Nguvu kuelekezwa katika ajira za walimu na matundu ya vyoo

Nguvu kuelekezwa katika ajira za walimu na matundu ya vyoo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Baada ya kujenga madarasa 15,000 na kuwezesha wanafunzi wote waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza, Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu inaelekeza nguvu kwenye ajira za walimu na mtundu ya vyoo. Azma ni kuimarisha ubora wa elimu kwa manufaa ya wananchi na Taifa. #MamaYukoKazini

Screenshot_20220119-144424.jpg
 
Kweli serikali iajiri walimu haswa shule za msingi kuna uhaba wa kutisha,mwalimu mmoja anafundisha mpaka masomo 12.

Kwa kawaida vipindi vipo 8 kwa siku unakuta mwalimu kila siku ana vipindi 8 na vingine anakosa muda wa kufundisha.

Vipindi 8 kwa siku kwa mwl mmoja

Ataandaa andalio la somo saa ngapi?

Ataandaa zana za kufundishia na kujifunzia kwa vipindi 8 kwa siku saa ngapi?

Atasahihisha mazoezi/kazi za wanafunzi saa ngapi?

Ataandaa nukuu za somo saa ngap?


Serikali wekeni mpango hata kila shule iwe na walimu wasiopungua 8.shule nyingi zina walimu 4-6 haswa hizi shule za vijijini.
 
Back
Top Bottom