Zanzibar 2020 Nguvu ya Dodoma katika maamuzi ya Urais wa Zanzibar (CCM)

Hao home grown candidate waliotajwa kwenye list wote ni mafisadi tu. huyo mmoja alitimuliwa na dk. Shein na huyo mwengine nae ana madudu ya kujineemesha akiwa serikalini.

Wote wana back up ya matajiri nyuma yao. Watatumika kuifisidi nchi kuliko Maelezo. Wakichaguliwa hao sitegemei kuona hata barabara ikipigwa repair kwenye shimo, hawashibi kabisa utafikiri hawafi.

Kama uchunguzi utapita kwa hawa watangaza nia, wanaweza kusafiri na kutafuta urai wa nchi nyengine
 
Dodoma ni makao makuu ya ccm
Majina ya wanaopitishwa ni wazanzibari tupu,na haijatokea akapitishwa mtu asiekuwemo katika waliopendekezwa.Tatizo lipo wapi?
 
Unamjua Jecha wewe
 
"kazi ya kwanza na muhimu kulizo zote ya chama cha siasa ni kushinda uchaguzi"

Pius Msekwa
 
Tabia za Ngalawa ulizofunika ni zipi mkuu?
 
Nasikia wanampa Mbarawa!! Ila kwa Maalimu ataisoma number dadadeki
Mbarawa out
Mwinyi out
Dr Khalid Salum Mohammed IN
 
Big up.. umenena vyema mkuu, mwenye masikio na asikie!
 
Kwa iyo mzee mwinyi siyo mzanzibar? Je ilikuwaje akawa rais wa Zanzibar, na kama inavyosemekania Husein alizaliwa Zanzibar na baadae akaenda masomoni nje ya nchi je ni wivu tu Ndiyo unaowasumbua kutaka kusema hakukuaa Nanyi kama waote kwenye vijiwe vya kahawa?je mulikubali vipi awe ni mbunge wenu kwa vipindi vyote?!

Kwa wenye akili Husein Ndiyo chaguo sahihi kwa sasa Zanzibar na ataleta mapinduzi ya uchumi makubwa kabisa RAIS JPM SIYO MJINGA KUFANYA NAE KAZI BILA KUMUAMISHA WIZARA KWA MUDA WOTE. ANGALIA MAGEUZI MAKUBWA ALIYO FANYA JPM. KWA KIPINDI KIFUPI SANA KULE BARA
 
wewe mtoa mada bichwa kubwa huna akili, wewe ni mpumbavu plus!! tuwe na wivu nyie na ukoo wenu mnatulisha?

yakhe sie hatutaki monarchy bongo msitulazimishe pelekeni utawala wa kifalme Arabuni!kwanini hamchoki kuleta hii mada mwataka kuufanyia nini urais? kuna list ya watu mwataka kuwaua? si kwa kulazimisha huku!!

huku Zenjibari hatutaki kuongozwa na mzanzibara full stop!! Mwinyi abaki kuwajambieni huko huko bara ati!! Zenjibari hatutaki kujambiwa na kuongozwa na mgeni ati!!
 
Mwinyi alikua mbunge wa kina kingwendu, kisarawe huko.. zanzibar ni mgeni.
 
Kwenye baba kua Raisi na mtoto kua Rais sion kama ni shida, endapo tu vigezo na masharti vimezingatiwa.
Mbona madaktari,wauguzi, engineers nk wanataka watoto wao wawe kama wao na hatuon ni uimla wa fani. Wacha watu wapambanie nafasi zao kwa utashi wao hata kukiwa na mbeleko iwe imetokana na uwezo uliooneshwa kabla na muhusika.
Ni hayo tu.
 
you can tell my dead body about that not me alive!! kuna tofauti ya kuiga taaluma ya mzazi na kulazimisha kushika cheo cha mzazi! uongozi ni kitu cha kuzaliwa nacho si cha kusomea kama utawala!! huwezi kusema jinsi Mwinyi alivyokuwa Rais na mwanae atakuwa kama yeye, Mzee Ruksa aliwahi kujiuzulu uwaziri kwa kuwajibika , mwanae ana kashfa ya upotevu wa mabilioni wizarani ila hata tamko hajatoa!!Baba ni sheikh mseahili mtoto ni mzungu mwarabu wa Misri wapi na wapi!!

Yaani urais imekuwa mali ya familia yenu hata kama mnatudharau wapiga kura tulio wengi kwakuwa tunashinda na kulala njaa basi msifikie kutujambia kwa kiwango hiki!!
 
Roho za kwanini za wa sawahili mimi ni mzanzibari sioni shida iko wapi kwa Husein kuwa kiongozi kwani baba yake Ndiyo anamrithisha nchi au anagombea kama wengine?! Dhambi ya ubaguzi itatuponza ndugu zangu. Tuwe makini. Na kwa bahati mbaya tunaowabagu Ndiyo wanaofaa kuongoza Zanzibar Wewe kama ni ACT chama kipya sana kwa sasa si wakati sahihi wa kuchukua Zanzibar, bahati mbaya Sharif Hamad ana miaka 76 ni mzee sana sasa,Mwinyi ndiye Rais Zanzibar JPM Rais Bara utakuja kunikumbuka.
 
Chama kingine kuongoza zanzibar na bara iwe ccm ni sawa na mbuzi kutaga mayai.
 
Ishu si nani anafaa kuwa Raisi, Mbunge, au Diwani. Ila ni namna gani CCM inaweza kuendelea kushika hatamu ya uongozi.

So kwa namna hiyo chama kina nguvu kubwa zaidi kuliko mtu/watu, na hakiwezi acha kwa chama kingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…