NGUVU YA MSAMAHA: Stori niliyosikia kwa January Makamba mwaka 2021

Bonge La Afya

Member
Joined
Dec 19, 2016
Posts
35
Reaction score
83
Anasema mwaka 2008, akiwa Msaidizi wa Rais Kikwete, alikuwa ziarani Makete. Alikuwa anatumia gari na dereva wake wa Ikulu, aliyeazimwa kutoka Jeshini. Jioni moja, kuna document ya Rais alitaka aifanyie kazi na kumpelekee kesho yake saa 1:00 asubuhi. Akamwambia dereva amfuate saa 12:30 asubuhi.

Dereva akachelewa, kila akimpigia simu hampati, akatafuta usafiri mwingine kitu kilichopelekea acheleweshe document na kukaripiwa. Baadaye dereva alipoonekana, alisema aliitwa amfuate bosi mwingine mkubwa zaidi. Kutokana na mazingira ya kuonekana anaharibu kazi basi akaomba atafutiwe dereva mwingine lakini akaambiwa aendelee naye walau hadi Mbeya.

Akalazimika kuendeshwa tena na “mbaya wake”, kumbuka dereva kwa muda ule tayari anajua anaondoka. Safarini wote walikuwa kimya. Walipokaribia Tukuyu, dereva akaanza kutoa machozi, akisema Tukuyu ndio kwao, na ndio anarudi baada ya muda mrefu na amewaambia ndugu zake waje kumuona kwenye msafara wa Rais.

Akaanza kuelezea story ya maisha yake kwamba, alipomaliza Darasa la saba mwaka 1984 alikuja Dar kuuza mahindi ya kuchoma junction ya Mwenge. Siku moja akaona kundi la vijana wanakimbia kutokea njia ya Lugalo; alipouliza, akaambiwa hao ni vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hivyo wanakimbia kutoka Jeshini Kunduchi kuelekea uwanja wa UDSM ikiwa ni zoezi la kupimwa pumzi.

Palepale, akatelekeza jiko la mahindi na kuunga tela. Kwakuwa alianzia mbio katikati, akafika wa kwanza UDSM kule kukawa na mtu anachukua majina ya vijana waliofika kwanza. Akaandikwa na kuambiwa kesho waripoti Kunduchi kwa vipimo zaidi.

Alipofika Kunduchi getini asubuhi akakuta orodha inayotumika kuwaingiza watu ndani kwa vipimo zaidi ni ile ya UDSM. Akaingia, akapasi vipimo, taarifa zake nyingine zikakusanywa, akapelekwa mafunzo. Jeshini huko akaingia kama mwanamichezo, mwanamieleka.

Baadaye, akawa anachukuliwa na dereva mmoja kama msukuma-gari kwa sababu dereva huyo alikuwa na 109 (one ziro nine) lisilowaka hivyo kwa nguvu za jamaa ilibidi awe anamchukua. Mwisho akajifunza gari, akawa dereva mzuri na mwenye nidhamu na ndio maana baada ya miaka kadhaa akaazimwa Ikulu. Wakati anamueleza kisa hiki, Mheshimiwa machozi yalikua yanamtoka.

Akamsamehe, dereva akabaki kazini. Baada ya ziara kikapita kitambo kidogo hawajaonana, muheshimiwa naye akaingia kwenye ubunge (akatoka Ikulu). Siku moja akamuona bado yumo kwenye msafara wa Ikulu, bado ana nidhamu. Akamuomba aelezee kisa hiki. Maisha yake ni elimu ya kutokata tamaa na maisha.

TUSAMEHEANE.
 
Sasa kaka Festo.. katika story Yako...wapi ipo nguvu ya msamaha?...ujue umenichosha sana kulisoma lithread lako?

Haya mastory ya bodaboda wakiwa vijiweni wamelala juu ya pikipiki msiwe mnayaleta humu....,mnatuudhi wengine!!!

Usimsingizie January Makamba kakupa story hii,...wewe ni boda boda...unadanganyana na bodaboda wenzako wakati wa mchana..then uleta mistory ya hovyo humu Jamii forum.
 
[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787] umetisha Mkuu dah
 
Sasa kaka Festo.. katika story Yako...wapi ipo nguvu ya msamaha?...ujue umenichosha sana kulisoma lithread lako?

Haya mastory ya bodaboda wakiwa vijiweni wamelala juu ya pikipiki msiwe mnayaleta humu....,mnatuudhi wengine!!!

Usimsingizie January Makamba kakupa story hii,...wewe ni boda boda...unadanganyana na bodaboda wenzako wakati wa mchana..then uleta mistory ya hovyo humu Jamii forum.

