Nguo za ndani za mitumba: Mkombozi wa maskini, msambaza magonjwa!

Nguo za ndani za mitumba: Mkombozi wa maskini, msambaza magonjwa!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KWA UFUPI


  • Baadhi yao wamezaliwa na kukuta utamaduni huo, nao wakauendeleza na kisha kuurithisha kwa watoto wao. Zipo sababu nyingi za wengi katika jamii kuendelea kununua na hata kuvaa mitumba, zikiwamo za kiuchumi, mazoea.




Nguo hizo zimekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania maskini, hasa wanawake kwani wakati mwingine huuzwa kuanzia Sh300 hadi Sh500.


Ni saa tano asubuhi jua linawaka, soko la Karume wilayani Ilala jijini Dar es Salaam tayari limejaa watu wa kila rika. Kwa jumla, ni mchanganyiko au mseto wa wafanyabiashara , wachuuzi na hata wanunuzi.

Wengi waliomo ndani ya soko hilo kwa maana ya wanawake na wanaume ama wananunua au kuuza nguo , viatu chakavu ambavyo tayari vimevaliwa na watu wa nchi tajiri za magharibi. Nguo hizo ndizo zimepewa jina maarufu la mitumba.

Miongoni mwa ‘mitumba’ hiyo, ni nguo za ndani, sidiria na hata chupi za kike na kiume, ambazo zimesheheni katika meza nyingi za wafanyabiashara huku nyingine zikiwa zimetundikwa.

Ununuzi huo wa nguo za mitumba ni jambo ambalo hadi asilimia 90 ya Watanzania hasa wa kipato cha chini au kawaida wamelifanya kaitka maisha yao.

Baadhi yao wamezaliwa na kukuta utamaduni huo, nao wakauendeleza na kisha kuurithisha kwa watoto wao. Zipo sababu nyingi za wengi katika jamii kuendelea kununua na hata kuvaa mitumba, zikiwamo za kiuchumi, mazoea.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanaonya na kusema kuwa nguo hizi za mitumba, hususan za ndani zina madhara mengi kwa wanawake na wanaume wanaopenda kuzitumia.

Hivi karibuni, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limepiga marufuku na kutoa kipindi cha mwisho kwa wafanyabiashara hao wanaouza nguo za ndani za mitumba, kuacha kuuza bidhaa hizo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kipindi cha mpito kuisha, ambapo kwa sasa TBS wamechukua uamuzi wa kuzichoma moto nguo hizo. Msemaji wa TBS, Rhoida Andusamile anasema hatua hiyo ni utekelezaji wa matakwa ya agizo la sheria ya mwaka 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani zilizokwishatumika.

Profesa Malise Kaisi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (Muhas) anasema, yapo madhara makubwa ya kuvaa nguo za ndani za mitumba kutokana na unyeti wa maeneo yanapovaliwa nguo hizo.

Anasema, walioketi juu ya hatari zaidi ni wanawake ambao maumbile yao yapo wazi zaidi na ni rahisi kwa vijidudu kuingia kwa urahisi pindi wanapokaribia vitu hatarishi. Kwa mfano, anasema, nguo za ndani zilizovaliwa huenda zina vijidudu vya fangasi au chawa wa sehemu za siri, mwanamke anapovaa hupata maambukizi hayo.

“Endapo watavaa nguo hizo bila kuzifua kwa usahihi na kuzichemsha, kisha kuzipiga pasi, ni rahisi kupata maambukizi. Lakini pia, si vyema kimaadili kuvaa nguo zilizokwishavaliwa na watu wengine” anasema Prof Kaisi. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwanyamala, Sophinias Ngonyani anasema nguo za ndani za mitumba ni hatari kubwa kwani zinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwa wanawake.
Anasema, nguo hizo huwa zimevaliwa na mtu mwingine ambaye hajulikani na inawezekana mtu huyo ana matatizo ya ngozi, fangasi, au hata magonjwa ya zinaa ambayo huweza kubakiza vijidudu katika nguo hiyo na vijidudu hivyo vikamuingia mtu wa pili.

“Hasa kwa wanawake ni hatari zaidi. Kama aliyevaa nguo hizo ana fangasi, basi fangasi hao wanaweza kuingia katika sehemu za mwanamke au mwanaume na kusababisha madhara makubwa katika mwili wake, ” anasema.

