Ngozi nyeusi ni laana?

Ngozi nyeusi ni laana?

Prof. Minzi na wengine!

Sijui kama Waafrika kuna siku tuta endelea na kufanikiwa kama wenzetu wazungu, wahindi, wachina, waarabu, nk. We seem to be at the lowest thinking, intellectual and moral level. Kwa nini nasema hivyo?

Nimewekeza hela nyingi sana kununua mashamba Mkoa wa Rukwa wilaya ya Kalambo about 2,000 acres.

Nimeajiri na nalipa mishahara mizuri kila mwezi for the second year! Sijaweza hata kuvuna kuanza kurudisha hela nilizowekeza. Wanapata malazi na chakula bure nje ya misharaha yao kwenye kambi ambayo nimejenga nyumba kadhaa, nimewekeza matrekta ya kilimo na mwaka huu ilikuwa tulime 500 acres kwa kuanzia. mafuta wanatumiwa, fedha za matumizi madogo madogo wanatumiwa.

viongozi ni watu wazima wa elimu ya chuo kikuu nikifikiri natoa ajira kwa waafrika wenzangu. Wapo wafanyakazi kama 50 wote kila mwezi wana mishahara na kula na kulala bure kwani ni mbali na mjini.

İli kusimamia nilimweka mtoto wangu wa kiume asimamie baada ya masomo ya diploma, nikamwondoa baadaye aweze kupata exposure kwenye miradi mingine. Nilimweka mpaka mchungaji rafiki yangu wa siku nyingi awe anatupia jicho la pembeni kwenye kijiji cha jirani na namlipa allowance kwa mwezi ila sio mfanyakazi.

To my surprise, kumbe wamejenga syndicate kubwa mno kati yao viongozi na operators wa trekta na hasa baada ya kumtoa mtoto wangu kwenye kazi zingine nikimwachia uongozi kijana mwingine ambaye nilipewa na mpendwa kanisani graduate wa UDOM wa zaidi ya 5 years experience ambaye kwenye interview showed quite good command of leadership.

Kumbe kwa siri, wameanzisha vijishamba vyao wanalima kwa mafuta yangu ninayowatumia; wanalima mashamba ya wenyeji kwa hela SH. 70,000 kwa ekari na fedha wanagawana kwa siri; matrekta yangu yote mawili yameharibikia kwenye mashamba ya kulimia watu kupata hela, muda wa kulima shamba langu hawana, shamba langu nililopanga kulima 500 acres this year, Limelimwa only 50 acres na matrekta yasingeharibikia huko wangelima hekari zaidi ya 200, ambazo zimethibitishwa kulimwa; gari yangu ya shamba Canter imekatika chasis kumbe wanafanya biashara ya kubebea watu mazao, kokoto na mawe kwa kulipwa hela wanazo pocket kwa kugawana bila sisi kujua na walifanya siri kubwa.

Nilisukumwa kuomba na kufunga for 3 days last week na sasa nipo kwenye maombi ya wiki nzima ya kufunga nikizidi kuomba ustawi na mafanikio kwenye kazi za mikono yangu.

Kwenye migao yao ya fedha za siri mmoja inaelekea hakuridhika na utaratibu wa mgawanyo akiona anapunjwa, walipoona anasumbua wakamfitini na kumfukuza kazi.
Ndiye baadaye aliyeanika syndicate yote ambayo kumbe mpaka mchungaji wa pale niliyemwamini sana sana naye yumo!😭😭

Nikimuuliza mchungaji huyo, kulikoni yote haya yanayotokea na yeye akiwamo kuhusu, aliishia kuwa na kigugumizi na ameshindwa kabisa hata kujitetea amebaki kuomba samahani!!!!

Waafrika tunaenda wapi jamaniii!!!😭😭😭
Umaskini kweli utaondoka kwa kuwa na roho chafu na mbaya kiasi hiki kweli. Hivi kama sio wokovu nilionao, watu kama hao akipigwa risasi na mwekezaji mwingine kama mimi, tutamlaumu hawa wezi, walafi, watu wasio na soni wala huruma kama hawa kweli?

Nimejinyima miaka yangu yote mpaka uzeeni ili niweke urithi kwa vizazi vyangu, nijisikie nilipambana wajukuu waje kuanzia maisha bora zaidi ya yale tuliyoishi sisi, tunaishia kuwekeza kwa wezi vijana wasio na roho kiasi hiki.

Nimeshea hili ili kama taifa tujitafakari tunakwenda wapi kwa kizazi hiki tulichonacho. Hawa ndio tunaowatengeneza wawe viongozi wa kitaifa, nchi itaweza kusogea kwa mentality ya jinsi hii.

