Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii mistari ya kitabu cha mwanzo kuhusu uumbaji ni mistari maarafu sana. Wengu tunaijua. Lakini tunajuaga ni story tuu tunasimuliwa kuhusu uumbaji. Kumbe kunae watu wanaichambua deep namna hii.Ufanye nini?
Wadau wengi sana wamefikia hatua ya kuhoji wafanye nini ili kutoka katika hali ya kujichua. Zingatia kwamba madhara haya yapo kwa wanawake na wanaume pia, hivyo hapa tunatazama pande zote. Leo nitaandika kifupi tu kuhusu suluhisho la kudumu la tatizo hili.
Kujichua ni tatizo la kiroho
Nilianza kufafanua kiini cha tatizo hili ili kufuta kabisa ile dhana kwamba ni tatizo la nje tu, yaani la kimwili na kujaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani tatizo hili limejikita upande wa roho zaidi kuliko mwili. Kutambua kuwa tatizo hili ni la kiroho ni hatua muhimu mno katika kutafuta suluhu yake. Sasa basi, ili kung'oamzizi wa fitina, usitarajie kusuluhisha kwa kutazama mambo ya mwilini.
Yako mapendekezo mengi ambayo yamekuwa yakitolewa kama suluhu ya tatizo la kujichua, shidani kwamba yote hulenga suluhu ya kimwili. Mfano, acha kukaa peke yako, tafuta mpenzi, usitazame picha za ngono nk. Yote haya yanaweza kuwa suluhu ya muda mfupi tu, lakini baadaye hamu hurudi kwa nguvu mara kumi zaidi kuliko mwanzo. Haiwezekani kutatua tatizo la kiroho kwa njia za kimwili. Ushahidi mwepesi ni pale unaposikia watu wameingia kwenye ndoa lakini bado wameshindwa kuacha tabia hiyo.
Chanzo cha maamuzi
Ni muhimu sana kwa mwanadamu kuelewa jinsi mfumo wake wa maisha ulivyokuwa designed. Mwanadamu kiasili ameumbwa kujiongoza ama kufanya maamuzi kutokea ndani (rohoni) na sio nje (mwilini). Tuone maana ya kufanya maamuzi kiroho na kimwili:
Maamuzi ya mwilini vs rohoni
Mungu alipomuumba mwanadamu alimpulizia pumzi ya uhai, akawa nafsi hai. Hiyo ndio roho yake mwenyewe, ambayo ilikuwa na mfano wake. Kwa hiyo lilikuwa kusudi la Mungu mwanadamu aitawale duniani kwa kutumia
kanuni zake, kwa kuongozwa na roho. Ndivyo walivyoishi Adam na Hawa. Sasa angalia kisa hiki cha Adamu na dhambi ya kwanza;
Mwanzo 3
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
⁵ kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
>>> Tujiulize kwanza, kwani wakati wa kuumbwa kwao, Adam na Hawa walikuwa vipofu? Iweje nyoka aseme WATAFUMBULIWA MACHO? Kama waliumbwa wakiwa na macho, basi kuna macho tofauti na haya ya mwili.
Tena anashawishi kuwa watakuwa kama Mungu, kwa sababu watajua MEMA NA MABAYA. Kumbe kujua mema na mabaya ni kuwa kama Mungu, kwavipi? Mungu ndiye mwenye definition ya mambo mema na mabaya. Mwanadamu alipaswa kufuata kile tu anachoambiwa na Mungu, kupitia roho yake, kwa sababu Mungu ni Roho, hivi huwasiliana katika roho. Kwa hiyo yote ambayo aliagiza Mungu ndio MEMA, nje ya hapo ni mabaya. Kama wewe ni wa Mungu basi yakupasa kuyajua mema tu, kwa kuongozwa na sauti yake, hiyo ndio katiba aliyopewa mwanadamu. Hata Yesu Kristo aliishi KWA MFUMO HUO:
(Yoh 8
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³⁸ Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.
³⁹ Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu.
…
⁴³ Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu.
…
⁴⁷ Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.)
Kristo hakuwahi kusema jambo isipokuwa amemsikia Mungu akisema, yaani ile adili yake ya kibinadamu aliyokuwa nayo hapa duniani iliishi kwa kusikiliza sauti ya Roho wa Mungu. Hakuongozwa kwa matukio ya nje ya mwili bali kile Roho alichomshuhudia ndicho alichokifanya.
