Nguvu inayomsukuma mwanamke kwenye mahusiano, ni umasikini

Nguvu inayomsukuma mwanamke kwenye mahusiano, ni umasikini

Nguvu inayomsukuma mwanamke, kuingia kwenye mahusiano, kwa asilimia kubwa huwa ni umasikini.

Wengi wanaingia kwenye mahusiano, ili kupata uhakika wa kula, kuvaa, kumiliki majengo, magari, kumiliki miradi, kupanda vyeo n.k

Hawaingii kwenye mahusiano, kwa sababu ya mapenzi ya kutoka moyoni; ndio maana hela ya mwanaume inakuwa ni ya wote, na hela ya mwanamke inakuwa ni ya kwake.

Ndio maana mwanaume fukara, asiyekuwa na kipato au ramani ya maisha; huwa anakimbiwa na wanawake, kwa sababu anakuwa hana vitu ambavyo humvutia mwanamke.

Kama itatokea mwanaume akapendwa na mwanamke aliyejitosheleza kiuchumi, na mwanamke ndio akawa analipa 'bill' bila kugusa hela ya mwanaume; hapo ndipo kutakuwa na mapenzi ya kweli; kwa sababu kilichomvutia mwanamke kwenye hayo mahusiano sio pesa, bali ni upendo tu.​
120% UKWELI mtupu
 
Jaman hata Adam aliumbwa kwanza , akapewa bustani then Mungu akaona anahtaji msaidizi, ndo akamuumba Eva

Vivyo hvyo kwa maisha ya Sasa , mwanaume anatakiwa ajiweze kwanza ndipo atafte mwanamke..
Mzee wangu alioa akiwa na 34 mimi nikazaliwa akiwa na 35
Na kila siku napata sababu mpya ya kuona mzee wangu aliamua kufanya ilo la kujiwekeza kwanza na kwakweli sijawai muona baba yangu au mama yangu hawatoshi maana kila shida aisee inamalizwa na wale makomandoo hakuna kutia tia huruma kwa watu
 
Hata mke wa ndoa anae kudharau kisa huna pesa siku ukizipata tu uanza kuwa mpole akiamini mda wowote ataporwa. Pesa na mwanamke ni nature
 
Ndio maana, Sasa hivi naona soko la mahusiano linahama toka kwa wanawake wazuri wenye tako kubwa na linahamia kwa mabinti wa kishua ambao kwao mambo safi. Inasemekana binti wa kishua akikupenda amekupenda kwelikweli. Je kuna ukweli?
Ndio ...akili ndogo sana
 
Wanawake 90% wakiwa na pesa za maana hawawezi kamwe kua wife material.

Mwanaume unaejielewa tafuta pesa uoe mwanamke wa hadhi yako. Mimi siwezi kuolewa na fukara mwenzangu wakati kuna mtu ana maisha anataka kunionyesha dunia upande wa pili ipoje.

Hakuna mtu hapendi pesa hata wanaume wanapenda maisha mazuri ila ndo hawawez kuchagua mtu mwenye hela awaoe..mwanaume haolewi anahangaika mbaka kufa kwake apate pesa ake aoe.

Kwanini umpende mtu asie na maisha wakati wewe mwenyewe huna maisha? Huo ni ufal*.
Yaan binti mrembo alafu kwenu hohe hahe bado uolewe na hohehahe mwenzio????
Wanaume tupeni break.
Mbombo ngafu fijo
 
Nguvu inayomsukuma mwanamke, kuingia kwenye mahusiano, kwa asilimia kubwa huwa ni umasikini.

Wengi wanaingia kwenye mahusiano, ili kupata uhakika wa kula, kuvaa, kumiliki majengo, magari, kumiliki miradi, kupanda vyeo n.k

Hawaingii kwenye mahusiano, kwa sababu ya mapenzi ya kutoka moyoni; ndio maana hela ya mwanaume inakuwa ni ya wote, na hela ya mwanamke inakuwa ni ya kwake.

Ndio maana mwanaume fukara, asiyekuwa na kipato au ramani ya maisha; huwa anakimbiwa na wanawake, kwa sababu anakuwa hana vitu ambavyo humvutia mwanamke.

Kama itatokea mwanaume akapendwa na mwanamke aliyejitosheleza kiuchumi, na mwanamke ndio akawa analipa 'bill' bila kugusa hela ya mwanaume; hapo ndipo kutakuwa na mapenzi ya kweli; kwa sababu kilichomvutia mwanamke kwenye hayo mahusiano sio pesa, bali ni upendo tu.​
Huo ni uongo bwana, hakunaaa
 
Ongeza na hii

Na ndio maana mwanamke anaweza kuwa na mwanaume wa kumtoa kimaisha na kuigiza anampenda wakati huo akawa na mwanaume anaempenda sasa, huyu anaweza kuwa hata kapuku tu.
 
Back
Top Bottom