Binafsi nimeamua kutafuta ku-employ Indians or Chinese kuendesha miradi yangu, nimechoka na waswahili acha waendelee kuwa vibarua na watumwa milele na laana zao.

Waafrika tusiporudi kumtafuta na kumwinamia Mungu kwa dhamira ya dhati mioyoni mwetu, laana ya umaskini na utumwa itaendelea kututafuna milele mpaka mwisho wa dunia

Nawashuhudia nyote kwamba Maombi yanafunua hata yaliyo sirini yaliyojificha. Mungu anaangalia dhamira iliyo safi mbele zake na humwekea ulinzi mja wake, kwenye hili, binafsi nimemuona Mungu akitenda.

Glory be to God The Almighty! 🙏🏾🙏🏾

mrangi
Pole Mwekezaji Mzawa
Usikate tamaa,inwezekana katika ajira zako ulizotoa ulisahau Makundi Makuu Matatu.Kwa mtu anayetaka kufanya uwekezaji mkubwa asisahau kaujiri au kuweka Wafuatao
1.Extenal Auditors;Siku hizi kuna kampuni binafsi ambazo hutoa huduma za ukaguzi wa Hesabu na Raslimali watu,Kampuni hizi hutoa mwelekeo wa Shughuli unzofanya katika kipengele cha Going Concern(Principle of Accountinmg Term)Kwa kawaida hawa hutoa huduma kwa Malipo kidogo na wanatambulika kisheria
2.Business Consultancy hawa watakutengenezea Tools za Monitoring and Evaluation yaani watakupa nyenzo za kuwa unajipima na kujifanyia Tathmini kadri ya Mwezi,Nusu Mwaka hadi Miaka Mitano,kwa hili kama unaelekea Shimoni utajua mapemaaaaa
3.Solicitors:Watakutengenezea jinsi ya Kutengeneza Mikataba ya Wafanyakazi na Biashara wezeshi au Shiriki.Upande wa Wafanyakazi watapewa Terms ambazo wakienda kinyume Sheria itachukua mkomdo wake na si vinginevyo
KUMBUKA UKIENDA KISHERIA(BUSINESS LAW) Biashara ni mtu naili iende inatakiwa iendeshwe kisheria na sio kindugu.Ndo maana huwa inasajiriwa(Kupewa uhai) inapewa chakula yaani Financial & Human Resource na pia
k
 
Sijasoma yote ila kuna vitu nimenote;
1.Umeanzisha mradi mkubwa kwa mkupuo bila maandalizi thabiti, hapo kufeli ni kugusa.

2. Unamwamini vipi binadamu mwenzako kwa sababu za ajabu kabisa eti huyu mchungaji😄😄😄😄 dini is just a very big hoax.

3. Unapenda ubwenyenye hivi unawezaje ukawa unaspend pesa kiasi hicho wahenyeke wenzako ww upo mjini unakula bata hivi unadhani hata hao wazungu wanahuo ujinga ww ukae mbali huko usitapeliwe.

4.Mradi wowote ni hatua anza mradi wako katika small scale ujue mradi stick na mradi mmoja ukikua ndo uanzishe mwingine.

5.Unatumia sana maneno ya kutaka upewe huruma kuwa umeonewa, big NO wewe hujaonewe dunia imejaribu kukufunza the HARD WAY huwenda uliweza kufuata utaratibu wote wa kuanzisha kampuni ila ukaleta USWAHIBA( KUWALALIA) hao makabwela unaodai unawalipa wasio na ujuzi wowote wala vision towards huo mradi,no way out utapata faida.

6.Unarudia makosa ya kila siku kuamini mtu akifika chuo kikuu anakuwa EXTRA ORDINARY GENIUS😆😆😆 Lazima uangukie pua, hao wasomi wa vyuo vingi most walienda chuo kukua and infact unazungumzia vyuo hivi majalalani and the like hapo lazima upate matokeo mujarabu kabisa🤗

7.Acha ubwanyeynye hilo shamba lako halijafikia hatua ya kujiendesha,ingia ground vaa boot simamia mradi DO or DIE,,, Unless otherwise hii ni chai kufurahisha bongo zetu na ndoto za kumiliki ESTATE.
Are you grown person ?. Hivi MOE anaweza simamia miradi mwenyewe ? Huyo mtu tayari ana miradi mingine.
Lakini kwa nini husomi habari kwa umakini.
Hii ni habari sensitive sana kwa sisi watu weusi.
Amesema alimuweka mtoto wake kisha akampeleka kwenye miradi mingine .
Hao wahitimu wa chuo si ndio hao hao wapo bank. Mbona hawaondoki na mahela pale bank ! Je mkabulu yupo kila bank ya NMB.
Kwani angekuwepo angeendesha yeye hayo matrekta ?
Tabia ya watanzania ni mbaya tu, kampuni ya Dangote madereva wa malori wanayatumia malori kuiba root ndogo ndogo, je Dangote anaweza simamia lori zaidi ya 200 . Profesa kakosea ndio ila watanzania ni MUFLISI.
Hakuna kitakacho ongoka kwa usimamizi wa watanzania wengi. Ni watu wa HOVYO sana.
 