Ndipo akawaambia Mafarisayo kuwa hawawezi kulisikia neno lake, sababu wao wanasikiliza kwa masikio ya mwili, wakati neno lake ni ROHO. Ndipo akasisitiza, aliye wa Mungu (aliye wa rohoni - Mungu ni Roho) ndiye pekee awezaye kuisikia sauti yake kwa sababu ni ya jinsi roho. Huo ndio mfumo wa maisha ya Kristo hapa duniani. Tuendelee....
⁶ Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
>>> Kwanza kabisa alimtilia shaka Mungu, kwamba alichowaambia ni uongo!! Kisha akasema katika macho ya awali yaliyokuwa ACTIVE toka kuumbwa kwake. Akatazama kwa macho ya nyama, AKAYAFUMBUA YAKAONA UPANDE WA PILI WA MAISHA. Ndipo akagundua kumbe lile tunda linavutia machoni. Jiulize kwa nini tangu mwanzo tunda lile halikuwahi kumvutia macho ingawa lilikuwapo bustanini? Macho ya nyama yalifungwaa kwa sababu waliongozwa na sauti ya ndani sio kile wakionacho.
⁷ Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Sasa tazama, iweje walipofumbuliwa macho ghafla wakagundua wako uchi? Ni kwa sababu tangu kuumbwa kwao hawakuwahi kutazama duniani kwa macho ya nyama, kwamba walikuwa wamezunguiwa na utukufu wa Mungu, hilo ndilo lilikuwa vazi lao. Nitakupa mfano mdogo tu ambao KILA MTU huvaa vazi hilo:
ni mara ngapi umekuwa ukiota ndoto umevaa nguo wakati ULILALA UKIWA UCHI? Unadhani nguo hizo hutoka wapi? Kisha ukiamka, kumbe uko uchi wa nyama ndani ya shuka!!
Ndivyo ilivyokuwa kwa Adam na Hawa. Walipoteza vazi la haki ya Mungu ndipo macho yakafunguka, wakaanza kuitazama duniani kwa nje. Dhambi ilifukuza ya Mungu iliyokuwa vazi lao:
(Ayubu 29 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.
¹⁵ Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.
*********
Zaburi 132
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Ee Bwana, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako.
⁹ Makuhani wako na wavikwe haki), Watauwa wako na washangilie.)
Ziko aya nyingi mno!! Hilo ndilo lilikuwa vazi la Adam na Hawa bustanini. Tuendelee.....
⁸ Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
⁹ Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
¹⁰ Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
¹¹ Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Nadhani umepata picha, nini kilichoendelea bustanini. Baada ya kula tunda, haki ikapotea, wakajiona wako uchi, kwamba tayari wameamsha macho ya mwilini, akili ikaanza KUFANYA REASONING kwa kutokana na kile wanachokiona, ndivyo ilivyo hata leo!! Sauti ya Mungu ikafifia ndani ya mwanadamu, sauti ya nje ikatawala (ndio vitu vituvutiavyo tuvionapo). Sauti kama starehe, tafiti mbalimbali, nk macho yakapata nguvu, ya kuona yanavutia na kuamua kwamba jambo fulani ni jema na lafaa kuliwa, kisha huipelekea nafsi nayo hula. Mungu akapoteza nafasi yake ndani ya mwanadamu, NDIPO MWANADAMU ALIPOANZA KUFANYA MAAMUZI TOKA NJE, SIO ROHONI. Ndipo tukapata vitu kama LOGIC, kwamba tuaamue wenyewe kipi ni chema na kipi ni kibaya, katika hilo hatuhitaji tena kuwa na Mungu atuamulie. Yesu Kristo ingawa alikuwa mwanadamu kamili kama sisi, hakuongozwa na logic yake mwenyewe kama mwanadamu bali ALISIKILIZA LOGIC YA MUNGU toka ndani kisha akaaply nje. Ndio maana alikuwa na matokeo positive kwa kila jambo!!
Sasa maamuzi ya mwilini ni kama uzinzi, ulevi, kupiga punyeto, kuwadhuru wengine nk. Katika hayo hakuna Roho wa Mungu. New agers wamekuja na siri hii lakini wakaitumia kwa jinsi ya giza, ndio tunapata vitabu kama the power of positive thinking, the power of subconscious mind nk. Ndipo huku tunapata mambo ya astral projection, levitation nk. Hayo yote ni mbinu za shetani kuwaingiza wanadamu kwenye nguvu za giza. HIZO NDIZO NGUVU ZA GIZA ZENYEWE.
Badili chanzo chako cha maamuzi
Itaendelea..............
