SoC02 Nguvu ya Bangi na Hempu kwa Afrika

SoC02 Nguvu ya Bangi na Hempu kwa Afrika

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 12, 2022
Posts
24
Reaction score
12
“Fikiria watu wanalima hempu na wanazalisha kila kitu kuanzia chakula mpaka nishati bila petroli”- Josh Tickell
1.png

Wakazi wa Afrika hawakati miti na kutumia vinyesi vya wanyama kupika kwa sababu hakuna mbadala wa kuni na kinyesi cha wanyama, kupitia mtambo wa gasifaya. Kila kaya inaweza kujitosheleza kwa mahitaji yake ya nishati pasipo kukata miti kwa kutumia rasilimali ya hempu.
2.png

3.png


4.png


Wakazi wa Afrika wanapotumia mafuta ya taa kumulika, ambayo si salama kwa afya zao si kwamba hakuna mbadala wake. Hempu inawezesha kuzalishwa kwa paneli za mwanga wa jua na betri. Vibatari na chemli zinatoa mwanga bora na safi kupitia mafuta ya hempu. Kabla ya mafuta ya taa yatokanayo na petroli taa za kumulika usiku zilitumia mafuta ya mbegu za hempu na samaki aina ya nyangumi (whales).
5.png

6.png


Wakazi wa Afrika wanapobeba ndoo za maji kichwani si kwamba hakuna rasilimali na tekinolojia za kutosha kuwezesha maji kusafirishwa kwa bomba na nishati za kuwezesha kusafisha na kusukuma maji. Hempu inatoa malighafi zinazowezesha uwepo wa maji safi na salama kila mahali. Paneli zenye kutumia mwanga wa jua kuvuna maji angani moja kwa moja bila uhitaji wa mabomba zinaweza kuzalishwa kwa malighafi za hempu. Pia mtambo wa ‘‘Atmospheric Water Generator ’’
8.png


9.png

unaweza unganishwa na mtambo wa gasifaya na kuvuna maji angani.
Wakazi wa Afrika wanapoishi kwenye nyumba za tembe si kwamba hakuna rasilimali za kutosha kuwezesha uwepo wa makazi bora. Hempu inawezesha kuzaliswa bidhaa za ujenzi kama tofali, zege, plasta, mbao, bati, vigae vya sakafuni, ukuta na darini, rangi za kuta, vanishi, milango na madirisha (PVC), choo, sinki, mabomba na viungio vyake,mbao, ubao wa MDF na kadhalika.
11.png


Watoto na wakazi wengine wa Afrika wanapopitia changamoto za miundombinu na vifaa duni ya kutolea elimu si kwamba hakuna rasilimali za kutosheleza kuboresha miundombinu na vifaa ya elimu. Hempu inawezesha kuboresha miundombinu na vifaa vya kutolea elimu ikiwamo majengo, madawati, karatasi, wino, kompyuta, simu na waya wa faiba/ mkonga.
12.png
.

13.png

14.png


Wakazi wa Afrika kukosa madawa si kwamba hakuna rasilimali za kuwezesha kupatikana madawa, hempu ilitumiwa kutibu zaidi ya 2/3 ya maradhi ya mwanadamu kabla ya katazo. Hempu inatibu zaidi ya

magonjwa 100 ikiwamo malaria ugonjwa unaogharimu maisha ya watoto zaidi ya 100 kila siku wenye miaka chini ya 5 kila siku kwenye taifa la Tanzania. Hempu inawezesha kupatikana neti bora na nafuu kijikinga na mbu. Pia ethano ya hempu inaweza kutumika kama dawa ya kuulia mazalia ya mbu pasipo kutumia sumu kudhuru viumbe wengine kama samaki.
15.png

16.png


Wakazi wengi wa Afrika kutumia mavazi ya mitumba si kwamba hakuna rasilimali na tekinolojia ya kuwezesha kujitengenezea mavazi mapya. Hempu inawezesha kila mtu kujitengenezea nguo zake mwenyewe kama ambavyo Baba wa Taifa la India, Mahatma Gandi alivyoweza kutumia gurudumu la kusokota uzi kusokota uzi wa hempu na kufuma kwa kutumia mtambo wa kufuma nguo kwa mikono.

17.png


Usafiri wa uma wa shida si kwamba hakuna rasilimali za kutosha kuwezesha usafiri wa uma unaotoshelezana wakuaminika. Kupitia hempu vyombo vya usafiri wa uma vinaweza kuzalishwa kwa kutumia malighafi za hempu na kuendeshwa kwa kutumia nishati za hempu,halikadhalika kwa usafiri wa binafsi.
19.png

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Kuthibi Madawa ya Kulevya (DCEA) wamerekebisha kanuni ya 12, kuruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya madawa na utafiti. Marekebisho haya hayaugusi mmea pacha wake wa hempu ambao una matumizi na faida zaidi ya 50,000. Pia mmea wa hempu tofauti na maruhana/ daga hauna ulevi.

