Kama ni ushindi, basi CHADEMA walishashinda mechi kabla hata ya mechi yenyewe kuchezwa. Hii mbinu ya kimapambano ni kubwa sana na haijapata kutokea hapa Tanzania.
Nimeona polisi kila kona ya jiji na unaweza ukafikiri kuna shambulio la kijeshi linasubiriwa kutoka majeshi ya nchi jirani au kutoka taifa kubwa duniani. Ni wazi kabisa kuwa hofu ya jeshi la polisi na uongozi wa nchi hii kwa CHADEMA ni kubwa sana.
Tafsiri yake:
1. CHADEMA inaogopwa sana kutokana na kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi
2. Watanzania wanaosemwa kuwa wapole na watulivu ukweli ni kwamba wanaogopwa kuliko majeshi ya nchi jirani
3. Viongozi wetu wapo tayari kutumia nguvu kupitiliza na hawako tayari kufanya mazungumzo na kusikiliza haja za wananchi
4. Watanzania wakiwa na umoja wanatatua matatizo sugu mara moja
5. Serikali ya Samia imeendelea kujitangaza kwa jumuiya ya kimataifa kama serikali yenye kutumia nguvu kupindukia na hairuhusu njia ya mazungumzo
Hitimisho
CHADEMA wameonesha nguvu kubwa kama chama cha upinzani kuweza kutetemesha vyombo vya dola na kwamba viongozi wa CHADEMA na CHADEMA kama taasisi ya kisiasa wana nguvu na ushawishi mkubwa sana katika nchi hii. Hata kama maandamano hayatafanyika, CHADEMA tayari wameshafikisha ujumbe, na kazi sasa ni kuendelea kushinikiza hadi hali ya uongozi wa nchi hii ibadilike.