Morg, Nature,
Maya Angelou, Africa Tanzania, dumbi, LOGARITHM, Sergei Lavrov, LOVE U JF, korino, Mshuza2, park don, Surya, big-diamond, Mwanamena, Tajiri wa Magomeni, dudupori, Bubolwa Chura, Patra31, Depal, alumn, Ed Kawiche, Sexless, The 13, Avriel, Styles
yna2, ngebo, iMind, HoneyBee, Will jr, gbmm, True Believer, Saint Anne[/i][/B][/B], gilldenu, Bilionea Asigwa, online24, stephot
Amina, barikiwa nawe mkuuHii mistari ya kitabu cha mwanzo kuhusu uumbaji ni mistari maarafu sana. Wengu tunaijua. Lakini tunajuaga ni story tuu tunasimuliwa kuhusu uumbaji. Kumbe kunae watu wanaichambua deep namna hii.
Leo najikuta nmeelewa vizuri saaana maandiko haya... ubarikiwe sir
Samahani mkuu kumbe umebase kidini,BADILI CHANZO CHAKO CHA TAARIFA
Wakuu, mimi ninaandika kwa kufuata misingi ya neno la Mungu. Wako wadau kadha wa kadha wamesimama ili kunipinga pasipo kuleta hoja za kujadili. Sasa sio kila mtu anaweza kuupokea ujumbe wa ufalme wa Mungu. Nitaanza kwa kutazama hili kwa kifupi...
Mathayo 13
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁰ Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
¹¹ Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
Wakuu, kama tungefundishwa habari hizi toka awali tusingekuwa hapa tulipo hivi leo. Mungu anaongea nasi hata leo kwa njia ya Mwana wake. Sasa wanafunzi wake wakiwa bado hawajaelewa hasa kusudi la Kristo waliuliza swali hili, wakishangazwa kwa jinsi anavyotumia lugha ya mifano. Kristo alisema wazi kuwa walio wake wamejaliwa kuzijua siri za UFALME WA MBINGUNI, kama ilivyokuwa kwa hao wanafunzi wake. Lakini hawa waliokuwa pembeni wakimsikiliza na kubishana naye (mfano Mafarisayo) hawakujaliwa kuijua kweli.
Sasa kuanzia leo fahamuni kwamba fundisho hili ndio MSINGI MKUU wa kuisikia sauti ya Mungu maishani mwako. Usipotoshwe tena na ASALI YA MACHO YA ROHONI, nk. Mifano ambayo Yesu alisema ilihusu siri za ufalme. Sasa kwa mwanadamu wa kawaida mafundisho haya yalikuwa ni upuuzi mkubwa, ndio maana yakaitwa SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI.
Nimesema ndio msingi wa kuisikia sauti ya Mungu kwa sababu, KAMA VILE KRISTO ALIVYOONGEA NA WANAFUNZI WAKE KWA MIFANO, ndivyo Mungu anavyoongea nawe leo kwa mifano!! How? Umewahi kujiuliza ni mara ngapi imelala halafu unapoamka, kumbe umeota ndoto usiyoielewa maana? Ni mara ngapi unewaeleza jamaa zako na marafiki wqkusaidie maana ya ndoto yako? SASA FUNGUA AKILI YAKO LEO. Mungu amesema wazi kuwa ni mtumishi wake MUSA PEKEE ndiye aliongea naye WAZI WAZI, lakini soma kwa habari za manabii na wengine wote, aliongea nao kwa njia ya ndoto:
Hesabu 12
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁶ Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.
⁷ Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
⁸ Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Kumbe wanaoweza kuelewa maana ya ndoto ni wale WALIOJALIWA, kwa maana ndoto hufunua siri za ufalme wa Mungu. Siri zipi? Mambo yaliyopita tusiyoelewa yalitokeaje, mambo yaliyopo na yale yatakayokuwapo ingawa hatuwezi kuyaona mpaka yatokee. Ndipo ilipo roho ya unabii hapo!!
[/I]¹² Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.[/I]
Sasa ukiwa na kitu utapewa tele. Yaani ukiwa na neno ndani yako, basi utazidishiwa tele, hata kuzijua siri za ufalme. Tazama andiko hili liko kwenye mfano wa mpanzi, ndipo ilipoandikwa mbegu ni NENO LA MUNGU (sio fedha mzazopanda makanisani). Ukiwa na neno ambalo limeanguka kwenye udongo mzuri, LITAKUZALIA MATUNDA, kwamba utazidishiwa na vingine kama ndoto, maono na mafunuo. Ndipo Mungu huzungumza kwa ndoto na hivyo unahitaji neno la Mungu KUZITAFSIRI.