Aisee ........ Hujaona wamiliki wa makampuni wanakuwa na watu wao,wako kama misukule ila ni waajiriwa na wanapata mshahara mdogo na kwa tabu? Boss kashawafunga wale, chochote kinachofanyika lazima wamueleze. Hata ukiwapa deal lazima waseme kwa boss. Boss anaweza kukaa hata mwaka bila kufika ofisini na Kila kitu shwari. Kampuni haziendeshwi kawaida boss wangu.
 
Story za kujitungia vijiweni kwa lengo moja tu, la kuwadhihaki na kuwatukana Waafrika kwa sababu za rangi ya ngozi yao.

================

Si ajabu mama zenu wanakata viuono kila wakisikia midundo ya ngoma za watu wenye Ngozi nyeusi. Itoshe Labda mimba za mama zenu wote , ambao wana laana, mimba zilitunga wakisikiliza nyimbo za "wenye ngozi nyeusi"
😂😂😂😂😂😂

JamiiForums is now a Home of Bigoted, Racist Twaats.
Huenda hayajawahi kukukuta haya
 
Solution yake inashangaza.

Kumrudia Mungu?!
Mungu gani sasa? Mbona hao wachina na Indians wenye ufanisi na anaotaka kuwaajiri hawamjui huyo Mungu anaemsemea? Nafikiri yeye ndio ana matatizo.

Anatakiwa ajue solution ya changamoto hizi siyo kumrudia Mungu.

Pathetic!
Inasikitisha wewe kuitwa binadamu!

Kwa nini? Kwa sababu wewe mwenyewe hujijui ni alama ya mambo gani!

Huwezi kuendelea au kupata maendeleo kama humjui Mungu.

Angalia unaosema hawamjui Mungu. Kiwango chao cha uadilifu kikoje? Na je, uwezo wao wa kufikiri na kufanya uchunguzi ukoje?

Wewe (Mwafrika) unafanya uchunguzi gani? Kwa nini uadilifu wa mwafrika ni zero? Ni kitu gani kingine kipya ambacho Mwafrika ameweza kuzalisha?
 
Professa kafeli sana. Tatizo halipo kwa wafanyakazi bali kwa yeye profesa.
Mie ndugu yangu mwenyewe ananihujumu sembuse mtu baki . Nilimleta ndugu yangu shambani shamba likaungua na barafu likaungua na moto wakati resource za kuzuia zipo. Ukiondoka nae anaondoka kwenda mashamba ya jirani akafanye vibarua.
Nilimuanzishia mradi wa kuku wa kumsaidia pale shambani akawa anauza kuku na kuzichinja mpaka zikaisha kisha akaanza kununua za kwake nazo zikamshinda.
Niliamua kumrudisha nyumbani, it was just a waste of time and resources.
Niichojifunza ni kuwa kila kitu unatakiwa usimamie mwenyewe japo haiwezekani.
Kwa hio sisi pesa zetu ni za kiwango cha kusimamia wenyewe zikizidi ukahitaji wafanyakaxi basi umetafuta wa kukusaidia kuzila.
Usipoandaa watu kiakili na kimwili, kiroho na kimaadili; mtu asipotambua kwa akili lipi ni jambo jema na lipi ni jambo baya, upi ni ukweli na upi ni uongo, hakuna maendeleo hapo. Ni umasikini tu.

Waafrika hawaandai watu; hawafundishi watoto wao kujua ukweli. Wako kama wanyama wanazaa na kuacha hapo!

Lakini wanataka matokeo, wanatamani maendeleo ila hawajui maendeleo ni utaratubu na mpango wa kiakili.
 
Inasikitisha wewe kuitwa binadamu!

Kwa nini? Kwa sababu wewe mwenyewe hujijui ni alama ya mambo gani!

Huwezi kuendelea au kupata maendeleo kama humjui Mungu.

Angalia unaosema hawamjui Mungu. Kiwango chao cha uadilifu kikoje? Na je, uwezo wao wa kufikiri na kufanya uchunguzi ukoje?

Wewe (Mwafrika) unafanya uchunguzi gani? Kwa nini uadilifu wa mwafrika ni zero? Ni kitu gani kingine kipya ambacho Mwafrika ameweza kuzalisha?
Duuuu!

