Ngozi ya korodani imechubuka baada ya kunywa dawa za mafua

Ngozi ya korodani imechubuka baada ya kunywa dawa za mafua

leyb

Senior Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
111
Reaction score
64
Ni kama siku nne zimepita, ilikuwa jumanne this week usiku nilikunywa dawa za mafua za chenga chenga sijui trof zileee. Asubuhi niliamka ngozi inayofunika korodani imechubuka na niligundua baada ya kwenda bafuni kuoga. Sikujali nikajua labda boxer imenichubua.

Nimekaa siku 3 panazidi kuuma na mapaja yanakuwa na viupele vinawasha nikivikuna. Niliamua kwenda kufanya check up hospitali nikapimwa magonjwa ya zinaa nimeambiwa non reactive. Nikapewa ampiclox na panadol wakasema labda kuna mdudu kanitambaa.

Leo siku ya nne hali haibadiliki, nimekuja hapa kuomba msaada wa mawazo nifanyeje ili nipate uvumbuzi wa jambo hili.

Ahsanteni.
 
Pole mkuu nakushauri mtafute daktari bingwa Wa magonjwa ya fungus. Usitishwe huo sio ukimwi ni hali ya kawaida.
 
Mkuu kwanza pole

Hiyo sio effect ya dawa hiyo ni hali imetokea na sababu kubwa huenda ni fungus ndio zinaleta hiyo ishu cha kuzingatia halikisha kila baada ya kuoga unajifuta vizuri ili kukausha maji sehem za siri

2.Hakikisha haushei nguo au ndoo za kuogea na watu wengi maana wengine sio wasafi ndoo hiyo hiyo inadekia na kufulia hapo hapo ,kuogea pia

So jaribu kuwa na ndoo yako mwenyewe safi ya kuogea na halikisha unavaa nguo kavu

Hiyo hali itapotea automatically cz mimi mwenyewe ishawahi kunitokea ngozi ya pumbu kubabula last week lakini baada ya kufwata hayo mashart yenyewe imepona
 
Mkuu kabla ya kula hio dawa unaweza kutuelezea ulikutana na mwanamke au una share taulo na mtu?. Ulikula chakula cha aina gani ambacho hujawahi kula kabla? Ulishika kitu baadae uligusa map*mbu yako? Hebu tuelezee kwanza kuna kitu gani kipya ulitumia zaidi ya hio dawa. Jee hio dawa ndio mara yako ya kwanza kutumia. Juu ya huyo jamaa anaesema umepata ukimwi tambua kama anatania tu usichukulie serious.
 
Mkuu kwanza pole

Hiyo sio effect ya dawa hiyo ni hali imetokea na sababu kubwa huenda ni fungus ndio zinaleta hiyo ishu cha kuzingatia halikisha kila baada ya kuoga unajifuta vizuri ili kukausha maji sehem za siri

2.Hakikisha haushei nguo au ndoo za kuogea na watu wengi maana wengine sio wasafi ndoo hiyo hiyo inadekia na kufulia hapo hapo ,kuogea pia

So jaribu kuwa na ndoo yako mwenyewe safi ya kuogea na halikisha unavaa nguo kavu

Hiyo hali itapotea automatically cz mimi mwenyewe ishawahi kunitokea ngozi ya pumbu kubabula last week lakini baada ya kufwata hayo mashart yenyewe imepona
naongezea...badili boxer mara kwa mara...ukioga asubuh vaa boxer safi...jion ukirud ukioga usiirudie vaa ingine...na taulo unalojifutia sio unakaa nalo mwezi ndo unafua...
 
naongezea...badili boxer mara kwa mara...ukioga asubuh vaa boxer safi...jion ukirud ukioga usiirudie vaa ingine...na taulo unalojifutia sio unakaa nalo mwezi ndo unafua...
Ahsanteni sana nitafuata maelekezo then nitaleta mrejesho.Mungu awabariki sana
 
Kanunue Candistat cream, siwezi kukutajia tatizo hapa
 
naongezea...badili boxer mara kwa mara...ukioga asubuh vaa boxer safi...jion ukirud ukioga usiirudie vaa ingine...na taulo unalojifutia sio unakaa nalo mwezi ndo unafua...

Kwenye taulo hapo inakata miezi 6 halijafuliwa.
 
Back
Top Bottom