Kaka we huna simile
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1417]
 
Kwa style hii tatizo la nguvu za kiume halitaisha
 
Sasa kaka Festo.. katika story Yako...wapi ipo nguvu ya msamaha?...ujue umenichosha sana kulisoma lithread lako?

Haya mastory ya bodaboda wakiwa vijiweni wamelala juu ya pikipiki msiwe mnayaleta humu....,mnatuudhi wengine!!!

Usimsingizie January Makamba kakupa story hii,...wewe ni boda boda...unadanganyana na bodaboda wenzako wakati wa mchana..then uleta mistory ya hovyo humu Jamii forum.
Jamaa haeleweki Stori ipo nusunusu Tu
 
Anasema mwaka 2008, akiwa Msaidizi wa Rais Kikwete, alikuwa ziarani Makete. Alikuwa anatumia gari na dereva wake wa Ikulu, aliyeazimwa kutoka Jeshini. Jioni moja, kuna document ya Rais alitaka aifanyie kazi na kumpelekee kesho yake saa 1:00 asubuhi. Akamwambia dereva amfuate saa 12:30 asubuhi.

Dereva akachelewa, kila akimpigia simu hampati, akatafuta usafiri mwingine kitu kilichopelekea acheleweshe document na kukaripiwa. Baadaye dereva alipoonekana, alisema aliitwa amfuate bosi mwingine mkubwa zaidi. Kutokana na mazingira ya kuonekana anaharibu kazi basi akaomba atafutiwe dereva mwingine lakini akaambiwa aendelee naye walau hadi Mbeya.

Akalazimika kuendeshwa tena na “mbaya wake”, kumbuka dereva kwa muda ule tayari anajua anaondoka. Safarini wote walikuwa kimya. Walipokaribia Tukuyu, dereva akaanza kutoa machozi, akisema Tukuyu ndio kwao, na ndio anarudi baada ya muda mrefu na amewaambia ndugu zake waje kumuona kwenye msafara wa Rais.

Akaanza kuelezea story ya maisha yake kwamba, alipomaliza Darasa la saba mwaka 1984 alikuja Dar kuuza mahindi ya kuchoma junction ya Mwenge. Siku moja akaona kundi la vijana wanakimbia kutokea njia ya Lugalo; alipouliza, akaambiwa hao ni vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hivyo wanakimbia kutoka Jeshini Kunduchi kuelekea uwanja wa UDSM ikiwa ni zoezi la kupimwa pumzi.

Palepale, akatelekeza jiko la mahindi na kuunga tela. Kwakuwa alianzia mbio katikati, akafika wa kwanza UDSM kule kukawa na mtu anachukua majina ya vijana waliofika kwanza. Akaandikwa na kuambiwa kesho waripoti Kunduchi kwa vipimo zaidi.

Alipofika Kunduchi getini asubuhi akakuta orodha inayotumika kuwaingiza watu ndani kwa vipimo zaidi ni ile ya UDSM. Akaingia, akapasi vipimo, taarifa zake nyingine zikakusanywa, akapelekwa mafunzo. Jeshini huko akaingia kama mwanamichezo, mwanamieleka.

Baadaye, akawa anachukuliwa na dereva mmoja kama msukuma-gari kwa sababu dereva huyo alikuwa na 109 (one ziro nine) lisilowaka hivyo kwa nguvu za jamaa ilibidi awe anamchukua. Mwisho akajifunza gari, akawa dereva mzuri na mwenye nidhamu na ndio maana baada ya miaka kadhaa akaazimwa Ikulu. Wakati anamueleza kisa hiki, Mheshimiwa machozi yalikua yanamtoka.

Akamsamehe, dereva akabaki kazini. Baada ya ziara kikapita kitambo kidogo hawajaonana, muheshimiwa naye akaingia kwenye ubunge (akatoka Ikulu). Siku moja akamuona bado yumo kwenye msafara wa Ikulu, bado ana nidhamu. Akamuomba aelezee kisa hiki. Maisha yake ni elimu ya kutokata tamaa na maisha.

TUSAMEHEANE.
Huyo Makamba ndiyo ameandika hiki kituko? Anawaona watanzania wote ni Mandina au?
Hiyo biashara ya kuchoma mahindi haikuwepo miaka hiyo, ni biashara ambayo ilianza kufanyika awamu ya pili ya rais Mkapa.
Mahindi ya kuchemsha ndiyo angalau ilikuwepo kwa muda mrefu na wakina dada/mama walikua wanachemsha majumbani kwao na kuanza kuzunguka na sufuria mitaani. Pia Mayai ya kuchemsha na ilikua ni biashara kongwe.