Nimerudia mara nyingi bado sijaelewa unaongelea nini hapa?

1)Labda unamaanisha kuwa mtu hawezi kuwa muadilifu bila kumjua Mungu!? (hata bado sielewi unaposema kumjua unamaanisha nini!)

2)Labda kuna sehemu unamaanisha kuwa waafrika sio waadilifu.

Kama 1) na 2) hapo juu ni sahihi, basi ni hoja mbili zenye muelekeo mmoja, na hivyo zinaweza kujibiwa kwa pamoja.

Ninachokiona kwako ni lack of exposure, inawezekana kabisa uelewa wako juu ya ulimwengu na wanadamu tamaduuni zao ni finyu.

Unaoanisha kumjua Mungu na uadilifu, ili hali anaezungumziwa kukosa uadilifu ni mchungaji!

This is ironic!

Unakili mwenyewe kuwa waafrika siyo waadilifu, je, unafahamu kuwa waafrika ni jamii (zinazomjua) huyo Mungu kuliko jamii nyingi?

Unafahamu kwa mfano, kwamba Japan ni nchi yenye watu waadilifu na wastaarabu zaidi?

Nikushangaze sasa, Japan hawajawahi kumjua huyo Mungu, hakuna makanisa na misikiti kule.kule.
 
Nianze na hili la exposure.

Sijui kama hiyo unayoita exposure imekusaidia kuelewa mambo!

Namaanisha huenda ukawa na exposure lakini usiweza kuchanganua na kuelewa mambo.

Kwa mfano, kwa nini wajapani ni waadilifu na wastaarabu?

Au swali la msingi: "uadilifu" ni nini? Na mtu anawezaje kuwa mwadilifu?

Kuhusu kwamba Japan hawamjui Mungu na kwamba hakuna Kanisa. Huo ni uongo.

Takiribani asilimia 0.4 ambayo ni sawa na watu zaidi ya laki tano (500,000) ya idadi ya watu wa Japani ni wakatoliki.

Hiki ulichoandika kinaonyesha kuna mambo mawili ambayo hujayajua. La kwanza: dini maana yake ni nini? Na la pili: Mungu maana yake ni nini?

Kumjua Mungu sio kuhudhuria Kanisani au msikitini. Kuwa padre au mchungaji au shehe hakumanishi ndio kumjua Mungu; au kwamba ni mwadilifu. Mapadre, mashehe au wachungaji wanatoka wapi? Huko wanakotoka kuna uadilifu?

Ndugu yangu.

Sisemi waafrika wote, lakini zaidi ya asilimia 98 ya waafrika "HAWAMJUI MUNGU".

Kwa nini? Angalia mambo wanayofanya! Je, hayo mambo ni yenye akili?

Watu ambao hawawezi kutambua kwa akili jambo jema na baya, uongo na ukweli, ambao hawawezi kutafuta ukweli wa mambo unawezaje kusema wanamjua Mungu?
 
Hapo nimekuelewa.

Nilidhani kumjua Mungu ni kuwa mfuasi wa imani za kidini kama vile ukristo na uislamu,

Kumbe kumjua Mungu unamaanisha kutambua jambo baya na jema, ukweli na uongo!

Kwa definition hiyo, nakubaliana na wewe kwamba ili kupata maendeleo au kuwa muadilifu, inatakiwa''kumjua Mungu''
 
Usipoandaa watu kiakili na kimwili, kiroho na kimaadili; mtu asipotambua kwa akili lipi ni jambo jema na lipi ni jambo baya, upi ni ukweli na upi ni uongo, hakuna maendeleo hapo. Ni umasikini tu.

Waafrika hawaandai watu; hawafundishi watoto wao kujua ukweli. Wako kama wanyama wanazaa na kuacha hapo!

Lakini wanataka matokeo, wanatamani maendeleo ila hawajui maendeleo ni utaratubu na mpango wa kiakili.
Hakuna mzazi asiefundisha mtoto maadili mema. Shule zote zinafundisha maadili mema. Msikitini na kanisani napo wanafundisha maadili mema. Kwa hio ni tabia tu za watu kukiuka maadili.
 
Hakuna mzazi asiefundisha mtoto maadili mema. Shule zote zinafundisha maadili mema. Msikitini na kanisani napo wanafundisha maadili mema. Kwa hio ni tabia tu za watu kukiuka maadili.
Tabia ni nini?

Na kwa nini watu wanakiuka maadili?
 
Waafrika hasa hawa watnzania ni takataka kamwe usiwape kazi,inatakiwa uendeshe huo mradi kama kampuni ,kuwe na human resources Manager ili mambo yaende katika ipasavyo
 
Back
Top Bottom