¹³ Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
¹⁴ Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
Sasa Kristo alitumia kanuni ya ufalme wa mbinguni kusema kwa mifano. Hapo watakaosikia ni wale waliojaliwa tu, yaani wenye msingi wa kweli ya Mungu. Wengine hata uwahubiri vipi, hata waote ndoto vipi hawawezi kamwe kuiona kweli. Kumbuka mfano wa maskini Lazaeo na tajiri, Yesu alisema HATA AKIFUFUKA MTU hawawezi kamwe kumwamini. Walio wa Mungu wala hawahitaji miujiza ili KUAMINI kwa sababu wana neno ndani yao. Angalia sana usiwe kama msukule mfuata miujiza, muabudu miungu!!
¹⁵ Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Kumbe sisi wenyewe tumeyafumba macho yetu ili tusione, tukaziba masikio tusisikie kweli ya Mungu tusije ponywa. Sasa macho na masikio yaliyifumbwa ni yapi? Macho na masikio ya rohoni. Tumeamua kutazama kwa macho ya mwilini na kwa hayo twafanya hukumu zetu!! Lakini neno la Kristo ni la jinsi ya rohoni na sio mwilini. Kumbe HUWEZI KAMWE KUISIKIA KWELI YA MUNGU KAMA UNASIKILIZA KWA JINSI YA MWILI. Ndio imani za mazoea hizi, zimewekwa kwa jinsi ya kimwili.
¹⁶ Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.
Ni heri kwako kama Unaona na kusikia kwa jinsi ya rohoni. Utaona na kusikia kwa njia ya ndoto, amini nakwwmbia siku ukiijua siri hii basi huwezi kamwe kushangazwa na tukio lolote maishani mwako. Acha habari za kununua vitabu vya kutafsiri ndoto kwani NDOTO ZOTE ZA UFALME HUJA KWA JINSI YA NENO LA MUNGU. Leo siko kwenye somo la ndoto bali naongea kwa habari ya wale wanaopinga pasipokuwa na msingi wa neno la Mungu.
Neno la Mungu limeandikwa kwa jinsi ya MIFANO, limeandikwa kama fumbo ambalo ukijibidiisha kuutafuta uso wa Mungu utapata kuluona WAZI WAZI. Iko siku nitaongea kwa habari ya 1. Uumbaji katika kitabu cha Mwanzo 2. Kunena kwa lugha 3. Jinsi ya kutafsiri ndoto zako mwenyewe 4. Jinsi ya kuzungumza na Mungu kwa habari zako mwenyewe naye akaongoza maisha yako.
Biblia ni kitabu cha kiroho, ndicho kitabu pekee nikijuacho mimi ambacho KAMA UTAKISOMA KATIKA ROHO, basi utagundua kwamba chenyewe ndio KINAKUSOMA WEWE!! Kama bado unaisoma Biblia kama novel, basi haujaisomq katika roho. Mtafute Mungu katika Roho na kweli, nawe utamwona maadam yu karibu.
Amina.
Leo nitaelezea zaidi sasa jinsi ya kujitoa kwenye MTEGO WA PUNYETO, tega sikio lako.
Huu uzi is too much deep and helpful.! Mungu akubariki Nyenyere.Warumi 8 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³ Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
⁴ ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
⁵ Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
⁶ Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
⁷ Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
⁸ Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
⁹ Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
¹⁰ Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
¹¹ Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
¹² Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,
¹³ kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
¹⁴ Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Renewal of mind - Kubadili niaBADILI CHANZO CHAKO CHA TAARIFA
Wakuu, mimi ninaandika kwa kufuata misingi ya neno la Mungu. Wako wadau kadha wa kadha wamesimama ili kunipinga pasipo kuleta hoja za kujadili. Sasa sio kila mtu anaweza kuupokea ujumbe wa ufalme wa Mungu. Nitaanza kwa kutazama hili kwa kifupi...
Mathayo 13
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁰ Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
¹¹ Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
Wakuu, kama tungefundishwa habari hizi toka awali tusingekuwa hapa tulipo hivi leo. Mungu anaongea nasi hata leo kwa njia ya Mwana wake. Sasa wanafunzi wake wakiwa bado hawajaelewa hasa kusudi la Kristo waliuliza swali hili, wakishangazwa kwa jinsi anavyotumia lugha ya mifano. Kristo alisema wazi kuwa walio wake wamejaliwa kuzijua siri za UFALME WA MBINGUNI, kama ilivyokuwa kwa hao wanafunzi wake. Lakini hawa waliokuwa pembeni wakimsikiliza na kubishana naye (mfano Mafarisayo) hawakujaliwa kuijua kweli.
