. Wewe unajiita Babati, usiharibu jina zuri la mji huo wenye mvuto, Au ninyi ndiyo wale mnaoendelea kuvamia ziwa Babati, Kwakuchinja, mdori, Burunge hadi wanyama wanashindwa kupita kutoka Tarangire NP hadi Manyara NP, Ebu tulia wewe tulia tuachie wakongwe wa field hiyo tuongee.
 
Muhifadhi unatoa somo huku unatoa mipasho pia.
 
We utakuwa kati ya watu wapuuzi sn, acha kutumika na mafisadi
 
Yatakuja MaCHADEMA hapa kuropoka na kushuta.’ Hakuna siasa. Masai waondoke Ngorongoro haraka.
 
Hivi watalii lazima waje Ngorongoro pekee? waende hata huko Serengeti
Ngorongoro pakijaa hata huko Serengeti tutahamia tu....

Hii sio Tanzania pekee, Binadamu ni Virus wa Mazingira na ataendelea kuharibu mpaka pale mazingira yatakapoanza (yameshaanza ku-retaliate)

“When the last tree has been cut down, the last fish caught, the last river poisoned, only then will we realise that one cannot eat money,”
 
Tunatakiwa tuwe na hifadhi za ambazo zenye wanyama ambao ni artificial siyo hii ya kufuga wanyama ambao hata hawana faida, baada ya miaka 40 ijayo hakuna mtu atakuja kuangalia fisi, sijui nyumba toka Ulaya, kutakuwa na wanyama ambao ni robot wenye tabia kama za wanyamapori, lazima tubadilike tuachane na hawa wanyama asili tujikije kwenye artificial
 
Back
Top Bottom