NGO's zaomba kukutana na Rais Samia

NGO's zaomba kukutana na Rais Samia

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
NGO's zaomba kukutana na Rais Samia

Mashirikaka yasiyo ya kiserikali Kanda ya ziwa yameomba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MH. Samia Suluhu Hassan ili kueleza kero na changamoto zinazowakabili.

Miongoni mwa changamoto ambazo masharika hayo yameeleza ni zile zinazochangia kuzorotesha ufanisi na utendaji kazi zao za kila siku za kusaidia jamii inayowazunguka.

Ombi hilo limetolewa na mjumbe wa kamati ya kitaifa ya mpito inayoratibh uchaguzi wa mabaraza ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NACONGO) YASSIN ALLY jijini Mwanza wakati wa uchaguzi wa kupata mjumbe wa mkoa wa Mwanza.

Ally amesema kuwa mashirika hayo yana mambo mengi ya kuzungumza na Rais wa Tanzania kuhusu changamoto zinazowakabili ili kuleta ufumbuzi.

"Tumeona Rais (Samia Suluhu) anakutana na makundi mbalimbali hapa nchini na sisi kama mashirika yasiyo ya kiserikali tunaomba tukutane naye kwani tuna mengi ya kuongea nae.

"Rais amekutana na viongozi wa dini, amekutana na kundi la wanawake na vijana, hivyo hata sisi tunaomba tukutane nae kwani na sisi ni kundi muhimu kwenye Taifa hili,"amesema Yassin.

Katika hatua nyingine mjumbe huyo ambaye aliteuliwa mei 7 mwaka huu na Waziri wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dorothy Gwajima, ameendelea kuongoza zoezi la uchaguzi katika mikoa ya Kanda ya ziwa.

Miongoni mwa mikoa ambayo tayari amesimamia na kufanyika uchaguzi bila malalamiko ni Geita na Mwanza ambako ambako uchaguzi umepata wajumbe wa kitaifa kutoka mikoa yao.

Katika mkoa wa Geita amechaguliwa Paulina Majogoro, mjumbe wa Baraza la NACONGO Taifa, ambapo Mwanza amechaguliwa Revocutus Sono ambao watawakilisha mikoa yao.

Msajili msaidizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Mwanza NGOS, Isack Ndasa amewataka wajumbe hao ambao wanawakilisha mikoa yao kwenda kuchapa kazi.

Amesema wajumbe hao wanapaswa kuhakikisha wanaenda kuwakilisha mashirika yaliyopo kwenye mikoa yao vizuri ili kutimiza malengo yanayokusudiwa na mashirika hayo badala ya kutumia nafasi hizo kwa maslahi yao.

Kamati ya mpito ya watu 10 iliyochaguliwa na waziri wa afya, kuratibu uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini NACONGO katika ngazi ya wilaya na mkoa itafanya kazi hadi Julai 10 mwaka huu.
 
Umekuwa mchezo sasa kila kakikundi hawajui wanaweza kumwambia hata DC tu


USSR
 
Change is inevitable, resisting for the change you see the consequences"King Mswatti". Always time speaks for itself.
 
Back
Top Bottom