Nguvu ya Maamuzi juu ya Maisha Yako ya Kitajiri hapa Duniani

Nguvu ya Maamuzi juu ya Maisha Yako ya Kitajiri hapa Duniani

Hapo ndo penye changamoto,ila huu uzi ni SHULE,unajitahid kuelekeza na unaeleweka.

Mkuu ujue vijana wengi tunashindwa kufanya mambo mengi sana kwa sababu ya kukosa uthubutu kama ulivyoelezea hapo awali. Wengi tuna mawazo lakini MAAMUZI ya kwamba sasa nafanya ni wachache sana wenye huo msukumo....!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu ujue vijana wengi tunashindwa kufanya mambo mengi sana kwa sababu ya kukosa uthubutu kama ulivyoelezea hapo awali. Wengi tuna mawazo lakini MAAMUZI ya kwamba sasa nafanya ni wachache sana wenye huo msukumo....!
Endelea kutoa elimu wataelewa tu.Japo mie nimefanya maamuzi lakini najifunza vitu hapa mdau, asante sana
 
Wasalaaaaaaam Wanajamvi

Leo nimeona nifunguke kwa upande huu, kama “heading” yangu inavyosema ili kusaidia wanajamvi wenzangu kuondokana na hali hii ngumu ya kimaisha ambayo kwayo sisi watanzania tulio wengi tumekuwa tukilalamika kila uchwao ya kwamba “ “MAISHA HAYASOGEI”

Nianze kwa kusema, wengi wetu tumekua tukisikia kelele za wadau mbalimbali kuhusu kujikwamua kiuchumi kwa kufanya Biashara au ajasiriamali na kuondokana na dhana ya KUAJIRIWA. Sikawii kusema wengi tumekuwa tukiyatupilia mbali mawazo hayo kwa sababu 1 au 2 hivi; utasikia mtu akisema

1. Mtaji wa hiyo Biashara/Ujasiriamali nautolea wapi wakati mimi ndio kwanza nimemaliza chuo/shule au;

2. Niache kazi (Kuajiriwa) wakati bado sijajipanga?, natafuta mtaji kwanza halafu baadae nianzishe Biashara yangu

Ngaja niseme hivi wadau, tunajicheleweshea wenyewe hayo maisha mazuri ya asali na maziwa. Mafanikio yangu ama yako yapo kwenye maamuzi yako binafsi. Ni mimi au wewe wa kuamua sasa nahitaji kuwa na pesa kwa kiasi gani.

Ajira tulizonazo zinatusaidia tu kupata pesa ya kuendesha maisha tena yale ya kawaida sana. Mwezi haujaisha lakini kamshahara kako kamekatika siku nyingi sana kutokana na majukumu tuliyonayo kifamilia na kijamii kwa ujumla na kama ofisi yako haina yale magumashi wanayopigaga wenzetu, basi madeni yanaanzia hapo mpaka mshahara mwingine utakapokuja. Mwisho wa siku mshahara wako unakuwa ni nusu kulipia madeni na nusu kukusogeza tena kwenye nusu nyingine ya mwezi ujao.

Hali hii ya maisha itaendelea hivyo mpaka pale utakapofanya MAAMUZI wewe mwenyewe(kwa ku‘resign’) ama kwa kusaidiwa na mwajiri wako (kwa maana ya kufukuzwa kazi). Kwani hata mwajiri wako akikuongeza mshahara bado matumizi yako pia huongezeka. Hivyo hali huendelea kuwa ile ile.

Maamuzi ya kile unachokihitaji kwa maisha bora ukijumlisha na jitihada stahiki kwenye hayo maamuzi, amini usiamini utaona ni kama ndoto kwenye maisha yako. Nina mifano kadhaa ya marafiki zangu ambao walifukuzwa kazi na kwa kupitia hali hiyo walijua hakuna namna nyingine ya haraka ya kuendelea kuwaingizia kipato ili familia zao zisione hilo “gap”. Basi WAKAAMUA kungia kwenye Biashara na kufanya yale mambo ambayo kabla walikuwa wakiyapenda na kufikiria kuyafanya lakini kwa sababu ya Ajira zao walishindwa na kudhani walistahili kutafuta mtaji kwanza.

Hivi leo hakuna hata mmoja ambaye utamwambia arudi kuajiriwa akakuelewa unampigia stori gani. Kimsingi walifanya MAAMUZI na wanayaona matunda ya MAAMUZI yao. Haya sasa tuachane na hizi stori nyingi, nashauri kuanzia muda huu ambao umemaliza kusoma hizi hadithi ambazo wengine watadhani ni zile za aina ya kusadikika, Ufanye UAMUZI.

Sijakwambia uache kazi (kwa wewe uliye kazini kwa sasa), na kwa wewe ambae ulikuwa unatafuta kazi achana na mawazo hayo, naomba vile vitu ambavyo ulikuwa unafikiria kuvifanya na ukadhani vinahitaji mtaji ili kuviaanza vianze sasa. Kinachohitajika hapa ni MAAMUZI na sio Mtaji.