Ni dhahiri kwa mabadiliko ya sheria hii hempu bado ipo kifungoni na mkulima wa kawaida anasafari ndefu kuiona siku atakapoweza kulima zao la hempu pasipo kusumbuliwa na vyombo vya dola.

Tuna ndoto kwamba siku moja, tutaweza kula chapati na maziwa ya hempu kutoka kwenye mashamba yetu, tutakuwa na uhakika wa kula mboga za majani mwaka mzima toka miti ya hempu inayomea njee ya nyumba zetu n.k.

uma.png


Tuna ndoto kwamba siku moja, tutaweza kuingia kwenye maduka ya hempu ya; vitu vya reja reja, madawa, migahawa, baa, kilimo, nguo, steshenari, muziki, ujenzi, bomba, magari, vituo vya mafuta n.k.
22.png


23.png


Tuna ndoto kwamba siku moja, wakulima na wananchi wa Afrika wataweza kuweka makapi ya hempu kwenye gasifaya ili kuendesha trekta,pampu za maji,jenereta na vyombo vya usafiri ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya nishati visukuku katika soko la dunia.

Screenshot_20220914-222327[1].png


Tunandoto ya kuona deni lote la Afrika linalipwa kwa hempu. Hempu imekua fedha halali huko Marekani hadi kwenye miaka 1800. Wamarekani waliweza kulipa kodi, madeni / mikopo ya kilimo kwa maana ya msingi uliokopwa na riba. kwa hempu.

25.png


Tunandoto ya kuona wakazi wa Afrika wakilipa bima ya Afya kwa hempu.Afrika inaweza kuruhusu wakazi wake kulima hempu majumbani ili wapate mbadala wa kuliia bima ya afya kama ilivyofanya Thailand ili kujenga mazingira kama yaliyokuwuwepo karne ya 6 ambayo Mfalme Henry VIII wa Uwingereza alimtaka kila mwananchi kulima miche 100 ya hempu na wamiliki wa ardhi kulima robo ekari ya hempu kwa kila ekari 60 wanazomiliki.

Tunandoto ya kuona bara la Afrika ikifanya biashara ya kimataifa yenye tija kwa kuuza nguo za hempu njee kama China. Kuuza mbao na samani kama Swedeni,Finland,Kanada na Austia. Pia njugu za hempu na bidhaa zaidi ya 25,000.

26.png


Tunandoto ya kuona wakazi wa Afrika wakipata ajira na ujira kupitia hempu. Hempu inauwezo wa kuajiri watu 200,000 kwa kila hekta 250,000 za hempu.
why cat.png


Tunandoto ya kuiona Afrika ikiachana na kuni, mkaa,karatasi, mbao n.k. za miti na ukataji miti kwa kuzalisha bidhaa mbadala zake kupitia hempu.
mbao.png


Kufahamu zaidi kuhusu hempu soma kitabu au “E BOOK” bure inayoitwa Hempu kwa Afrika kwa kutembelea “HEMPOWER AFRICA” kwenye mitandao ya kijamii.
 

Attachments

  • 29.png
    29.png
    25 KB · Views: 12
  • why cat.png
    why cat.png
    50.5 KB · Views: 13
  • mbao.png
    mbao.png
    80.4 KB · Views: 12
  • end.png
    end.png
    270.5 KB · Views: 12
  • end.png
    end.png
    270.5 KB · Views: 14
  • 8.png
    8.png
    34.8 KB · Views: 13
Upvote 5
Hili jambo hapa kwetu lingetufaa sana...na nitajitolea kuwa mdau wa kwanza katika kuandaa mikakati kwenye kuhakikisha tunafanikiwa
 
Kwahiyo hemp Tanzania inachukuliwa kama madawa ya kulevya au imekaajekaaje? Na je nini kifanyike ili fursa hiyo watu walime na zao lilete viwanda vingi kama ilivo bidhaa zake
 
Kwahiyo hemp Tanzania inachukuliwa kama madawa ya kulevya au imekaajekaaje? Na je nini kifanyike ili fursa hiyo watu walime na zao lilete viwanda vingi kama ilivo bidhaa zake
Majibu yapo kwenye kitabu cha Hempu kwa Afrika, pata nakala yako sasa.
IMG-20220716-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom