Ufanye nini?
Wadau wengi sana wamefikia hatua ya kuhoji wafanye nini ili kutoka katika hali ya kujichua. Zingatia kwamba madhara haya yapo kwa wanawake na wanaume pia, hivyo hapa tunatazama pande zote. Leo nitaandika kifupi tu kuhusu suluhisho la kudumu la tatizo hili.
Kujichua ni tatizo la kiroho
Nilianza kufafanua kiini cha tatizo hili ili kufuta kabisa ile dhana kwamba ni tatizo la nje tu, yaani la kimwili na kujaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani tatizo hili limejikita upande wa roho zaidi kuliko mwili. Kutambua kuwa tatizo hili ni la kiroho ni hatua muhimu mno katika kutafuta suluhu yake. Sasa basi, ili kung'oamzizi wa fitina, usitarajie kusuluhisha kwa kutazama mambo ya mwilini.
Yako mapendekezo mengi ambayo yamekuwa yakitolewa kama suluhu ya tatizo la kujichua, shidani kwamba yote hulenga suluhu ya kimwili. Mfano, acha kukaa peke yako, tafuta mpenzi, usitazame picha za ngono nk. Yote haya yanaweza kuwa suluhu ya muda mfupi tu, lakini baadaye hamu hurudi kwa nguvu mara kumi zaidi kuliko mwanzo. Haiwezekani kutatua tatizo la kiroho kwa njia za kimwili. Ushahidi mwepesi ni pale unaposikia watu wameingia kwenye ndoa lakini bado wameshindwa kuacha tabia hiyo.
Chanzo cha maamuzi
Ni muhimu sana kwa mwanadamu kuelewa jinsi mfumo wake wa maisha ulivyokuwa designed. Mwanadamu kiasili ameumbwa kujiongoza ama kufanya maamuzi kutokea ndani (rohoni) na sio nje (mwilini). Tuone maana ya kufanya maamuzi kiroho na kimwili:
Maamuzi ya mwilini vs rohoni
Mungu alipomuumba mwanadamu alimpulizia pumzi ya uhai, akawa nafsi hai. Hiyo ndio roho yake mwenyewe, ambayo ilikuwa na mfano wake. Kwa hiyo lilikuwa kusudi la Mungu mwanadamu aitawale duniani kwa kutumia
kanuni zake, kwa kuongozwa na roho. Ndivyo walivyoishi Adam na Hawa. Sasa angalia kisa hiki cha Adamu na dhambi ya kwanza;
Mwanzo 3
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
⁵ kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
>>> Tujiulize kwanza, kwani wakati wa kuumbwa kwao, Adam na Hawa walikuwa vipofu? Iweje nyoka aseme WATAFUMBULIWA MACHO? Kama waliumbwa wakiwa na macho, basi kuna macho tofauti na haya ya mwili.
Tena anashawishi kuwa watakuwa kama Mungu, kwa sababu watajua MEMA NA MABAYA. Kumbe kujua mema na mabaya ni kuwa kama Mungu, kwavipi? Mungu ndiye mwenye definition ya mambo mema na mabaya. Mwanadamu alipaswa kufuata kile tu anachoambiwa na Mungu, kupitia roho yake, kwa sababu Mungu ni Roho, hivi huwasiliana katika roho. Kwa hiyo yote ambayo aliagiza Mungu ndio MEMA, nje ya hapo ni mabaya. Kama wewe ni wa Mungu basi yakupasa kuyajua mema tu, kwa kuongozwa na sauti yake, hiyo ndio katiba aliyopewa mwanadamu. Hata Yesu Kristo aliishi KWA MFUMO HUO:
(Yoh 8
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³⁸ Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.
³⁹ Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu.
…
⁴³ Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu.
…
⁴⁷ Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.)
Kristo hakuwahi kusema jambo isipokuwa amemsikia Mungu akisema, yaani ile adili yake ya kibinadamu aliyokuwa nayo hapa duniani iliishi kwa kusikiliza sauti ya Roho wa Mungu. Hakuongozwa kwa matukio ya nje ya mwili bali kile Roho alichomshuhudia ndicho alichokifanya.
Ndipo akawaambia Mafarisayo kuwa hawawezi kulisikia neno lake, sababu wao wanasikiliza kwa masikio ya mwili, wakati neno lake ni ROHO. Ndipo akasisitiza, aliye wa Mungu (aliye wa rohoni - Mungu ni Roho) ndiye pekee awezaye kuisikia sauti yake kwa sababu ni ya jinsi roho. Huo ndio mfumo wa maisha ya Kristo hapa duniani. Tuendelee....
⁶ Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
>>> Kwanza kabisa alimtilia shaka Mungu, kwamba alichowaambia ni uongo!! Kisha akasema katika macho ya awali yaliyokuwa ACTIVE toka kuumbwa kwake. Akatazama kwa macho ya nyama, AKAYAFUMBUA YAKAONA UPANDE WA PILI WA MAISHA. Ndipo akagundua kumbe lile tunda linavutia machoni. Jiulize kwa nini tangu mwanzo tunda lile halikuwahi kumvutia macho ingawa lilikuwapo bustanini? Macho ya nyama yalifungwaa kwa sababu waliongozwa na sauti ya ndani sio kile wakionacho.
⁷ Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Sasa tazama, iweje walipofumbuliwa macho ghafla wakagundua wako uchi? Ni kwa sababu tangu kuumbwa kwao hawakuwahi kutazama duniani kwa macho ya nyama, kwamba walikuwa wamezunguiwa na utukufu wa Mungu, hilo ndilo lilikuwa vazi lao. Nitakupa mfano mdogo tu ambao KILA MTU huvaa vazi hilo:
ni mara ngapi umekuwa ukiota ndoto umevaa nguo wakati ULILALA UKIWA UCHI? Unadhani nguo hizo hutoka wapi? Kisha ukiamka, kumbe uko uchi wa nyama ndani ya shuka!!
Ndivyo ilivyokuwa kwa Adam na Hawa. Walipoteza vazi la haki ya Mungu ndipo macho yakafunguka, wakaanza kuitazama duniani kwa nje. Dhambi ilifukuza ya Mungu iliyokuwa vazi lao:
(Ayubu 29 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴
Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.
¹⁵
Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.
*********
Zaburi 132
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Ee Bwana, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako.
⁹
Makuhani wako na wavikwe haki), Watauwa wako na washangilie.)
Ziko aya nyingi mno!! Hilo ndilo lilikuwa vazi la Adam na Hawa bustanini. Tuendelee.....
⁸ Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
⁹ Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
¹⁰ Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
¹¹ Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Nadhani umepata picha, nini kilichoendelea bustanini. Baada ya kula tunda, haki ikapotea, wakajiona wako uchi, kwamba tayari wameamsha macho ya mwilini, akili ikaanza KUFANYA REASONING kwa kutokana na kile wanachokiona, ndivyo ilivyo hata leo!! Sauti ya Mungu ikafifia ndani ya mwanadamu, sauti ya nje ikatawala (ndio vitu vituvutiavyo tuvionapo). Sauti kama starehe, tafiti mbalimbali, nk macho yakapata nguvu, ya kuona yanavutia na kuamua kwamba jambo fulani ni jema na lafaa kuliwa, kisha huipelekea nafsi nayo hula. Mungu akapoteza nafasi yake ndani ya mwanadamu, NDIPO MWANADAMU ALIPOANZA KUFANYA MAAMUZI TOKA NJE, SIO ROHONI. Ndipo tukapata vitu kama LOGIC, kwamba tuaamue wenyewe kipi ni chema na kipi ni kibaya, katika hilo hatuhitaji tena kuwa na Mungu atuamulie. Yesu Kristo ingawa alikuwa mwanadamu kamili kama sisi, hakuongozwa na logic yake mwenyewe kama mwanadamu bali ALISIKILIZA LOGIC YA MUNGU toka ndani kisha akaaply nje. Ndio maana alikuwa na matokeo positive kwa kila jambo!!
Sasa maamuzi ya mwilini ni kama uzinzi, ulevi, kupiga punyeto, kuwadhuru wengine nk. Katika hayo hakuna Roho wa Mungu. New agers wamekuja na siri hii lakini wakaitumia kwa jinsi ya giza, ndio tunapata vitabu kama the power of positive thinking, the power of subconscious mind nk. Ndipo huku tunapata mambo ya astral projection, levitation nk. Hayo yote ni mbinu za shetani kuwaingiza wanadamu kwenye nguvu za giza. HIZO NDIZO NGUVU ZA GIZA ZENYEWE.
Badili chanzo chako cha maamuzi
Itaendelea..............
Morg,
Nature,
Maya Angelou,
Africa Tanzania,
dumbi,
LOGARITHM,
Sergei Lavrov,
LOVE U JF,
korino,
Mshuza2,
park don,
Surya,
big-diamond,
Mwanamena,
Tajiri wa Magomeni,
dudupori,
Bubolwa Chura,
Patra31,
Depal,
alumn,
Ed Kawiche,
Sexless,
The 13,
Avriel,
Styles
yna2,
ngebo,
iMind,
HoneyBee,
Will jr,
gbmm,
True Believer,
Saint Anne[/i][/B][/B],
gilldenu,
Bilionea Asigwa,
online24,
stephot