bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,334
- 2,463
Mimi ni kijana nayependa sana miguu yangu, Haya mapenzi yameanza zamani wakati nasoma shule ya msingi kipindi nilipoanza kuoga mwenyewe. Nishagombana sana na ndugu zangu wa damu na mama yangu mzazi pale ilipofika zamu yangu kuingia bafuni eti kisa natumia muda mwingi.
Mimi oga yangu naosha kiungo kimoja kimoja, napitia mwili mzima nikiwa natoka nasikiliza kwa umakini mlio wa ndala zangu za Umoja "ngaaatu ngaaatu" nisiposikia huo mlio basi siku inakuwa imeharibika sitaweza kula ata ungekuwa wali maharage.
Nasumbuliwa na majinamizi ya miguu michafu niliyopata kuiona nikiwa ndotoni, mpaka leo kijana mimi miaka AroBainI sijampata Sindelelah wangu binti mwenye miguu misafi iliyotunzwa kama yangu. Mahusiano mengi yameisha kutokana mamanzi kuwa na sura mpya lakini miguu ya zamani.
Mimi nikitoka kuoga lazima nipakae mafuta miguu yangu, kila wiki lazima nikate kucha vidole vyote vya mguuni.