Sasa kuanzia leo fahamuni kwamba fundisho hili ndio MSINGI MKUU wa kuisikia sauti ya Mungu maishani mwako. Usipotoshwe tena na ASALI YA MACHO YA ROHONI, nk. Mifano ambayo Yesu alisema ilihusu siri za ufalme. Sasa kwa mwanadamu wa kawaida mafundisho haya yalikuwa ni upuuzi mkubwa, ndio maana yakaitwa SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI.
Nimesema ndio msingi wa kuisikia sauti ya Mungu kwa sababu, KAMA VILE KRISTO ALIVYOONGEA NA WANAFUNZI WAKE KWA MIFANO, ndivyo Mungu anavyoongea nawe leo kwa mifano!! How? Umewahi kujiuliza ni mara ngapi imelala halafu unapoamka, kumbe umeota ndoto usiyoielewa maana? Ni mara ngapi unewaeleza jamaa zako na marafiki wqkusaidie maana ya ndoto yako? SASA FUNGUA AKILI YAKO LEO. Mungu amesema wazi kuwa ni mtumishi wake MUSA PEKEE ndiye aliongea naye WAZI WAZI, lakini soma kwa habari za manabii na wengine wote, aliongea nao kwa njia ya ndoto:
Hesabu 12
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁶ Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.
⁷ Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
⁸ Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Kumbe wanaoweza kuelewa maana ya ndoto ni wale WALIOJALIWA, kwa maana ndoto hufunua siri za ufalme wa Mungu. Siri zipi? Mambo yaliyopita tusiyoelewa yalitokeaje, mambo yaliyopo na yale yatakayokuwapo ingawa hatuwezi kuyaona mpaka yatokee. Ndipo ilipo roho ya unabii hapo!!
[/I]¹² Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.[/I]
Sasa ukiwa na kitu utapewa tele. Yaani ukiwa na neno ndani yako, basi utazidishiwa tele, hata kuzijua siri za ufalme. Tazama andiko hili liko kwenye mfano wa mpanzi, ndipo ilipoandikwa mbegu ni NENO LA MUNGU (sio fedha mzazopanda makanisani). Ukiwa na neno ambalo limeanguka kwenye udongo mzuri, LITAKUZALIA MATUNDA, kwamba utazidishiwa na vingine kama ndoto, maono na mafunuo. Ndipo Mungu huzungumza kwa ndoto na hivyo unahitaji neno la Mungu KUZITAFSIRI.
¹³ Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
¹⁴ Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
Sasa Kristo alitumia kanuni ya ufalme wa mbinguni kusema kwa mifano. Hapo watakaosikia ni wale waliojaliwa tu, yaani wenye msingi wa kweli ya Mungu. Wengine hata uwahubiri vipi, hata waote ndoto vipi hawawezi kamwe kuiona kweli. Kumbuka mfano wa maskini Lazaeo na tajiri, Yesu alisema HATA AKIFUFUKA MTU hawawezi kamwe kumwamini. Walio wa Mungu wala hawahitaji miujiza ili KUAMINI kwa sababu wana neno ndani yao. Angalia sana usiwe kama msukule mfuata miujiza, muabudu miungu!!
¹⁵ Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Kumbe sisi wenyewe tumeyafumba macho yetu ili tusione, tukaziba masikio tusisikie kweli ya Mungu tusije ponywa. Sasa macho na masikio yaliyifumbwa ni yapi? Macho na masikio ya rohoni. Tumeamua kutazama kwa macho ya mwilini na kwa hayo twafanya hukumu zetu!! Lakini neno la Kristo ni la jinsi ya rohoni na sio mwilini. Kumbe HUWEZI KAMWE KUISIKIA KWELI YA MUNGU KAMA UNASIKILIZA KWA JINSI YA MWILI. Ndio imani za mazoea hizi, zimewekwa kwa jinsi ya kimwili.
¹⁶ Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.
Ni heri kwako kama Unaona na kusikia kwa jinsi ya rohoni. Utaona na kusikia kwa njia ya ndoto, amini nakwwmbia siku ukiijua siri hii basi huwezi kamwe kushangazwa na tukio lolote maishani mwako. Acha habari za kununua vitabu vya kutafsiri ndoto kwani NDOTO ZOTE ZA UFALME HUJA KWA JINSI YA NENO LA MUNGU. Leo siko kwenye somo la ndoto bali naongea kwa habari ya wale wanaopinga pasipokuwa na msingi wa neno la Mungu.
