SoC02 Nguvu ya kushindwa (Mandonga vs Kaoneka)

SoC02 Nguvu ya kushindwa (Mandonga vs Kaoneka)

Stories of Change - 2022 Competition

JOZEY MAGANGA

New Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
3
Reaction score
0
Si Kila unapoteleza na kujikuta umeanguka kwamba wewe ni mvivu sana au wew hujui chochote,la hasha! Ni muda na wakati uliamua tu kushindwa kwako kutokee Ili kufanikiwa kwako kung'are kama nyota ya alfajiri!

Tuangalie pambano la mandonga MTU KAZI na KAONEKA, aliyesema atashusha mvua ya mangumi, aliyesema atampiga mtu nguvu kama Ngoma ndio yeye alieshushiwakipigo kikali Hadi mtu KAZI alikuwa amelewa kwasababu ya kipigo alichopewa kutoka kwa KAONEKA.

Katika lille pambano ni kweli KAONEKA alishinda kwa kumpiga mandonga Ila mandonga kwa kupigwa kwake kumemuongezea umaarufu mara mia Moja na KAONEKA kwa kushinda kwake hakujamuongezea thamani kama aliyoipata mandonga kutokana na kichapo alichopata. Huenda mandonga angelazimisha kushinda lille pambano asingepata umaarufu kama huu alioupata Sasa.

Muda mwingine tusikate tamaa Ila tusilazimishe kufanikiwa kwa Kila jambo tunalolitaka, mfano mtu analazimisha kununua gari matokeo yake anafanikiwa kununua na siku hio hio anapata ajari anakufa kumbe muda sahihi wa kununua Gari ulikuwa haujafika, mtu anaweza akalazimisha kupata fedha matokeo yake anaingia kwenye ujambazi anakamatwa na kuuwawa kabisa!

Muda mwingine tusikate tamaa kwa tufanyayo Ila tusilazimishe tunapoona inashindikana huenda mungu Kuna njia nyingine nzuri amekuandalia ya kukufanikisha.

Mfano mwingine ni Mimi mwenyewe, ndoto zangu zilikuwa ni kuwa mwanasisa, na wakati nasoma nilichagua masomo ya Sanaa kwani nilikuwa nayapenda, nilikuwa napenda na nafanya vizuri kwenye midaharo ya Ndani ya shule na shule Hali iliyopelekea Hadi walimu kuniambia nikazane Kuna kitu wanakiona Ndani yangu huenda ntakuwa mwanasisa mkubwa sana, wakati huo dada yangu alishafika chuo kikuu na alikuwa anasoma uhandisi na yeye kidato cha SITA alichukua PCM, Mimi nilichukua masomo yangu ya Saba tu ya Sanaa ikiwemo hesabu!

Matokeo ya kidato cha nne yakatoka nikamwambia dada aniangalizie matokeo, alipoyaona akaona masomo yote nimefaulu sana ikiwemo hesabu Ila hakufurahia alipogundua niliacha fizikia, kemia na baiologia ndio akawaambia na wazazi, walikasirika sana walipogundua sikusoma masomo ya sayansi.

Hivyo wakajakigundua kuwa Kuna EGM naweza nikaenda kusoma kwenye hayohayo masomo ya Sanaa kwani hesabu nilifaulu vizuri.

Walinilazimisha nikasome kwani dada yangu ni mwanamke na alisoma PCM nami
ni mwanaume haifai kusoma HKL Bora nikasome EGM, nilienda kusoma Ila nilisoma Ili nifaulu na sio kupenda, matokeo yalivyotoka sikufanya vizuri kuniwezesha kusoma shahada na nyumbani walipojua familia yote ilinigeukia na kunilaumu, wakaniona Mimi sio kitu.

Kila siku wananisemasema ndipo niliamua kukimbia nyumbani na kwenda mkoa mwingine ambako sikuwa na ndugu, nikaanza kulala kwenye maboksi na nikawa nafanya kibarua chochote Ili niishi Ila kadri siku zinavozidi kusonga nikawa nakumbuka nyakati zile nafanya vizuri kwenye masomo yangu ya Sanaa,jinsi nilivyokuwa napata zawadi na kusifiwa na walimu!

Nikajisemea hata kama nyumbani hawataki Ila nitasoma Sanaa ilibidi nikaongea na mkuu wa chuo Fulani kuwa nataka kusoma stashahada(diploma) ya siasa Ila sitohudhuria vipindi vyote darasani Ili nipate muda wa kutafuta ada, yule mwalimu alinielewa na nikawa nasaidia fundi, nauza mitumba, nauza Karanga na nikipata kiasi cha pesa nalipa ada kidogo kidogo huku Nalala kwenye boksi!

Nikabahatika kumaliza na kufaulu diploma yangu vizuri, nikamwambia dada nimemeliza diploma ya siasa na nataka niombe kusoma digrii.

Akanambia kwanza ni diploma pili ni diploma ya siasa akanambia tena mkopo hautapata nikasema Mimi nitaomba Ila nikikosa sitolaumu kwani nitakuwa nimejaribu, Mungu ni mkubwa nikaomba chuo na nikapata chuo na nikapata mkopo asilimia mia Moja na nataraji kuingia mwaka wa pili sasa silali tena kwenye boksi.

FUNZO, kushindwa Kuna nguvu kama utakuwa tayari kuijua nguvu hio. Mungu alinipangia kusoma siasa, ndugu walivyolazimisha nisome uchumi ndio kushindwa kwangu kukatokea na walipoamua kuacha kunilazimisha ndio nikafauru.

NB. Hivi siku Ile mtu KAZI angelazimisha kushinda si angeuawa na kaoneka,Ila kashindwa na umaarufu kapata na alieshinda hajapata umaarufu, tutegemee kumwona mtu kazi kung'ara zaidi
 
Upvote 0
Back
Top Bottom