Kama unadhani haiwezekani, mimi nakwambia INAWEZEKANA na naomba unitafute kwa ushauri zaidi endapo unadhani unahitaji ushauri zaidi. Tanzania hii ni yetu na ninakuomba kwa moyo wote kabisa tuijenge kwa pamoja.


MAAMUZI + JITIHADA = MAFANIKIO
Mm Jana tu nimeamuwa kujiajili.
 
Dah hepu pitia thread zote. Kwani mtaji huwa unapatikanaje? Mtaji unatafutwa hivi utapata tu mtaji kwa kuweka miguu juu unasema huna mtaji. teh teh teh. come on guys...Tusiwe wavivu kutafakariii...Kitu cha kwanza ni kujua unahitaji mtaji kiasi gani ili kukamilisha wazo lako. Sasa hapo ndo unaanza mbinu mbali mbali. Unaweza ukafanya saving ili uanze at least mahali fulani. Au unaweza kuomba support kwa ndugu marafiki na familia. Njia nyingine ni kwenda na wazo lako kwa watu wenye hela zao. Na wazo si wazo tu ili mradi eti lipo kichwani au sababu ya wewe kutaka kulima nyanya ni maneno uliyosikia kwamba nhyanya zinawatoa watu yaani unatakiwa uwe na a clear business plan sio kusema tu mimi nataka kulima nyanya halafu unaita ni wazo. Wazo linaandikwa chini na plan yake vizuri kabisa. Kama hujaliandika chini hilo si wazo una hallucinate tu..teh teh teh. Njia nyingine ni kujaribu kutafuta mkopo kwa ndugu na jamaa sasa hii inategemea uaminifu wako upo vipi. Kama unawafanyiaga usalnii basi hawawezi kukuchukulia serious. Lakini best way ya kuanza ni kuanza kidogo kidogo kwa kiasi kile ambacho umedunduliza mwenyewe. Huwezi kulaza damu kwa hela ambayo umeidunduliza mwenyewe kwa jasho kwa hiyo utapambana tu huku ukijifunza taratibu. Kama hujawahi fanya biashara ya milioni usikurupuke kutamani kufanya biashara ya milioni 20. Anza na milioni moja kwanza. Kwa mfano wewe ungesema wazo lako ni lipi ingesaidia zaidi..
Nimekuelewa vizuri sana mkuu, wazo langu ni kufungua bakery hapa nnapoishi sasahv natafuta mtaji tu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
mkuu nikwambie tu mahitaji na si wazo
CHEREHANI AINA YA JAMES,GODORO 1 LA UREFU WA FUTI 6 UPANA 1/2 INCHI NAJORA LA KITAMBAA CHA MOROKO!
Mkuu! Naona umeweka baadhi ya mahitaji ukimaanisha wazo tayari lipo lkn tatizo ni mtaji. Lakini ngoja nikwambie hivi, mimi sijui ww unafanya nn kwasasa lkn naweza nikakushauri mambo mawili ya kuwa ;

1. Jiwekee muda wa lini unataka kuanza kutekeleza hilo wazo lako, (utasema unataka kuanza sasa ) basi anza kufanya savings za kuweza kupata kiasi unachokihitaji kwa kuanzia. Ukifanya hvyo sio tu utakuwa unatafuta mtaji lkn pia utakuwa umeanza kutekeleza hilo wazo lako. Baada ya kipindi fulani utajikuta kumbe tayari umeshafika nusu ya safari ya kule uendako

2. Andika wazo lako vzr , ukionesha ni kwa vipi litakuwa na faida kama litatekelezwa tena kwa kianzio kdg kabisa. Shirikisha jamaa zako wanaokufahamu vzr kwa kuwaeleza kinagaubaga khs wazo lako na nikwambie tu huwezi kukosa mtu Wa kukwambia tunafanyaje fanyaje mkuu! akimaanisha lini tuanze mchakato wa utekelezaji

3. Onesha ya kuwa uko serious na hilo wazo lako. Weka nguvu na akili yako yote ktk kutafuta huo mtaji. Acha uoga, jiamini ya kwamba unaweza, aibu weka pembeni na Omba Mungu wakati wote akupe afya njema na uondokane na uvivu usiokuwa na tija. Simamia maamuzi yako kwa nguvu zako zote ukiamini kuwa inawezekana. Binadamu yeyote asijekukatisha tamaa ya kwamba hutoweza. Ziba masikio na usonge mbele.

4. Kwakuwa wazo lako liko kimaandishi, basi hakikisha kila siku unapitia utekelezaji wa majukumu yako ya kila siku kama unayatekeleza vzr na kama kuna marekebisho ya kiutekelezaji basi fanya na endelea kutumia nguvu zako ktk kufanikisha yote.

MAAMUZI + JITIHADA = MAFANIKIO
 
Afrikans be praying all night😀😀😀😀, Guys prayer is not in the success equestion, prayer is in the revelation equestion. DECISION MAKING is in the success equestion, You have to make a decision and be sound.Thats all!!
Make a decision
Make a decision
Make a decision
Fanya maamuzi
Fanya maamuzi
Fanya maamuzi
Usisahu kuja kunishukuru baadae ushauri wangu ukikusaidia.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom