ndammu
JF-Expert Member
- Apr 21, 2017
- 3,971
- 4,440
Kama huu.Nilikuwa Mbezi jana wakati wa ufunguzi. Tuweni wakweli na bila chembe ya unafique uzinduzi ulidoda magari ya serikali na chama yalikuwa chini kidogo ya idadi ya wahudhuriaji.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama huu.Nilikuwa Mbezi jana wakati wa ufunguzi. Tuweni wakweli na bila chembe ya unafique uzinduzi ulidoda magari ya serikali na chama yalikuwa chini kidogo ya idadi ya wahudhuriaji.
Mkuu umenena, umechambua, umeeleweka. Lissu amebadilili kabisa game, tokea alipotua Tanzania akitokea Ubelgiji kwenye matibabu. CCM wanapojaribu kumjibu Lissu, wanakwama zaidi.Adhabu ya kifungo cha kutofanya kampeni imemalizika jana saa tano na dakika 59 usiku, kwa hiyo kuanzia asubuhi hii ya leo ya tarehe 9 yuko huru kuendelea na kampeni zake.
That punishment wasn't a fair play in political grounds lakini waswahili wanasema kumpiga chura teke ni kumwongezea hatua kwakuwa tembea ya chura ni ya kurukaruka.
Lissu aliamua kukubaliana na uamuzi wa tume pamoja na kuwa adhabu husika haikuwa sahihi...lakini akatumia muda huo kujiachia na kufanya mengi ambayo kama si adhabu husika asingeyafanya kamwe.
Mengi aliyoyafanya yalikuwa burudani tosha kwake na kwa jamii lakini pia yakamuongezea umaarufu na ufahamu mpya wa maisha ya mtanzania wa kawaida huko mitaani na huko uswazi.
Matukio yake yote yametengeneza headlines na kufunika matukio mengine yote ya kiserikali kwa wiki hii yote ya adhabu. Tukio la ufunguzi wa stand mpya Mbezi lilidoda na kudorora kuliko tukio la Lissu kuzuiwa kuingia mkoa wa Pwani pale eneo la Gogoni.
Kuna ufunuo wa ajabu kwa CHADEMA na LISSU. Japo mamlaka na wapinzani wa Lissu na Chadema hawawezi kulikubali hili,lakini huo ndio ukweli mchungu. Lissu is unbeatable. CHADEMA is unconquered.
Mitandaoni, vijiweni, makazini, sehemu za starehe, majumbani na kila mahali ni mijadala ya Lissu na Chadema. Mfano hai ni hapa JF. Asilimia 90 ya habari za siasa ni Lissu na Chadema, bila hivi vitu viwili ni kama hakuna mijadala ama mijadala inakuwa imepoa na kupooza kabisa.
Kuna maono makubwa sana kwa CHADEMA NA LISSU, umaarufu wao umefika kileleni na kuvunja rekodi kupindukia. Ni ukweli mchungu kwenye masikio ya wapinzani wao.
Ujasiri wa ajabu wa Lissu umeipeleka Chadema next level, umewapa Wananchi mwamko mpya lakini wakati huohuo umepeleka ganzi kubwa CCM yote juu mpaka chini.
Ukufunzi wake mahiri wa sheria za uchaguzi kwenye majukwaa ya kampeni ni kigezo kingine kinachoongeza mvuto na ufuasi mkubwa kila alikopita.
Kibonzo cha DW kinamuonesha Lissu kama nyani mzee aliyekwepa mitego mishale na vizingiti vingi, lakini kiroho kinatoa tafsiri pana zaidi ya MBEBA MAONO. Kumbuka sterling hafi, mbeba maono hafi.
View attachment 1594518
kundi hili ndilo linalo tembea na mabadiliko bila kujiuliza litapata faida gani, kwa kawaida huwa halina cha kupoteza[emoji848][emoji848][emoji848][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji818][emoji1548][emoji1534][emoji1548][emoji1534]Mr Mshana, As your nephew kindly accept this comment, never take it as inappropriate or particularly offensive.
Katika siasa za ushindani ukiona vitu vitatu vifuatavyo vinatokea na unaeshindana nae ndio mnufaika mkubwa, jiulize sana.
1) Unapoona wafanya biashara na Elites hawakuungi mkono, na ulio nao wanakukimbia jiulize sana. Kwakuwa kundi hili lina kila uwezo na ujuzi wa kukusaidia kwa vyovyote vile utavyo hitaji wewe.
2) Ukiona kundi ambalo unataka likuunge mkono na kundi hilo halina cha kupoteza lisipo muunga mkono mpinzani wako ( wananchi wa chini )jiulize zaidi kwa maamuzi yao na ujitafute kwako kuna upungufu gani ? kundi hili ndilo linalo tembea na mabadiliko bila kujiuliza litapata faida gani, kwa kawaida huwa halina cha kupoteza.
3) Mawasiliano ni ujuzi wa wewe msemaji na msikilizaji mnavyo weza kukonnect. Mama anapo zungumza kwa lugha ya kitoto kwa mtoto wake mdogo, wazazi wa kiume huona mama anapiga kelele na mwanae. Lakini wewe baba unaesema vizuri ukiongea na mtoto wako mdogo anaweza akapata taabu sana kuelewe au asikuelewe kabisa.
Magufuli ni mfano wa 99.7% ya Watanzania, hawawezi kuongea kiingereza fasaha, kwa broken yake hiyo wengi haiwasumbui kwa kuwa hawana uwezo wa kufananisha english proficiency kwa sahihi kabisa.
NB: Kwa tunaofahamu kiingereza hata Lissu proficiency yake iko chini kabisa. Na hili muulize yeyote anaefahamu kingereza atakwambia. (hana uwezo wa kutumia maneno sahihi kwa wakati sahihi, kwa tukio sahihi, use of noun vocaburary, verb, a message whose ingenuity or verbal skill or incongruity has the power to invoke laughter).
Kwa mfano: watoka Dar es salaam au nje ya nchi tukienda Upareni vijijini tunapo ongea kiswahili chetu bila lafudhi sahihi ya kipare haiwi rahisi kuconnect na pals kirahisi, mpaka waaminishwe na mzee huyu ni kijana wangu.
Kwa hiyo bwana mkubwa anapongea kama mshamba ni rahisi kwake kuunganika na washamba wenzake akiwa anaongea nao, kwa bahati mbaya washamba Tanzania ndio wengi hasa vijijini Tanzania.
Ushamba wake Magufuli wa kuongea na matendo unampa credit sana kwa washamba ambao ni wengi. Mshamba yeyote yule awe Mchaga, Msukuma, Mbondei, Muhaya, Mgogo au kabila lolote lile, wanao ongea nae hujiunganisha moja kwa moja na watu wa kabila la muongeaji anako toka. Tabia za ujumla na kuaminika kwa kundi hilo la "washamba" ndio humpa ama faida au hasara muongeaji.
Aibu. Ninafunika macho na masikio kwa English hiyo! PhD?!!!From Birmingham palace!?[emoji848][emoji30][emoji2960][emoji2827]
Very encouraging and inspiring indeed.