Neno la Mungu limeandikwa kwa jinsi ya MIFANO, limeandikwa kama fumbo ambalo ukijibidiisha kuutafuta uso wa Mungu utapata kuluona WAZI WAZI. Iko siku nitaongea kwa habari ya 1. Uumbaji katika kitabu cha Mwanzo 2. Kunena kwa lugha 3. Jinsi ya kutafsiri ndoto zako mwenyewe 4. Jinsi ya kuzungumza na Mungu kwa habari zako mwenyewe naye akaongoza maisha yako.
Biblia ni kitabu cha kiroho, ndicho kitabu pekee nikijuacho mimi ambacho KAMA UTAKISOMA KATIKA ROHO, basi utagundua kwamba chenyewe ndio KINAKUSOMA WEWE!! Kama bado unaisoma Biblia kama novel, basi haujaisomq katika roho. Mtafute Mungu katika Roho na kweli, nawe utamwona maadam yu karibu.
Amina.
Leo nitaelezea zaidi sasa jinsi ya kujitoa kwenye MTEGO WA PUNYETO, tega sikio lako.
Renewal of mind - Kubadili nia
Wakuu, leo tuna turudi ili tujifunze ni jinsi gani hasa ya kujitoa kutoka kwenye mtego huu dhalimu wa ibilisi. Ni vema kutambua kuwa tumeingia huko kwa sababu ya mazingira yanayomzunguka. Tunasikia masimulizi ya vijana wenzetu kuhusu utamu wa punyeto na kujichua, tunatazama picha za uchi zinazopelekea kuamsha hamu ndani yetu, tunatazama vipindi vya TV vyenye kurukuza mambo ya ngono, tunasikiliza miziki inayosifia ngono, tunazungukwa na wanawake wanaovaa kwa jinsi ya kuamsha hamasa ya ngono, tunaishi katika ya wanaume ambao watatongoza mpaka mbwa mradi yuko mbele yao nk.
Sasa jumla ya mambo yote haya ndicho kilichojaa mioyoni mwetu. Mwili hujazwa hisia za mapenzi tangu tukiwa watoto. Sasa matokeo yake ndio hawa wakuu wanaodai kuwa haiwezekani tena kujizuia kufanya sex, vinginevyo mtu ajichue!! Kwamba nikiwashauri vijana kuepuka tendo hili baya kabisa, yabidi niwaeleze watazipeleka wapi nyege zao. Ni kweli kabisa, haiwezekani kuacha tabia hii kama hujabadili yale yaingiayo moyoni. Ni sawa na kuandika nguo ndani ya maji ukitarajia itakuwa. Utakuwa unaitoa unaikamua, inakupa matumaini kwamba itakuwa, kisha unaianika ndani ya pipa lililojaa maji. Pasipo kubadili mazingira yako, yaani kwenda kinyume na mfumo wa awali, huwezi kamwe kukishinda kifungo hiki.
Warumi 12
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Itoeni miili yenu iwe dhabihu - neno dhabihu lina maana ya SACRIFICE - sadaka ya kuteketezwa. Kwa hiyo yatupasa kwanza kuwa tayari kuitoa MIILI yetu (sio roho) kuiteketeza kama sadaka kwa ajili ya Mungu wetu. Maana yake ni kwamba tuishi kwa ajili ya kusudi lake na si kwa kufuata kusudi la dunia hii, mafundisho mbalimbali ambayo hayana asili ya Mungu (ndio asili ya kuumbwa kwetu, kupiga punyeto, kujichua, kusagana nk. sio asili ya kuumbwa mwanadamu).
Ndio tunaambiwa TUSIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII, ndio mawazo ya hao wanaodai kuna raha kwenye mambo yasio ya asili. Huku ni kujidanganya, ni sawa na raha iliyomo kwenye madawa ya kulevya lakini sote twqjua mwisho wake. Tena msisitizo ni kwenye KUBADILI NIA - RENEWAL OF MIND. Katika mambo yote, chunga sana moyo wako, ndimo yatokamo maamuzi yote. Sasa nia zetu zimewekwa kuendana na mfumo wa dunia SIO KWA ASILI YA KUUMBWA, bali kutokana na ushawishi wa dunia. Zamani tuliamini mwanamke mrembo ni mwembamba, ndio kina dada wakawa wanajinyima kula ili kujikondesha, ingawa leo wqkiambiwa wajinyime vivyo hivyo kwa ajili ya ufalme wa Mungu linakuwa jambo gumu na zito!! Zikaja zama za MISS BANTU, zikqja zama za kuchubua uso na mikono, kisha leo tuna mchanganyiko, weupe na unene na matako makubwa, ndicho kipimo cha urembo. Haya yote si kwa namna ya asili, kwani asili ni jinsi mtu alivyotoka tumboni mwa mama yake, zaidi ya hapo ni kitumikia mfumo wa dunia hii.
Kiuhalisia tumekubali kuwa watumwa, ndio maana maisha yetu tumeyaweka kujaribu kufikia kilele cha kuifurahisha dunia, tunaishi kutafuta sifa za nje huku tukiua kabisa kusudi la Mungu ambalo ni roho yake iliyo ndani yetu. Hatufanyi maamuzi kwa kusikiliza sauti ya ndani bali twaenenda kwa kuona. Tuliumbwa kuwa PROACTIVE lakini sasa tumeinamishwa chini na kukubali kuwa REACTIVE, yaani tunaamua baada ya kuona tukio, sio kuamua kabla tukio halijawa. Tumekufa kiroho, hivyo imetupasa ku-flash yale yote yaliyomo ndani yetu tuwe na nia mpya, nia ambayo ni tofauti na mwenendo wa dunia hii. Nafikiri mpaka hapa tumegundua ni kwa nini Biblia inasema URAFIKI NA DUNIA NI UADUI NA MUNGU!!
[]Tito 3
3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;[/I]
Kwa hiyo maisha ambayo tunayaishi sasa kwa kufuata namna ya dunia hii ni UONGO, tumedanganywa na kujikuta tukitumikia anasa za namna nyingi. Tumetekwa nia zetu hatu hatufikiri nje ya kile kilichoandaliwa na dunia.
Tumeokolewa na KUFANYWA UPYA, ndio kubadilishwa nia zetu na sasa tunatumikia nia ya Kristo. Hapo ndipo ilipo maana halisi ya kuzaliwa mara ya pili, KUUA MWILI UNAOTUMIKIA MAMBO YA DUNIA kisha kuzaliwa na mwili mpya wenye kutumikia kusudi la Mungu. Kwamba hatuendi tena sawa sawa na mfumo wa dunia hii. Kristo alisema mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kamwe kuuingia ufalme wa Mungu. Kwamba usipousulubisha mwili, yaani kuutoa kuwa sadaka ya kuteketezwa, kisha ukaifufua roho yako iliyosinzia ili ichukue uongozi, haiwezekani kamwe kuingia kwenye ufalme. Mungu ni roho, ndio maana hata tukifa mwili hubaki hapa duniani na na roho hurejea kwa muumba wake. Kumbe kidumucho ni roho nayo ndio yapaswa kuwa kiongozi, mwili ni housing tu, iwwjw basi tutumikie kisichodumu?
Warumi 8
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Sasa aichunguzaye mioyo ni Mungu, tukiruhusu kuongozwa na roho tokea ndani, maana yake Roho wa Mungu atakaa ndani yetu na kutufundisha yote yatupasayo. Tena mwili wa nje hautakuwa na nguvu kwetu kwa sababu Roho wa Mungu anajua NIA YETU, kwamba tumedhamiria kuacha PUNYETO NA KUJICHUA. Yeye anajua jinsi ya kutuombea hilo na siis tutashinda kabisa. Hili ni janga la kiroho, hivyo hatuwezi kamwe kulishinda kwa juhudi za kimwili, haiwezekani!!
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake
“And we know that all things work together for good to them that love God, to them who are the called according to his purpose.”
— Romans 8:28
Napenda kutumia tafsiri ya Kiingereza kwani inaleta maana halisi iliyokusudiwa. Kwamba:
"nasi twajua kwamba mambo yote hufanya kazi pamoja kwa ajili ya mema, kwao wampendao Mungu, kwa wale walioitwa kwa kusudi lake."
Mambo yote aliyowekewa mwanadamu hufanya kazi kwa ushirikiano ili kumpatia mema. Sasa mambo kama punyeto na kujichua hayana ushirikiano sawia wa mwili na roho, ndio maana yanaleta madhara. Lakini tukimpenda Mungu tutasimamia kusudi lake kwetu nasi tutavuna mema, wala hatutatawaliwa na tamaa za dunia hii.
1 Wakorintho 6
12 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.
13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.
14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.
Mwili haukuumbwa kutumikia zinaa, bali ni kwa Bwana, kwamba mwili umepaswa kutii kusudi la Mungu, sio mwili kuitiisha roho. Mungu alitupa roho ili iutawale mwili, lakini mwanadamu amegeuza mwili ndio unaoendesha roho. Vitu vyote ni halali kabisa kwa mwili, ukitaka kuzini waweza, ukitaka kupiga punyeto waweza nk. Lakini hilo sio kusudi la mwili.
