Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Adhabu ya kifungo cha kutofanya kampeni imemalizika jana saa tano na dakika 59 usiku, kwa hiyo kuanzia asubuhi hii ya leo ya tarehe 9 yuko huru kuendelea na kampeni zake.
That punishment wasn't a fair play in political grounds lakini waswahili wanasema kumpiga chura teke ni kumwongezea hatua kwakuwa tembea ya chura ni ya kurukaruka.
Lissu aliamua kukubaliana na uamuzi wa tume pamoja na kuwa adhabu husika haikuwa sahihi...lakini akatumia muda huo kujiachia na kufanya mengi ambayo kama si adhabu husika asingeyafanya kamwe.
Mengi aliyoyafanya yalikuwa burudani tosha kwake na kwa jamii lakini pia yakamuongezea umaarufu na ufahamu mpya wa maisha ya mtanzania wa kawaida huko mitaani na huko uswazi.
Matukio yake yote yametengeneza headlines na kufunika matukio mengine yote ya kiserikali kwa wiki hii yote ya adhabu. Tukio la ufunguzi wa stand mpya Mbezi lilidoda na kudorora kuliko tukio la Lissu kuzuiwa kuingia mkoa wa Pwani pale eneo la Gogoni.
Kuna ufunuo wa ajabu kwa CHADEMA na LISSU. Japo mamlaka na wapinzani wa Lissu na Chadema hawawezi kulikubali hili,lakini huo ndio ukweli mchungu. Lissu is unbeatable. CHADEMA is unconquered.
Mitandaoni, vijiweni, makazini, sehemu za starehe, majumbani na kila mahali ni mijadala ya Lissu na Chadema. Mfano hai ni hapa JF. Asilimia 90 ya habari za siasa ni Lissu na Chadema, bila hivi vitu viwili ni kama hakuna mijadala ama mijadala inakuwa imepoa na kupooza kabisa.
Kuna maono makubwa sana kwa CHADEMA NA LISSU, umaarufu wao umefika kileleni na kuvunja rekodi kupindukia. Ni ukweli mchungu kwenye masikio ya wapinzani wao.
Ujasiri wa ajabu wa Lissu umeipeleka Chadema next level, umewapa Wananchi mwamko mpya lakini wakati huohuo umepeleka ganzi kubwa CCM yote juu mpaka chini.
Ukufunzi wake mahiri wa sheria za uchaguzi kwenye majukwaa ya kampeni ni kigezo kingine kinachoongeza mvuto na ufuasi mkubwa kila alikopita.
Kibonzo cha DW kinamuonesha Lissu kama nyani mzee aliyekwepa mitego mishale na vizingiti vingi, lakini kiroho kinatoa tafsiri pana zaidi ya MBEBA MAONO. Kumbuka sterling hafi, mbeba maono hafi.