Baadhi ya biashara kongwe za vyakula na vyakunywa na vya kulambwa ambavyo vilikuwepo wayback mitaani ni;
Mahindi ya kuchemsha
Mayai ya kuchemsha
Mapupu/supu ya ngozi ya ng'ombe
Mishikaki
Mihogo ya kukaanga - maeneo ya shule (Chips ziliikuta mihogo, na zilipokuja chips, mihogo ikaanza kuitwa chips dume)
Kachori
Sambusa
Kababu
Visheti
Ufuta
Kaukau
Askrim
Togwa
Bwimbwi
Miguu ya kuku, vichwa na utumbo vya kukaangwa

Wahenga mnaweza mkajazia
 
Yan driver kalia....makamba kalia..hawa wajinga watazamwe vizur inawezekana kuna kitu hakikua sawa..mnaliaje liaje wanaume wawili
Mimi nilipofikia pale anasema...eti eti Mwanajeshi akaanza kulia.....daah...nikaona kabisa huyu lazima atakua bodaboda!!!

Hawa jamaa wana story za hovyohovyo sana wanapokua kwenye vijiwe vyao.
 
Anasema mwaka 2008, akiwa Msaidizi wa Rais Kikwete, alikuwa ziarani Makete. Alikuwa anatumia gari na dereva wake wa Ikulu, aliyeazimwa kutoka Jeshini. Jioni moja, kuna document ya Rais alitaka aifanyie kazi na kumpelekee kesho yake saa 1:00 asubuhi. Akamwambia dereva amfuate saa 12:30 asubuhi.

Dereva akachelewa, kila akimpigia simu hampati, akatafuta usafiri mwingine kitu kilichopelekea acheleweshe document na kukaripiwa. Baadaye dereva alipoonekana, alisema aliitwa amfuate bosi mwingine mkubwa zaidi. Kutokana na mazingira ya kuonekana anaharibu kazi basi akaomba atafutiwe dereva mwingine lakini akaambiwa aendelee naye walau hadi Mbeya.

Akalazimika kuendeshwa tena na “mbaya wake”, kumbuka dereva kwa muda ule tayari anajua anaondoka. Safarini wote walikuwa kimya. Walipokaribia Tukuyu, dereva akaanza kutoa machozi, akisema Tukuyu ndio kwao, na ndio anarudi baada ya muda mrefu na amewaambia ndugu zake waje kumuona kwenye msafara wa Rais.

Akaanza kuelezea story ya maisha yake kwamba, alipomaliza Darasa la saba mwaka 1984 alikuja Dar kuuza mahindi ya kuchoma junction ya Mwenge. Siku moja akaona kundi la vijana wanakimbia kutokea njia ya Lugalo; alipouliza, akaambiwa hao ni vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hivyo wanakimbia kutoka Jeshini Kunduchi kuelekea uwanja wa UDSM ikiwa ni zoezi la kupimwa pumzi.

Palepale, akatelekeza jiko la mahindi na kuunga tela. Kwakuwa alianzia mbio katikati, akafika wa kwanza UDSM kule kukawa na mtu anachukua majina ya vijana waliofika kwanza. Akaandikwa na kuambiwa kesho waripoti Kunduchi kwa vipimo zaidi.

Alipofika Kunduchi getini asubuhi akakuta orodha inayotumika kuwaingiza watu ndani kwa vipimo zaidi ni ile ya UDSM. Akaingia, akapasi vipimo, taarifa zake nyingine zikakusanywa, akapelekwa mafunzo. Jeshini huko akaingia kama mwanamichezo, mwanamieleka.

Baadaye, akawa anachukuliwa na dereva mmoja kama msukuma-gari kwa sababu dereva huyo alikuwa na 109 (one ziro nine) lisilowaka hivyo kwa nguvu za jamaa ilibidi awe anamchukua. Mwisho akajifunza gari, akawa dereva mzuri na mwenye nidhamu na ndio maana baada ya miaka kadhaa akaazimwa Ikulu. Wakati anamueleza kisa hiki, Mheshimiwa machozi yalikua yanamtoka.

Akamsamehe, dereva akabaki kazini. Baada ya ziara kikapita kitambo kidogo hawajaonana, muheshimiwa naye akaingia kwenye ubunge (akatoka Ikulu). Siku moja akamuona bado yumo kwenye msafara wa Ikulu, bado ana nidhamu. Akamuomba aelezee kisa hiki. Maisha yake ni elimu ya kutokata tamaa na maisha.

TUSAMEHEANE.
Kanaflow
 
Back
Top Bottom