15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
Kufanya zinaa, kujichua, kupiga punyeto nk ni kuutumia mwili wa Mungu kutekeleza hamu zako. Kama ukilala na kahaba tayari mmekuwa mwili mmoja, ni kwa vipi? Ni kwa sababu nafsi zenu zimeungana, katika ulimwengu wa roho ninyi ni wamoja. Kumbe aya hii haizungumzii mambo ya mwilini kulalana na kumwaga shahawa, bali ni kile kinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho. Tendo la nje linadhihirisha tendo la rohoni ambalo limekwisha kufanyika.
Sasa mpiga punyeto na mchuaji walidhani wako salama. Katika mwili unamwaga nje kama udhihirisho tu kuwa tayari iko entity ya kiroho umeungana nayo ili kukamilisha tendo. Umevuta hisia ukajisikia ni kama una sex na mtu mwingine hata kufikia kilele. Tayari umekuwa mwili mmoja nanyi ni mahaba, na mapepo mengine.
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Katika DHAMBI ZOTE NDANI YA BIBLIA ni dhambi moja tu ambayo tumeambiwa tuikimbie, ZINAA. Dhambi zote hufanyika NJE YA MWILI, kwa maana kwamba sio dhambi za kiroho ingawa matokeo yake huichafua roho. Uzinzi ni dhambi ya kiroho kwa sababu, kabla halijatukia ni lazima roho zenu ZIUNGANE KUNIA MAMOJA, kwamba kweli tujifiche sehemu tulale kama mke na mume. Dhambi hii ni sawa na kufanya mapenzi NYUMBANI MWA MUNGU!! Mwili ni nyumba ya Roho Mtakatifu, haukuumbwa ili kufuata matakwa ya dunia. Kwa hiyo inabidi kumpa notisi kwanza aondoke ili kuala bata!! Kisha akiondoka ndipo roho wachafu huchukua uongozi wa maisha na hapo maisha ya mtu hubadilika. Ona ndoa zinavyoyumba kwa sababu ya uzinzi, ona kesi nyingi mahakamani ni kuhusu mashauri ya ndoa, uzinzi!!
Sasa wewe Mpiga punyeto na unayejichua, unafanya zinaa na mapepo kwa sababu tendo hili ni la kiroho. Kimwili uko peke yako lakini kiroho umejitwalia mpenzi ambaye ni pepo. Kisha ni vema tujue kifungo cha ngono ni kibaya kuliko. Hilo ni agano lenye nguvu kubwa katika ulimwengu wa roho, hivyo unapojichua na unaimarisha agano hilo.
IKIMBIENI ZINAA - ndugu zangu, dhambi ya zinaa haina mjadala, KIMBIA!! Huna nguvu ya kujadiliana na pepo la ngono kwani ukiruhusu mazingira hayo hakika utaanguka!! Ndivyo ilivyo kwa wazee wa punyeto! Labda niseme tu, neno lililotumika hapa kwenye "zinaa" ni PORNEIA ambalo hujumuisha uzinzi, kulala na wanyama, kujichua nk. Haya yote yatupasa kuyakimbia.
>>> Leo tumejenga msingi wa jinsi fikra zetu zinapaswa kuwa, kisha sasa tutaingia kwenye hatua zenyewe za kuishinda dhambi ya kupiga punyeto na kujichua.
Mbarikiwe nyote
Well taught mr Nyenyere.!Renewal of mind - Kubadili nia

Mbarikiwe nyote.
Morg, Nature, Maya Angelou, Africa Tanzania, dumbi, LOGARITHM, Sergei Lavrov, LOVE U JF, korino, Mshuza2, park don, Surya, big-diamond, Mwanamena, Tajiri wa Magomeni, dudupori, Bubolwa Chura, Patra31, Depal, alumn, Ed Kawiche, Sexless, The 13, Avriel, Styles, yna2, ngebo, imind, HoneyBee, Will jnjr, @jbmm, True Believer, @Sainr Anne, Recu, Bilionea Asigwa, youngkato, Clinker belite
por-ni'-ah Noun FeminineAmen..umenifungua macho hapo mwishoni kwenye neno PORNEIA..kumbe neno zinaa kibiblia ni pana sana...huenda lugha yetu ina mapungufu...imetudhulumu baadhi ya contents.