Kweli serikali iajiri walimu haswa shule za msingi kuna uhaba wa kutisha,mwalimu mmoja anafundisha mpaka masomo 12.
Kwa kawaida vipindi vipo 8 kwa siku unakuta mwalimu kila siku ana vipindi 8 na vingine anakosa muda wa kufundisha.
Vipindi 8 kwa siku kwa mwl mmoja
Ataandaa andalio la somo saa ngapi?
Ataandaa zana za kufundishia na kujifunzia kwa vipindi 8 kwa siku saa ngapi?
Atasahihisha mazoezi/kazi za wanafunzi saa ngapi?
Ataandaa nukuu za somo saa ngap?
Serikali wekeni mpango hata kila shule iwe na walimu wasiopungua 8.shule nyingi zina walimu 4-6 haswa hizi shule za vijijini.