Nguvu ya Michezo

Nguvu ya Michezo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
微信图片_20220929082125.jpg




Katika mashindano ya mbio za Marathon ya Berlin 2022, bingwa wa dunia wa mbio za marathon, Eliud Kipchoge amevunja rekodi yake ya dunia aliyokuwa akiishikilia mwenyewe na kutwaa ubingwa huo kwa muda wa saa 2, dakika 1 na sekunde 9. Kikomo cha uwezo wa binadamu kimevukwa tena. Kwa Wachina wengi, Kipchoge ni mtu mwenye ushawishi kwao na mfano wa kuigwa.

Timu ya taifa ya mbio za marathon ya China kwa sasa inafanya mazoezi katika eneo la Eldoret, Kenya. Kabla ya Kipchoge kusafiri hadi Berlin, vijana hawa wa Kichina mara nyingi walifanya mazoezi na timu ya Kipchoge, akiwemo yeye mwenyewe. Hili ni jambo la kufurahisha sana kwa wanariadha vijana wa timu ya China. Kwa sababu mafunzo na watu wenye nguvu kuliko wewe yatakusaidia zaidi. Na kumtazama Kipchoge kwa karibu, au hata kufanya mazoezi naye, kunaleta mabadiliko mazuri kimya kimya.

Mawasiliano ya michezo kati ya China na Afrika yalianza katika miaka ya 1950. Mwaka 1957, ndani ya mwaka mmoja tu baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Misri, China ilituma timu ya mpira wa meza kuitembelea Misri, na kuwa timu ya kwanza ya michezo ya China kukanyaga ardhi ya bara la Afrika. Baada ya kuingia katika karne ya 21, wakati diplomasia ya umma inazidi kuwa muhimu, michezo imekuwa ikionyesha nafasi muhimu sana kama daraja la uhusiano kati ya China na Afrika, na maudhui na mawasiliano kati ya pande hizo mbili yamekuwa ya aina mbalimbali.

Kwa mfano, kwa msaada wa China, mpira wa meza na voliboli na michezo mingine iliyokuwa dhaifu siku za nyuma barani Afrika sasa imeimarika sana, na baadhi ya wanariadha katika michezo hii wamefanikiwa kuonekana kwenye uwanja wa michezo ya Olimpiki. China pia imetuma wanariadha kufanya mazoezi barani Afrika, kama vile mbio za masafa marefu, na manufaa yake yameonekana mara nyingi. Mbali na kufunzana kwa wachezaji, China pia imejenga makumi ya viwanja vya michezo mikubwa kwa nchi za Afrika.

Kama washiriki wawili wakuu duniani, michezo ya China na nchi za Afrika ina sifa zao pekee. Ikiwa ni moja ya mambo yanayokuza uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika, mawasiliano ya michezo yamefanya kazi kubwa katika kukuza viwango vyao vya michezo vya kila upande, kuonyesha kwa vitendo dhana ya jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja na kuleta maendeleo ya michezo duniani. Kama mshika rekodi huyu ya dunia wa mbio za Marathon Elud Kipchoge alivyosema hivi karibuni, "tukiwa wachezaji wa China na Kenya, tumeungana na kukuza michezo ya dunia".
 

Attachments

  • VCG31N1427172969.jpg
    VCG31N1427172969.jpg
    53.2 KB · Views: 5
  • 下载.jpg
    下载.jpg
    20.3 KB · Views: 4
  • 下载 (1).jpg
    下载 (1).jpg
    20.9 KB · Views: 6
Back
Top Bottom