Anasema fangasi hupenda kuishi sehemu zenye unyevuunyevu, na wanapoingia katika sehemu za siri hasa za mwanamke huweza kuingia hadi katika kizazi na kusababisha madhara makubwa ikiwemo mimba kuharibika au kutokushika mimba.

“Wanawake wanapata madhara makubwa bila kufahamu chanzo chake. Wanajikuta wanawashwa sehemu za siri na kumbe ni fangasi waliowapata katika nguo za ndani za mitumba” anasema.

Dk Ngonyani anasema, nguo za ndani za mitumba si nzuri na anashauri watu wavae nguo za dukani ambazo hata hivyo nazo zinatakiwa zifuliwe na kukauka vyema kisha kupigwa pasi kabla ya kuvaliwa.

“Nguo za ndani za mitumba zinashikwa na watu wengi wakati wanapozichagua, zimevaliwa na mtu asiyefahamika ambaye hatujui ana matatizo gani…hazifai kabisa” anasema

Kwa upande wao, baadhi ya wanawake waliohojiwa kuhusu sababu ya wao kupenda kuvaa nguo za ndani za mitumba wanasema kuwa, ni uzuri wa nguo hizo, bei rahisi na tamaduni walizozikuta katika familia zao.

Aisha Mbwene (si jina lake halisi) anasema, nguo za ndani za mitumba ni bei nafuu na imara kuliko nguo za ndani za dukani, lakini pia, anadai zina uzuri wa kipekee na zinadumu.

“Ingawa kweli nguo za ndani za mtumba zinaleta kichefuchefu fulani hasa ukitafakari kuwa zimevaliwa na mtu mwingine, lakini ni imara kuliko za dukani, hasa sidiria,” anasema.

Anasema, nguo hizo zimekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania maskini, hasa wanawake kwani wakati mwingine huuzwa kwa bei ya kuanzia Sh300 hadi 500.

“Kwa maisha ya Mtanzania, hizi nguo za ndani ni nafuu kwa sababu kuna watu hawana uwezo wa kununua nguo kwa gharama ya shilingi 1500 au 2000,” anasema Aisha. Imani iliyojengeka
Lakini uvaaji wa nguo za ndani za mitumba, umechukua sura mpya kwa baadhi ya watu kwani, limeingiliana na mtazamo wa kiimani.

Juliana Masinde anachambua madhara ya kuvaa nguo za ndani za mtumba katika mtazamo wa kiimani na kusema, nguo hizo huweza kubeba laana, au nguvu za giza na kuzihamisha toka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

“Zipo habari nyingi za watu waliobeba mashetani, magonjwa ya kurithi na laana kwa sababu ya kuvaa nguo za ndani za mtu mwingine. Kiimani, hata nguo mpya ya dukani inahitaji kuombewa kwanza,” anasema

Wafanyabiashara wa soko hilo nao walieleza kuwa, kwao biashara hiyo ni mkombozi kiuchumi.

“Hapa kinachotakiwa kufanyika ni serikali kuhimiza usafi, watu wakinunua hizi nguo wazifue kwa maji ya moto na kuzipiga pasi, si kuzipiga marufuku kabisa. Wanatutesa” anasema Silvester Mongi, mfanyabiashara, Karume.

Historia ya mitumba

Nguo hizi za mitumba zilianza kupata umaarufu Afrika wakati wa kuingia kwa imani zikiwamo za kidini na kuzorota kwa uchumi katika nchi hizo.

Zamani hizo, wamisionari wa Kizungu waliofika nchini kuhubiri dini walileta marobota ya nguo za zamani yaani mitumba, zikiwemo nguo za ndani kwa ajili ya watu wasiojiweza.

Hata hivyo, baadaye misaada hiyo iligeuka kuwa biashara nzuri na kubwa ambapo wafanyabiashara wengi walinunua nguo hizo na kuziuza kwa bei rahisi.

Kwa upande mwingine, nguo za ndani za mitumba zimedaiwa kusaidia watu wengi wenye kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za nguo mpya hasa zile zinazouzwa madukani. chanzo.Nguo za ndani za mitumba: Mkombozi wa maskini, msambaza magonjwa! - mwanzo - mwananchi.co.tz
 
Si kila king'aacho ni dhahabu, kuna magonjwa mengi sana ya ngozi, nimeona kwa macho yangu watu wakiugua magonjwa haya hatarishi. Tafadhali chukua tahadhari kila ununuapo "kifuniko cha asali" kwa wewe Dada yangu mpenzi, hakikisha unakifua na kukiloweka kwa muda kisha kinyooshe kwa pasi na moto mzuri tu, ndipo kafunikie asali yako!

Usipofanya hivyo wote hatubaki salama, sio mwenye asali wala mlinaji wa asali, chukua tahadhari
 
Hahahahaha asali aisee nimesoma mara3 ndio nikang'amua. Sasa na vifuniko vya wanaume vinafunika mdomo?
 
Heeeeeeheeeeeee! Mwana wamkulima! Si amewekeza kwenye asali? TBS si wapo?
 
Kweli nimekubali kiswahili ni lugha inayo inayo jitahidi kupunguza ukali wa maneno.
 
Unazungumzia asali yenyewe mbichi au za siku hizi zakuchovyaa ambayo inabeba magonjwa mengi
 
Asali, asali aisee nimeelewa baada ya kusoma posts za watu,duh tafsida imetumika vizuri.
 
Si kila king'aacho ni dhahabu, kuna magonjwa mengi sana ya ngozi, nimeona kwa macho yangu watu wakiugua magonjwa haya hatarishi. Tafadhali chukua tahadhari kila ununuapo "kifuniko cha asali" kwa wewe Dada yangu mpenzi, hakikisha unakifua na kukiloweka kwa muda kisha kinyooshe kwa pasi na moto mzuri tu, ndipo kafunikie asali yako!

Usipofanya hivyo wote hatubaki salama, sio mwenye asali wala mlinaji wa asali, chukua tahadhari
Kifuniko cha asali kilowekwe? then kifuliwe? kivipi yani!!! hebu fafanua vizuri sio kila mtu anaelewa. unajua asali mara nyingi menaona inauzwaga kwenye ka dumu ka lita 5. sasa kale kakizibo kake ndo kafuliwe? utakafuaje sasa? au utakalowekaje sasa? mbona kitu kisichowezekana? coz ni plasitc
 
Teh sisi dukani kwetu kila kitu kipo byeeeee.

Ha ha ha, najiuliza zetu sisi tutaita vifuniko vya nini?

Maana naona tafsida ni ya upande mmoja tu.

Kaboom saidia hapa, maana nataka nijue kama vifuniko vyetu vipo nije kununua, ila ningependa nimkute mwanao Heaven Sent ndo anisaidie kujipima maana wewe unaweza kuniuzia famba.
 
Ha ha ha, najiuliza zetu sisi tutaita vifuniko vya nini?

Maana naona tafsida ni ya upande mmoja tu.

Kaboom saidia hapa, maana nataka nijue kama vifuniko vyetu vipo nije kununua, ila ningependa nimkute mwanao Heaven Sent ndo anisaidie kujipima maana wewe unaweza kuniuzia famba.
Teh vyenu vinaitwa vifuniko vya "achali"

Teh daddy mnaweza kutaniana kote, sio kwa binti ake aisee. Urafiki utazikwa mapema, so atakupima tu yeye mwenyewe
 
Teh vyenu vunaitwa vifuniko vya "achali"

Teh daddy mnaweza kutaniana kote, sio kwa binti ake aisee. Urafiki utazikwa mapema, so atakupima tu yeye mwenyewe

No! Unajua mwanaume anakuwa so objective ku-judge uzuri wa kitu alichovaa mwanamke na vivyo hivyo mwanamke kwa mwanaume.

Sasa eti nivae halafu mwanaume mwenzangu aseme imekutoa, imekupendeza, aaaghh! Siyo kabisa.

Dad anatakiwa kuelewa kwamba It's just business!
 
No! Unajua mwanaume anakuwa so objective ku-judge uzuri wa kitu alichovaa mwanamke na vivyo hivyo mwanamke kwa mwanaume.

Sasa eti nivae halafu mwanaume mwenzangu aseme imekutoa, imekupendeza, aaaghh! Siyo kabisa.

Dad anatakiwa kuelewa kwamba It's just business!
Hahahaa daddy kwenye hilo suala na duka atafunga tu kwa kweli. itabidi tu yeye mwenyewe akusifie au utasubiri ufike home wifi akusifie. Hizo habari ni mwiko kwa daddy
 
Back
Top Bottom